Bashe awa mbogo akimjibu Mpina "Siwezi ruhusu sukari ifike Sh10 elfu kwa kilo kama disemba 2023"

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 3 чер 2024
  • Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amejibu hoja za Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina ambaye amesema kuwa Serikali isipolinda viwanda vya ndani itashindwa kukusanya kodi akisema kuwa Serikaii imeagiza sukari tani 410 wakati kiasi cha sukari kinachohitajika ni tani 120 pekee.
    Akijibu hoja hiyo leo Jumanne, Juni 4, 2024 wakati wa mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2024/25, Bashe amesema hawezi kuruhusu bei ya sukari ifikie Sh10 elfu kwa kilo moja kama ilivyokuwa kwenye baadhi ya maeneo mwezi Disemba 2023.

КОМЕНТАРІ • 79

  • @malugukushaha6764
    @malugukushaha6764 23 дні тому +4

    Namkubari sana mh. Mpina. Bravo mh Mpina👏👏👏. Bunge hili lingekuwa na wabunge machachali kama akina Mpina , Bashe, Slaa , Makonda, n.k wote wakawa wanachalenjiana hivyo , nchi hii ingekuwa mbali kimaendeleo.

  • @chandeyusufu9570
    @chandeyusufu9570 11 днів тому +3

    Kwanza anza kumshukuru Allah harafu spika wa bunge

  • @issaramadhani9141
    @issaramadhani9141 25 днів тому +8

    Nchi yetu kwakweli wafanyabiashara hawana uzalendo hata kidogo, yaani wao wanachojua ni kupiga hela tu. Issue ya sukari miaka yote ni shida na ukiweka ile kauli ya kulinda viwanda vya ndani wao wanaitumia kujinufaisha wao.

    • @bundaman8542
      @bundaman8542 24 дні тому

      Umenena.

    • @MrKhatibu
      @MrKhatibu 23 дні тому +1

      Mfanya biashara lengo lake ni kunenepesha account yake, tatizo ni serikali inatakiwa wanapotoa tax exemptions kutokana na mazingira kama haya basi wawape na bei ya final consumers. Kinyume chake ndio haya ya kukomolewa wateja wa mwisho ambao ni mimi na wewe

  • @samwelsimon6842
    @samwelsimon6842 18 днів тому +2

    Mpina yupo makini sana

  • @emmanuelmlekwangano9991
    @emmanuelmlekwangano9991 12 днів тому

    Bashe yupo sahihi sana chapa kazi mheshimiwa

  • @liannsambu7264
    @liannsambu7264 21 день тому +4

    Mpina uwa unanini na hon .Bashe ? What is behind this cz sioni uzalendo hapo ila Kuna kitu kikonyuma ya pazia , ? Je hon mpina why kila akipresent hon Bashe hukosi kumpinga ?? Na Uzuri Bashe ameshakujua kuwa uwa unakuja kumchallenge na kwakuwa Yuko smart huwezi kumnock out maana Yuko smart na hajibu KISIASA anajibu ki technically na Kwa ushahidi ,so hon mpina jipange kuwapinga wale wanapokuja na hoja nyepesi na waliona mashaka nao ila siyo Bashe ,maana hautamnock out he is smart than you think

    • @yateramadavaathumanmmbaga7776
      @yateramadavaathumanmmbaga7776 9 днів тому

      Ukifunua pazia mplna ana jambo lake kule kagera sugar la kimaslahi sasa ameona bashe anaharibu deal kwa kuruhusu sukari ya nje iingie, hapo ndipo mgogoro ulipo na nyuma ya mpina kuna vigogo wengi mabwanyenye. Mwenyezi Mungu amsimamie bashe ashinde hii vita ya mabwanyenye. Inauma na kuumiza mnoo unapotetea wanyonge tena pekeyako halafu kundi la mabwanyenye linatafuta kila njia kukuvuruga

    • @yateramadavaathumanmmbaga7776
      @yateramadavaathumanmmbaga7776 9 днів тому

      Yaani tuna spika msomi na anayeijua kazi yake. Hongera sana Dr. Tulia, Mwenyezi Mungu akubariki zaidi

  • @SuleimanMuhudi
    @SuleimanMuhudi 12 днів тому +1

    Muacheni Bashe afanyekaz

  • @VASCoMgoli-to7ql
    @VASCoMgoli-to7ql 23 дні тому +2

    Mpina mtu sana

  • @msafiriomary893
    @msafiriomary893 24 дні тому +2

    Bunge tukufu kivipi wakati wizi rushwa zimejaa bungeni utukufu ni kwa mungu tu peke yake.

