MAPYA YAIBUKA CHADEMA MAJINA YALIYOKATWA YAREJESHWA 'TUTAZUIA UCHAGUZI USIFANYIKE'

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 28 лис 2024
  • Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mkoa wa kichama Kinondoni kimewataka wasimamizi wa uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji kutenda haki katika hatua ya kuwarejesha wagombea walioengeuliwa kwa sababu mbalimbali.
    Akizungumza na wanahabari leo Jumatano, Novemba 13, 2024 mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kinondoni, Henry Kileo amesema taarifa walizonazo wagombea wao huenda watarejeshwa lakini sio maeneo ambayo ndio ngome zao.
    Jana, Jumanne Novemba 12, 2024 katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Waziri wa Tamisemi, Mohamed Mchengerwa alitoa agizo kwa kamati za rufani zinazoongozwa na makatibu tawala wa wilaya kuongeza muda wa siku mbili kupitia rufaa za wagombea wa nafasi mbalimbali za uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji.

КОМЕНТАРІ •