INASIKITISHA!!..KONDAKTA APOTEZA MAISHA KWENYE AJALI

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 6 лют 2025
  • Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la KHAMIS SAIDI (27) ambaye alikuwa kondakta amefariki dunia na wengine kumi kujeruhiwa, baada ya basi la kampuni ya PREMIER LINE lenye namba T 853 DHA, kugonga loli lililokuwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara usiku wa jana January 25 2025 katika kijiji cha Nkuhi Wilayani Ikungi Mkoani Singida.
    Basi hilo lilikuwa likitokea Tunduma Mkoani Songwe likielekea Mkoa Mwanza ambapo dereva wa basi hilo alikuwa akijaribu kulipita lori lililokuwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara ndipo basi hilo likagonga lori kwa nyuma na kusababisha kifo na majeruhi.
    Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kwa njia ya simu kamanda wa polisi Mkoa wa Singida SACP. Amon Kakwale amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi hilo.
  • Розваги

КОМЕНТАРІ •