  • @AbdilahiMriri
    @AbdilahiMriri 25 днів тому +2

    Maana yake mpango huo haifai shotikati ilikuwa tu kwanza ni kuingiza mpango huo kwenye kuwaondolea kodi.
    Na pili kwann makampuni ya mbolea ni matano tu?

  • @mmarycalvin6395
    @mmarycalvin6395 24 дні тому

    Unaanza Mwenyezi Mungu ndio unakuja hao sijui spika na wowotee walee

  • @godfreybitakama9845
    @godfreybitakama9845 9 днів тому

    Walaji wanalindwaje kwa gharama ya 5000.mpaka zaidi sehemu nyingine unamsaidiaje nauliza

  • @balexendersun2793
    @balexendersun2793 24 дні тому +2

    Mpina oyo

  • @athumanmkomwamkomwa2912
    @athumanmkomwamkomwa2912 9 днів тому

    Sawa

  • @davidsimbeye1548
    @davidsimbeye1548 11 днів тому +2

    Tatizo la Mpina ni machungu ya kukosa uwaziri bahati mbaya sana ni kwamba amemgusa mtu ambaye ni mwadilifu, mzalendo, na ambaye yuko smart kichwani

    • @albinusmkono5887
      @albinusmkono5887 11 днів тому

      Unachuki binafsi na mpina.unahoja za ubinafsi unasema ni kwasababu hajapata uwaziri.!!! Yaani unachuki sana mpina pia ni mvivu sana wa kuchambua hoja pole sana.lkn tulip wengi tumemwelewa mpina angalia hata coment jitafajari😅😂😂🎉

    • @evelynmwaimu-vd9jo
      @evelynmwaimu-vd9jo 11 днів тому

      Llooooo!!!

    • @user-lw3tg3yg5b
      @user-lw3tg3yg5b 10 днів тому

      Kwani kila mtu lazima awe waziri? Hayo mawazo yako potofu mpina ni mzalendo wa kweli

    • @davidsimbeye1548
      @davidsimbeye1548 10 днів тому

      @@albinusmkono5887 Tatizo lako ni uelewa tu ndo unakusumbua, hivi mtu anaposema kuhusu kulinda viwanda vya ndani unaelewa maana yake? Hakuna mtu anayekuja kushambulia viwanda na mabomu, tafsiri yake ni kulinda viwanda vya ndani ndani dhidi ya bidhaa kutoka nje zinazouzwa kwa bei ya chini wakati bidhaa za ndani zinauzwa kwa bei kubwa. Kwa hiyo unazuia sukari kutoka nje ila wafanyabiashara wa ndani wauze kwa bei ya juu, na mwananchi wa hali ya chini anaumia huku wafanyabiashara wakijipatia faida kubwa. Ukishabikia hoja kama hiyo maana yake ni kwamba unashabikia siasa za kijinga. Yaani wafanyabiashara wanaficha sukari inaonekana imeadimika ili wauze Kwa bei kubwa halafu mbunge anawatetea na unamwita mzalendo uzalendo gani huo

  • @zobakazizi7637
    @zobakazizi7637 25 днів тому +1

    Kwa nini sukari ya viwanda vyetu haionekani. Sukari ya nje iwekewe nembo yake. Zisitumike nembo za viwanda vyetu.

