KERO YA MAJI YAMUIBUA RC CHALAMILA ASHTUKIZA DAWASA "HATUA ZA HARAKA ZIMECHUKULIWA"

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 1 жов 2024
  • Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amewatoa hofu Wananchi na Wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam kwamba hatua za haraka zimechukuliwa kukabiliana na uhaba wa maji, ikiwemo kununua mitambo maalumu kwa ajili ya kuchuja na kusafirisha kutoka kwenye vyanzo vya maji.
    Hayo amebainisha leo wakati alipokutana na Wakuu wa Wilaya, Watumishi wa Dawasa na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM, huku akisema kuwa zaidi ya Billioni 6 zimetengwa na tayari zimeidhinishwa kugharamia maboresho na kazi hiyo inatarajiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu ili kuondoa kero ya maji kwa Wananchi na Wakazi wa Dar es Salaam.
    Hata hivyo naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mkama Bwire, amesema "mahitaji ya maji Dar ni zaidi ya lita million 600 kwa siku, kiwango ambacho ni kikubwa ikilinganishwa na uzalishaji wa sasa, tumepokea maelekezo ya mkuu wa mkoa na tutahakikisha tunayafanyia kazi kwa haraka ili mitambo ifungwe kwa wakati na kuanza kufanya kazi ndani ya miezi mitatu kama ilivyopangwa".

КОМЕНТАРІ •