KONGAMANO LA VIJANA KASULU DC/KATIBU TAWALA WILAYA AZUNGUMZA

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 30 вер 2024
  • Vijana wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kuwa wazalendo kwa taifa lao kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria za nchi zilitowekwa ili kuwa na maendeleo endelevu katika jamii.
    Wito huo umetolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Kasulu Bi,Theresia Mtewele wakati akizungumza katika Kongamano la vijana halmashauri ya wilaya ya Kasulu lenye lengo la kuwajengea uwezo vijana na kuwapa elimu juu ya utawala bora na fursa za kimaendeleo zinazopatikana kwenye maeneo yao.
    Bi.Mtewele amesema wazazi na walezi wanapaswa kuwafundisha vijana stadi za maisha na uongozi ikiwa ni pamoja na namna ya kujiinua kiuchumi kwa kutumia fursa zinazowazunguka na kwamba hii itasaidia kupunguza vijana tegemezi katika jamii.

КОМЕНТАРІ • 1