  • @roberttagaya9098
    @roberttagaya9098 5 днів тому

    Wabunge wetu bana. Yani wao kila kitu hata kisichokuwa na tija wanapiga meza tu.😂😂

  • @AgnesShiwali
    @AgnesShiwali 8 днів тому

    Na huo ushaid spika tunaomba tuujue na tuushudie kinachoendlea

  • @rmimy
    @rmimy 11 днів тому

    Nimewasikiliza wote na media address ya Mpina naona kama mpina anatumika na makampuni yanayozalisha Sukari. Bashe piga kazi baba. hakuna kurudi nyuma, afadhali kuwapa NRA kibalia kuliko wafanya biashara. Big up

    • @albinusmkono5887
      @albinusmkono5887 11 днів тому

      Mimi namkubali mpina.bahati mbaya hujabalance mkumbatie bashe😅😅😂😂😢😢.Kuna barua wenye viwanda waliomba mapema kibali lkn bashe hakutoa kwa wakati.waziri analalamika kua sukari.iliuzwa kwa bei kubwa tofauti na bei elekezi Ina maana alishindwa kusimamia hata Hilo hulioni.??😅😅😅😂😂

  • @rweumbizalugaimukamu4905
    @rweumbizalugaimukamu4905 24 дні тому +1

    Bashe yupo vizuri

  • @Ahmedikiringamoyo
    @Ahmedikiringamoyo 9 днів тому

    Bashe nasamia wananiamzuri ila tatizolaokubwa awawezi kutufatilia sisiwakulima tunavyonyanyaswa nakuzulumiwa pesazamazaoyetu

  • @philipombwambo1980
    @philipombwambo1980 12 днів тому +1

    Huyu bashe maneno mengi sana hayana maana na ukimchunguza huyu ni mhuni

  • @albinusmkono5887
    @albinusmkono5887 11 днів тому

    Kiseme hicho kitu.bashe ni wapigaji mpina ana hoja za kitosha amemdhika pa baya bashe pole msaidie kwa hoja bashe.sio kwa chuki kumchukia mpina

  • @allymusira2153
    @allymusira2153 24 дні тому

    Waziri yupo sahihi

  • @MwigaAdam
    @MwigaAdam 11 днів тому

    Ili bunge utukufu wake nini wakati CAG kaumaliza mwendi wa wizi na ubadhirifu wa mali za umma??

  • @respiceandason
    @respiceandason 11 днів тому +2

    Mkoa upi sukari iliuzwa elf10?????????? Emungu lisamehe taifa letu" kuna watu hawakumbuki kuwa walikuja bila kitu wataondoka bila kitu"

  • @user-df5mj2ft4w
    @user-df5mj2ft4w 12 днів тому

    Aibu naon mm mpk leo tunaongelea sukari

  • @IlalioMbunju-hv7kw
    @IlalioMbunju-hv7kw 13 днів тому

    Kwa nini mnapenda sana kupiga makofi, wananchi tuwaelewaje wapiga makofi

  • @liannsambu7264
    @liannsambu7264 21 день тому

    Na uzuri hon.speaker ameshakujua pia unaraise point kupinga na siyo kujenga hoja za kuleta MAENDELEO so hon .mpina kubali tu kuwa bashe anafanya kazi na wewe subiri wakati wako ukirudi kuwa waziri na pia kama unapersonal interest naye ungemfata mkaongea , maana ninyi ni WANAUME MNAJENGA NYUMBA MOJA ,

  • @selemaniigosha
    @selemaniigosha 24 дні тому +3

    Mnaomshabikia bashe wote uelewa wenu ni mdongo!!

  • @shabanipanya1033
    @shabanipanya1033 13 днів тому +1

    Miaka zaidi ya 50 ya uhuru bunge letu na wasomi wetu wanajadili sukari tena wanazungumza kisooooomi

  • @chandeyusufu9570
    @chandeyusufu9570 11 днів тому

    Mnafki tu mkweli mpina

  • @twoboyztv1
    @twoboyztv1 24 дні тому

    Sheria ifuatwe

  • @fredrickipembe8188
    @fredrickipembe8188 24 дні тому +1

    Bashe ukiendelea kumfata mwiguru atakuponza mana mpango wenu wewe na waziri wa fedha eti sisi wakulima the na machine ya ifd mwaka ujao utaenda kulima wewe na huyo mwiguru nchembe wako

  • @kennethmhaiki8957
    @kennethmhaiki8957 10 днів тому

    Bashe yupo vzr na ana confidence

  • @AbdilahiMriri
    @AbdilahiMriri 25 днів тому

    Kama ni mbolea ndo mmefeli kabisa, mwaka jana tu kulikuwa na karibu maduka 1000 yaliyonyang'wa vibali vya mbolea

  • @user-jx8ix3yv4k
    @user-jx8ix3yv4k 23 дні тому

    Unamshukuru spika ndo umshukuru mungu?

