OMO: Wenzetu wameigeuza hii nchi kuwa kituko, yaani ni kama samaki yuko majini lakini analia kiu

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 17 жов 2024
  • Mwenyekiti wa Taifa wa ACT - Wazalendo, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, leo Jumatatu Mei 06, 2024 amehutubia mbele ya Viongozi, Wananchi, Wapenzi na Wafuasi wa Chama chake, akiwa Mgeni Rasmi wa Mkutano wa Hadhara, hapo Katika Viwanja vya 'Mkongoro Center', Kata ya Mkongoro, Jimbo la Kigoma Kaskazini, Mkoa wa Kigoma.
    Mheshimiwa Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, amehutubia Mkutano huo ambao Viongozi mbali mbali wamehudhuria hapo wakiwemo; Makamu Mwenyekiti wa Chama Tanzania Bara Ndugu Is-haka Mchinjita, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Ndg. Ado Shaibu Ado; pamoja na Kiongozi wa Chama Mstaafu, Ndugu Zitto Zuberi Kabwe.
    Awali, kabla ya Mkutano huo ambao pia lengo lake ni kusikiliza na kuzipatia ufumbuzi Kero za Wananchi, Mheshimiwa Othman amewatembelea na kuwajulia-hali Wagonjwa na Wazee mbali mbali wasiojiweza, wakiwemo wa Mitaa ya Seremala na Kalinzi, ikiwemo Familia ya Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mkoa wa Kigoma, kufuatia Kifo cha hivi karibuni cha Mama yao Mkubwa, Marehemu Bi.Farida Ibrahim Kitandala; sambamba na kuwakagua Alhaj Yahya Mahwisa Omar, na Mzee Wilson Mfumya (Katibu Mstaafu wa Kata ya Kalinzi).
    Mheshimiwa Othman, ambaye huko ameambatana na Mke wake, Mama Zainab Kombo Shaib, yupo Kanda ya Magharibi mwa Tanzania, katika Ziara ya Siku Sita (6), kwaajili ya Harakati za Kisiasa na Kijamii, pamoja na Uimarishaji wa Chama.
    Kitengo cha Habari
    Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
    Mei 06, 2024.

КОМЕНТАРІ • 6

  • @alijuma7674
    @alijuma7674 5 місяців тому +2

    Hongera Mh OMO hakika ni kiongozi uliyevaa viatu vya Almarehemu Maalim Seif Sharif Hamad ,kwa siasa za Ulimwengu wa Leo Mh OMO na wenzake akiwemo Babu na Mbungo hakika tunawategemea kwa uwezo wa Allah tuvuke salama

  • @AllyMustapha-kq8fs
    @AllyMustapha-kq8fs 5 місяців тому +1

    Tuko pamoja uko v 6:53 6:54 vizuri wewe 6:46 ni kiongozi Bora hongera sana

  • @SalehRashid-zz7dc
    @SalehRashid-zz7dc 5 місяців тому +1

    Ah ww mzee mzee uko vizuri

  • @AbrahmanMakame-qj2eu
    @AbrahmanMakame-qj2eu 5 місяців тому

    KACHUME KARAFUU MAKOMBO YA WAARABU KWIOKATIBS TUNAYO