SWALI: Mwanamke anapomaliza EDA ya kufiwa au kuachwa je anatakiwa Afanye nini....???

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 21 вер 2024
  • Eda ni muhula maalum ambao mwanamke, aliyekwisha olewa, anatakiwa ‎kusalia bila ya kuolewa wala ‎kuposwa kutokana na mojawapo wa sababu ‎mbili kuu: ‎
    ‎A. kutalikiwa\kuachwa au kuachika na ‎
    B. Kufiwa na mumewe (au mume kutoweka ‎au kukimbia pasipo kujulikana ‎aliko…). ‎
    #MwanamkeanapomalizaEDAyakufiwaaukuachwajeanatakiwaAfanyenini #EDAndioniniaumaanayakenini #Edazikozaainangapi #niniHekimayaEda
    Kwa maana hiyo, Eda ni muhula wa wajibu, uliofaradhishwa ndani ya ‎Qur’ani ‎Tukufu na Hadithi za Mtume ‎ﷺ‎ ambazo ziko nyingi. ‎Mwenyezi ‎Mungu anasema: ‎
    ‏ وَالْمُطَلَّقَاتُ يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ ثَلاَثَةَ قُرُوَءٍ وَلاَ يَحِلُّ لَهُنَّ أَن يَكْتُمْنَ مَا خَلَقَ اللّهُ فِي أَرْحَامِهِنَّ )‏
    ‏ . وقوله تعالى ‏‏(وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجاً يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْراً )‏
    ‎“Na wanawake walioachwa (watalikiwa): wangoje (wasiolewe) mpaka ‎tohara tatu ‎zishe. Wala haiwajuzii kuficha mimba aliyoumba Mwenyezi ‎Mungu katika ‎matumbo yao, ikiwa wanamuamini Mwenyezi Mungu na siku ‎ya Mwisho”.Q;2.28.‎
    ‎“Na wale wanaofiwa na waume zao, miongoni mwenu na kuacha wake, wake ‎hao ‎wangoje (wakae eda) miezi mine na siku kumi.” Q.2:34.‎
    Ama mja mzito aliyefiwa na mumewe, basi eda yake ni tokea tarehe ya ‎kufa ‎mumewe hadi ajifungue. ‎
    Vivyo hivyo, mtalikiwa mja mzito, eda yake ni hadi kujifungua. ‎
    Akijifungua tu basi eda yake imeisha.‎
    ‏‎(‎وَأُوْلَاتُ الْأَحْمَالِ أَجَلُهُنَّ أَن يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ‏‎ ).‎
    ‎“Na wale waja wazito, basi muhula wao ni pale watapotua ujauzito wao.”‎
    Ama mwanamke alieachwa kabla ya kujamiiana na mumewe, yeye hakai ‎eda ‎yoyote, na wala hana mahari -iwapo mahari hayo hayakutajwa ‎kinaganaga-, ‎isipokuwa kiliwazo (i.e. kiacha nyumba, yaani kitu cha kuanzia ‎maisha ya ujane). ‎
    Lakini ikiwa kima cha mahari kilishatajwa na akaachwa kabla ya kujamiana ‎na ‎mumewe, basi mwanamke huyo, pamoja na kwamba hakai eda, anapaswa ‎kulipwa ‎nusu ya mahari ya kima kilichotajwa; ila kama yeye mwenyewe au ‎walii wake ‎‎(mzee wake, kwa mwanamwari) atasamehe malipo hayo Q.2;37. ‎Na katika aya ‎nyengine Q.33.49 Mwenyezi Mungu anasema: ‎
    ‏‎ (‎يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نَكَحْتُمُ الْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ طَلَّقْتُمُوهُنَّ مِن قَبْلِ أَن تَمَسُّوهُنَّ فَمَا لَكُمْ عَلَيْهِنَّ مِنْ عِدَّةٍ ‏تَعْتَدُّونَهَا ‏فَمَتِّعُوهُنَّ وَسَرِّحُوهُنَّ سَرَاحاً جَمِيلاً‎ )‎
    ‎“ Enyi mlioamini! Mtakapowaoa wanawame; wenye kuamini kisha mkawpa ‎talaka ‎kabla ya kuwagusa (kuingiliana kimwili), basi hamna eda juu yao ‎mtakayoihisabu. ‎Na wapeni cha kuwaliwaza na muwawache muachano ‎mzuri” Q.33.49.‎
    Ama mwanamke anayefiwa na mume basi eda yake ni miezi mine na siku ‎kumi, ‎kama nilivyotaja hapo juu na kunakili aya ya Qur áni. Na ni sawa ‎ikiwa mume ‎huyo alikwisha jamiiana na mkewe au la; mke atakaa eda ya ‎miezi mine na siku ‎kumi. ‎Yaani, mfiwa na mume anakaa eda ya miezi mine na ‎siku kumi. Iwapo ana mimba basi mpaka ajifungue.‎
    Vile vile, mke huyo anamrithi mumewe huyo aliyefariki, awe aliingiliana ‎naye ‎kimwili au la. Kama mume hakuacha mtoto au watoto (kwa mke ‎mwengine, kwa ‎mfano) basi mwanamke atarithi robo ya mali yote ya mume ‎na kama mume aliacha ‎mtoto au watoto basi mke atarithi thumuni (one ‎eighth) ya mali yote ya mume. ‎
    Hivyo ndivyo alivyoamua Mtume ‎ﷺ‎ kwa Sahaba mmoja aliyekuwa ‎akiitwa: ‎Ma’qal Ibn Yasar ambaye alifariki na kuacha mke kabla ya kuingiliana ‎naye ‎kimwili. ‎
    Hali kadhalika, Ibn Masúd - mmoja wa Maswahaba wakubwa- alikabiliwa na ‎kesi ‎kama hiyo ya mke kufiwa na mume ambaye bado hajaingiliana naye ‎kimwili. Ibn ‎Mas’ud akatoa fatwa ya mke kukaa Eda na pia kumrithi ‎mumewe. Akapewa ‎khabari kuwa Mtume ‎ﷺ‎ alitoa hukumu kama hiyo kwa ‎Ma’qal Ibn ‎Yasar! Ibn Mas’ud alifurahi sana kuona kuwa hukumu yake ‎imewiana na hukumu ‎ya Mtume ‎ﷺ‎ . ‎
    Pili, ni muhimu kujua kwamba mwanamke anakaa eda kwenye nyumba ‎ya ‎mumewe, awe mume yuhai au la, na katika muhula wote wa eda, ‎mwanamke huyo ‎anaendelea kulishwa kama kawaida kuktokana na mali ya ‎mume, mpaka eda yake ‎ishe. Mwenyezi Mungu anasema: ‎
    ‎(‎لَا تُخْرِجُوهُنَّ مِنْ بُيُوتِهِنَّ وَلَا يَخْرُج

КОМЕНТАРІ • 1

  • @MuslimuTv
    @MuslimuTv  3 роки тому

    Yupi Yatima Zaidi Aliyefiwa Na Mama Au Baba?
    👇👇👇👇👇👇
    ua-cam.com/video/Muaf6zyM_Iw/v-deo.html