Makamu wa Rais wa Zanzibar akutana na uongozi wa Kanisa Katoliki Kigoma

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 17 жов 2024
  • Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, leo Mei 07, 2024 amekutana na kufanya Mazungumzo na Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma, Mchungaji Joseph Mlola.
    Mkutano huo uliobeba Dhamira ya Kujitambulisha na Kukuza Mahusiano Mema kati ya Pande Mbili hizo, ambao umejikita katika kubadilishana mawazo juu ya mambo mbali mbali ya Kiserikali, Siasa na Kijamii, umefanyika Ofisini kwa Askofu huyo, huko katika Kanisa Katoliki Jimbo la Kigoma, Mkoa wa Kigoma.
    Viongozi mbali mbali wa ACT Wazalendo wameambatana na Mheshimiwa Othman katika Mkutano huo, wakiwemo; Makamu Mwenyekiti ACT Wazalendo Tanzania Bara, Ndg. Is-haka Mchinjita; Katibu Mkuu, Ado Shaib Ado; na Kiongozi wa Chama Mstaafu, Ndugu Zitto Zuberi Kabwe.
    Kitengo cha Habari
    Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
    Mei 07, 2024

КОМЕНТАРІ • 2