CHALAMILA AWA MBOGO SAKATA LA WAFANYABIASHARA KARIAKOO, ATAKA MAJINA 891 YAFUTWE

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 11 лип 2024
  • Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Albert Chalamila ameagiza kuondolewa majina 891 ya wafanyabiashara yaliyowekwa kwenye mtandao wa Shirika la Masoko Kariakoo mpaka pale vyombo vya dola vitakapojiridhisha na majina hayo.
    Hatua hiyo inakuja baada ya wafanyabiashara zaidi ya 800 waliokuwepo sokoni hapo kabla ya soko kuungua Julai 2021 kuandamana jana Alhamisi, Julai 11, 2024 kwenda Ofisi za CCM Lumumba kupinga kutorejeshwa.
    Katika orodha hiyo, wafanyabiashara 891 kati ya 1,861 ndio walioelezwa kuwa na vigezo vya kurejea. Uamuzi huo uliwafanya kujitokeza katika viwanja vya Mnazi Moja kuhakikiwa na baada ya kutoridhishwa ndio wakaandamana.
    Chalamila ametoa maagizo hayo leo Ijumaa Julai 12, 2024, alipozungima na uongozi wa Shirika la Masoko Kariakoo katika Ofisi ya Shirika la Masoko Magogoni.

КОМЕНТАРІ • 14

  • @binsherbal6089
    @binsherbal6089 23 дні тому +5

    Hebu nyoosha maneno, Rais amelipa!!!??? Hapo hapo unasema ni Kodi zetu walalahoi!!!??? Amelipa Rais au tumelipa sisi? Hii kauli inakera sana, Kila kitu Rais kafanya Rais kafanya Rais anatoa wapi pesa? Mbona mambo yakiharibika hamsemi kama Rais kaharibu? Kila kitu ni Uchawa tu siku hizi.

  • @hamidabarraball3162
    @hamidabarraball3162 23 дні тому +3

    Yaani kila kiongozi akitoa hutuba lazima amtaje rais zaidi ya mara kumi, inatia aibu sana, tunaona nchi za wenzetu raisi hasifiwi kiasi hicho

  • @user-hi8le2vb7z
    @user-hi8le2vb7z 23 дні тому +1

    leo ajastua leo😊

  • @hudhaifamsafiri8731
    @hudhaifamsafiri8731 23 дні тому +1

    Kwan wakuu wetu hawawezi kufanya kazi bila kumuusisha Raisi

  • @gmdigitostore8550
    @gmdigitostore8550 23 дні тому

    Hapo safi. Kibano hicho.

  • @maimunaathumani9121
    @maimunaathumani9121 23 дні тому

    Kweli mkuu wengine pale kariakoo walisishana familia zima sisi twende wapi

  • @GeorgeSikazwe-mm7nn
    @GeorgeSikazwe-mm7nn 23 дні тому

    😂 hii nchi bhn..serikali nd inalipa ww

  • @faustinluambano2958
    @faustinluambano2958 23 дні тому

    Huyu naye.

  • @mbwanakiting7180
    @mbwanakiting7180 23 дні тому

    Tuliambiwa pesa katoa maamaa na serikalli sasa shirika limeweka mtaji gani?

  • @evamacha4861
    @evamacha4861 23 дні тому

    Mkuu wa mkoa nadhani unakumbuka soko la.mbagala zakgiem ulituuza sana kwa kutudanganya kuwa ukiona kuna mafisadi lakini ulitudanganya soko la zakhiem uliweka wafanyabiashara wapya badala ya wale waliopisha soko kujengwa.ulifanya dhambi kubwa sana bado tunalia machozi ya damu na mungu pekee ndio natafuta machozi yetu.

  • @user-tn7ic2ky3i
    @user-tn7ic2ky3i 23 дні тому

    Aneye lipa ni Samiya ao ni serikali acha uchawa

  • @user-xk7vy4gb6g
    @user-xk7vy4gb6g 23 дні тому

    Soko la ccm hilo

  • @hebronmwamwaja7660
    @hebronmwamwaja7660 23 дні тому

    Siyo ameripa tumeripa acheni ayo mambo ya uchawa tumeripa

    • @edsonnelson4464
      @edsonnelson4464 23 дні тому

      Amelipa tumelipa au tutalipa tusiharibiane kiswahili