  • @lovenessmohamedy6329
    @lovenessmohamedy6329 24 дні тому +2

    Mpina anatakiwa apewe tuzo hakwenda bungeni kulala

    • @husseinmramba
      @husseinmramba 24 дні тому

      We acha ushabiki sio kila mtu anaepinga pinga ni mpiga kazi na waukweli huyu anawafurahisha watu kama nyie mnaopenda kuchukia serikali ufarijike na nafsi yako

  • @AbdilahiMriri
    @AbdilahiMriri 25 днів тому

    Hiyo Sukari hadi leo wala haijaaa vizuri.
    Kwakuwa Sukari hadi sasa katikati ya miji ni 3200.
    Je vijijini si itakuwa ni 4000?

  • @saiditoroka602
    @saiditoroka602 12 днів тому

    Mh unatudanganya sukari hajafika sh. 10000 @ kg

  • @AnnoyedFlowerPot-mr2ps
    @AnnoyedFlowerPot-mr2ps 25 днів тому

    Hongera bashe

  • @hamzakimaro3764
    @hamzakimaro3764 25 днів тому +1

    mpina amepokea mlungula kwa wenye viwanda vya sukari,serekali isinge agiza sukari ya bei nafuu kutoka nje ,kilo ya sukari ingezidi elfu kumi!!
    Pia wenye viwanda vya sukari nao wauze nje wapate pesa za kigeni,kwani lazima wawauzie watanzania tu? Acha roho mbaya Mpina!!

    • @issaidrisamusa5962
      @issaidrisamusa5962 24 дні тому +1

      Wenye sukari wanaruhusiwa kuuza nje ziada , na si vinginevyo. Nchi yetu Bado hatujafikia kuzalisha ziada. Na hiyo inayotoka nje huko nje huzalisha ziada ndio huja kwetu

    • @lovenessmohamedy6329
      @lovenessmohamedy6329 24 дні тому

      Tatizo sukari inayoingia ina ubora? Sukari inatoka brazir ikija huku inauzwa bei ya chini jiulize

    • @onelovetz7935
      @onelovetz7935 22 дні тому

      Imetoka elfu 40000 Hadi laki 410000 hapo hakuna watanzaniani wazungu hao jerr sraa mpina makonda hao ndio waafrica

  • @PhilipoMwita-wc1ku
    @PhilipoMwita-wc1ku 24 дні тому

    Wakulima wa mahindi tunalia njaa kali

  • @AlexBoniface-rr6jk
    @AlexBoniface-rr6jk 24 дні тому

    Jangwani

  • @DavidSemu-gu6wp
    @DavidSemu-gu6wp 23 дні тому

    Kuna nini Kwa Mpina toka atemwe kwenye uwaziri!!? Kila waziri amekuwa mpinzani wake, NI uzalendo ni chili au wivu inabidi wenye akili wajiulize.

    • @DavidSemu-gu6wp
      @DavidSemu-gu6wp 23 дні тому

      Aah! Mpina Mzee WA kupima samaki Kwa rula sijui alitaka kuwashonea suti?

  • @jacksonngusi4122
    @jacksonngusi4122 25 днів тому +1

    bashe huku wakulima wa maind ni majonzi makubwa bei iko chin mno na uliahid bei itakuwa nzur vp shinda iko wap huk kwetu

    • @issaidrisamusa5962
      @issaidrisamusa5962 24 дні тому +1

      Unataka ipande hadi sh ngp ili tulie njaa , Hali ngumu unataka chakula kiwe bei juu . Tuhurumiane ndugu yangu

    • @jacksonngusi4122
      @jacksonngusi4122 24 дні тому

      ​@@issaidrisamusa5962 mkulima anapata hasara pembejeo bei juu wewe kama mvivu hata bei iwe ndogo utalia njaa tu amka haviji kirahis

  • @abdul-azeezmagram4973
    @abdul-azeezmagram4973 25 днів тому +1

    Nilichogundua mpina anachuki na bashe pili mpina hana elimu

  • @CosmasLudege
    @CosmasLudege 5 днів тому

    😅😅😅😅😅😅