Mpina asimamishwa kuhudhuria vikao 15 vya Bunge

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 23 чер 2024
  • Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamebariki kifungo cha mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina cha kutohudhuria vikao 15 vya Bunge mfululizo kwa kosa la kumtuhumu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kuwa alilidanganya Bunge kuhusu sakata la kuagiza sukari nje.
    Hatua hiyo imefikiwa baada ya Mwenyekiti wa Kamati Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge, Ally Makoa kuwasililisha taarifa ya kamati hiyo na wabunge kutoa maoni kuhusu tuhuma za Mpina kudharau mamlaka ya Spika na Bunge, jijini Dodoma leo Jumatatu Juni 24, 2024.
    Kamati ilipendekeza mbunge huyo kusimamishwa vikao 10 vya Bunge, lakinimaazimio na maoni ya wabunge wamependekeza kusimamishwa vikao 15. Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amebariki adhabu hiyo.
    Pia, Dk Tulia amesema adhabu ya mbunge huyo imeanza kuhesabiwa kuanzia leo Juni 24, 2024 na kusema hatarudi katika kikao cha pili cha Bunge cha Novemba, 2024.
    Endelea kufuatilia Mwananchi

КОМЕНТАРІ • 9

  • @nkorankoranigwa4058
    @nkorankoranigwa4058 3 дні тому +1

    Tuna bunge la ajabu Sana.. uchunguzi ufanyike wa tuhuma sio kumsimamisha mbunge....
    Angekuwa mbunge wangu , tungeandamana Hadi bungeni..
    Bunge limedhauriwa vipi..halitaki kuambiwa ukweli..

  • @isamony58
    @isamony58 3 дні тому +1

    Siku zinaenda mtakomaa kwenye uchaguzii tumesha wachokaaaa kufa kwa magufuli tu mambo yamebadilika upywa 😢😢😢😢😢

  • @user-oo1vz3zi1t
    @user-oo1vz3zi1t 3 дні тому

    Dah kaz ipo

  • @saidhamza5318
    @saidhamza5318 4 дні тому

    ndugai hajawah fungia mbunge wa ccm. Sita pia.

  • @SmilingCityMap-xb9md
    @SmilingCityMap-xb9md 2 дні тому

    Hii ndio dunia sasa natambua kwa nini mandela alisota jela miaka 25 kwa makosa lukuki

  • @isamony58
    @isamony58 3 дні тому

    Tunawangoja kwahamu mwakani 2025🤔🙄😏😏😏😏😏😏😏

  • @CharlesSomeke-ml7ju
    @CharlesSomeke-ml7ju 4 дні тому

    Mwamba

  • @antidiusalfred4686
    @antidiusalfred4686 4 дні тому

    Tunawasubil2024,2025

  • @hapaupdates9277
    @hapaupdates9277 3 дні тому

    HUYO MPINA NI MPOTOSHAJI SANA LAKIN NDIO NINEJUA HATA WAKINA LISU WALIKUWA WANASEMA UONGO NA UPOTOSHAJI ASILIMIA 90%.