IRINGA: WANAFUNZI WA IT WADUKUA MFUMO WAIBA ADA KWA CHUO

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 18 вер 2024
  • CHUO Kikuu cha Iringa(UoI) kimewafukuza wanafunzi zaidi ya 50 waliokuwa wakisoma kozi mbalimbali chuoni hapo baada ya kushindwa kulipa ada.
    Wanafunzi hao ni sehemu ya wanafunzi 256 waliokusudia kukiibia chuo baada ya mfumo wa chuo hicho wa malipo ya ada kudukuliwa na kuonesha wamelipa ada waliokuwa wakidaiwa.
    Taarifa ya Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Ndililio Urio inaonesha kwamba mfumo huo ulidukuliwa na baadhi ya wanafunzi wa Teknolojia ya Habari (IT) chuoni hapo siku za nyuma ambao wanafunzi hao wamegoma kuwataja.
    "Jambo hili tulianza kulishughulikia toka Julai mwaka jana lakini hatukupata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wanafunzi hao," alisema.
    Katika kuwachukulia hatua, alisema chuo kilijiridhisha na kufikia uamuzi wa kutoa maonyo kwa wahusika na kuwataka walipe upotevu wa fedha uliosababishwa na kadhia hiyo.
    Prof alisema wanafunzi hao wamewaingiza hasara wazazi wao kwa kuwalipa watu waliodukua mfumo huo badala ya chuo.
    Alisema seneti iliyoketi Mei 24, mwaka huu imewasamehe wale waliokiri na kuomba msamaha na kulipa ada huku wale wachache waliokaidi wakifukuzwa.
    Alisema ni jambo la kawaida kuchezewa kwa mifumo ya chuo na kwamba matukio hayo yanapojitokeza taratibu za kuimarisha mifumo hiyo hufanywa.
    Aidha uongozi huo wa chuo umetoa ufafanuzi wa malalamiko yaliyotolewa bungeni hivikaribuni na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mainuna Ahmad Pathan alipokuwa akichangia hoja ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhusu chuo kikuu cha Iringa.
    Katika malalamiko yake, chuo hicho kimesema mbunge huyo alikituhumu chuo hicho kwamba kina uongozi dhaifu, mfumo dhaifu wa ulipaji malipo na kwamba wahasibu wake hughushi namba za malipo ya ada na kuwapa wanafunzi.
    Kadhalika alidai kuwa chuo hicho kimewalipisha wanafunzi mara mbili na kiliwafukuza wanafunzi kwa kosa la kughushi malipo.
    Makamu Mkuu wa chuo alisema chuo chao kina uongozi imara wenye weledi na uzoefu katika kuendesha na kusimamia vyuo vikuu kwa kufuata taratibu na miongozo iliyowekwa kwa mujibu wa kanuni na sheria ya vyuo vikuu nchini.
    Alisema chuo kikuu cha Iringa kina mifumo imara ya uongozi ikiwemo mifumo ya fedha ambapo namba za kufanyia malipo (control numbers) hutengenezwa na kutumwa moja kwa moja kwa mwanafunzi husika kupitia barua pepe au namba yake ya simu.
    Alisema mwanafunzi akishalipa ada hupokea ujumbe mfupi kwa njia ya simu, na kutokana na uimara wa mfumo huu chuo kilibaini udanganyifu uliojitokeza kwa baadhi ya wanafunzi kughushi malipo na kukiibia chuo.
    "Uongozi wa chuo unawasihi watanzania na wadau wote ndani na nje ya nchi kuendelea kuwa na imani na chuo katika kuwaletea maendeleo sahihi kwa njia ya taaluma inayotolewa na chuo hiki," alisema.

КОМЕНТАРІ • 2