Tafiti: Zaidi ya asilimia 54 ya wanawake Kinondoni wanajichubua

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 23 чер 2024
  • Moja ya tafiti iliyofanywa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas), imeonesha kwamba asilimia 54.5 ambayo ni zaidi ya nusu ya wanawake wilayani Kinondoni wanatumia vipodozi vya kujichubua.
    Utafiti huo unasema wengi wao ni wale wanaofanya kazi mapokezi ndio wanaobadili rangi zao ili kuwa weupe. Hivyo zimefanyika tafiti kuona vipodozi vinavyotumika kuwa ni salama katika afya ya ngozi na haliveti madhara kwa mtumiaji.
    Akidokeza juu ya tafiti hiyo na nyingine nyingi zilizofanywa na chuo hicho ambazo zitawasilishwa katika kongamano la Kisayansi litakalofanyika Juni 27 na 28 mwaka huu.
    Makamu Mkuu wa Muhas, Profesa Appolinary Kamuhabwa amesema pia wamebaini asilimia 15 ya wagonjwa wa VVU wana kiwango cha juu cha sukari (Hyperglycaemia).
    "Unywaji wa pombe na shinikizo la juu la damu linachangia wagonjwa hawa kuwa na kiwango cha juu cha sukari mwilini," amesema Profesa Kamuhabwa hii Juni 24, 2024 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujio wa kongamano hilo.
    Aidha, amesema katika kongamano hilo litakalo wakutanisha wadau zaidi ya 400 wa ndani na nje ya nchi linatarajiwa kuwasilisha tafiti za kisayansi 80 kwa njia ya maongezi na 107 kwa njia ya mabango ambazo zitawasilishwa katika mada ndogo nane.

КОМЕНТАРІ •