Gundi ya miti | utajiri uliojificha.

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 23 сер 2022
  • Mbuga ya Wembere ni hifadhi yenye ukubwa wa hekta 160,000 inayopatikana katika kingo za wilaya ya Igunga mkoani Tabora, wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga na wilaya za Iramba na Ikungi mkoani Singida.
    Mbuga hii inauoto wa asili wa nyasi na miti mbalimbali ikiwemo miti aina ya Migunga inayotoa gundi ''Gum Arabica'' kwa kiwango kikubwa zaidi nchini.
    Gundi ipatikanayo katika miti aina ya migunga hutumika kuzalisha bidhaa mbalimbali kama vipodozi, dawa mbalimbali kwaajili ya mbao(varnish), dawa za karatasi, sukari, pipi na matumizi mengine mengi kama kwenye chakula, vinywaji nakadhalika. Wakati wa kiangazi ni msimu rafiki sana kwa uvunaji wa gundi ya miti.
    Hapa nchini kiasi cha gundi ya miti kinachozalishwa ni takribani tani 1000 kwa mwaka na sehemu ya gundi hii husafirishwa katika nchi mbalimbali kama India, Ufaransa, Uingereza n.k.
    Ni wazi kuwa iwapo wananchi hasa vijiji jirani na hifadhi watajishughulisha na utunzaji pamoja na upandaji miti itapunguza utegemezi wa binadamu kwenye miti ya asili kukidhi mahitaji ya msingi kama nishati kwa kutumia kuni na mkaa, mbao na miti ya ujenzi.
    Vilevile zao hili la kibiashara ni fursa kubwa ya kiuchumi kwa wanakijiji wanaozunguka maeneo ya mbuga hii ya mti ikiwa ni pamoja na ongezeko la ajira ikiwamo wazalishaji, wavunaji, wasafirishaji na wafanyabiashara kwa ujumla hivyo kuboresha maisha ya wanavijiji wanaozunguka maeneo hayo kwani hunufaika kutokana na mapato yatokananyo na hifadhi.
    Uhifadhi misitu unatajwa kuwa muhumu zaidi kwa ustawi wa binadamu ndiyo maana serikali kupitia wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) inachukua jukumula kulinda utajiri huu kwa kuanzisha shamba la miti ya gundi wilayani Iramba mkoani Singida hasa kwa kutunza miti iliyopo na upandaji wa miti ya migunga, kutoa elimu ya umuhimu wa uhifadhi wa uoto huu wa asili kwenye jamii kwaajili ya kizazi cha sasa na cha baadae.
    Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na wakala wa huduma za misitu Tanzania mkoani Iringa kwa barua pepe;
    dfmiramba@tfs.go.tz

КОМЕНТАРІ •