Wakati Mtume swalawātu Allāhi wasalāmuhu álayhi alipowaamrisha maswahāba zake wamwage pombe baada ya kushika aya inayokataza moja kwa moja haijaripotiwa hadīyth kuwa walitwaharisha vyombo hivyo. Na pia inasema kuwa Madina nzima ilikuwa inatiririka pombe na kama ingekuwa ni najisi basi tungelipata qawli ya mtume juu ya hilo.
Kwenye dakika ya 8 anasema kuhusu kutwaharisha ngozi za mbwa na nguruwe kuwa haritwahariki. Naám, ila huyu nguruwe kuna khilafu baina ya wanachuoni kuhusu unajisi wake. Kuna baadhi ya wanachuoni wanasema kuwa ni najisi, na kuna baadhi wanasema kuwa sio najisi. Ama wanaosema kuwa ni najisi hawa hawana dalili juu ya najisi yake yeye kama yeye sio kinyesi wala mikojo yake. Bali wameegemeza kwenye uharamu wake. Na ndio maana utasikia wakisema "ikiwa mbwa ni najisi na nguruwe hakutajwa unajisi wake kwenye quran je huyu nguruwe ambae ni haramu kula vipi asiwe ni najisi?" Wanajibiwa na wake ambao wanasema kuwa nguruwe si najisi kwa maneno haya" laiti angelikuwa ni najisi basi Mtume swalawātu Allāhi wasalāmuhu álayhi asingeacha kuwabainishia umma wake kwasababu haijuzu kuchelewesha Bayani wakati wa haja" Na laiti angelikuwa najisi na zama zake nguruwe walikuwepo angelisema, na kwanini hakumtaja, kwasababu sio najisi. Na ndio maana wakaweka kanuni wanachuoni "sio kila haramu (mfano nguruwe) ni najisi lakini kila najisi ni haramu" Ukizielewa kanuni hizi huwezi kuyumba.
"Yaani kitu kilichotupwa ndani ya pombe kinapata najisi kwa pombe hilo halafu pombe likabadilika likawa siki basi halitwahariki kwasababu kuna kitu ambacho ni najisi kilicho najisiwa na pombe" Yaani haya maneno ni mageni sana na ya ajabu sana. Na ni kwasababu ashakosea tokea mwanzo kwenye hukmu ya unajisi wa pombe, na kinachoendelea pia hakiwezi kusalimika hapo. Kanuni haisemi kuwa kuingiza kitu ndani ya pombe ndiko ambako kunasababisha isitwaharike. Bali kinachosemwa ni kuifanyia hila hiyo pombe ili ibadilike huku hakutofaa, bali ibadilike yenyewe bila ya kuingizwa kitu, au kuwekwa sehemu ambayo kwakujua khasa inaharakisha kubadilika. Hii ni nukta nyengine ya makosa.
Kufanyia dibaghi, hata kama kwa najisi eti inafaa. Nani kakutangulia kwenye hili. Hivi vitabu mnavyoona vinakupotezeni kiasi kwamba hata qaaida hamtumii na sijui kama unazijua. Na Hii ndio asli ya ujinga na kinachoendelea hapo ni kufanya tarjama ya maneno ya kiarabu tu hata hajui usahihi wake. Usahihi ni kwamba: chukua msingi huo: "kila najisi ni haramu na si kila haramu ni najisi" kanuni hii imeshatangulia hapo nyuma. Mfano huwezi ukatumia najisi kusafishia kitu halafu kikawa twahara. Na juu ya usahihi ni kuwa ilichokitaja hapo "kinyesi cha ndege" usahihi wake ni kwamba " ikiwa ndege au mnyama analiwa basi kinyesi chake wamehukumu wanachuoni kuwa sio najisi wala damu yake, wala mikojo yake" na ikiwa kuwa haliwi basi itazingatiwa kuwa ni najisi ikiwa imekuja dalili juu ya hilo. Mfano tu mikojo ya ngamia Mtume swalawātu Allāhi wasalāmuhu álayhi aliwaamuru baadhi ya wagonjwa waliokuja kwake na hali duni kuwa wanywe na maziwa yake, kuna maswahāba wanasimulia kuwa walichinja na wakaswali hali yakuwa na damu kwenye nguo zao na wala hawajaamrishwa kurejea swala zao, na kuna wengine wameswali wakiwa na damu za majeraha na wala hawajaamrishwa kurejea swala. Basi kwa hadithi hizi zinajumuisha kuwa wale wenye kuliwa kinyesi chao mikojo yao na damu zao sio najisi juu ya kauli yenye nguvu. Na tukitumia msingi wa kuwa najisi ni haramu basi haifai kutumia kitu cha haramu, kama vile mbolea za wanyama kama ng'ombe, mbuzi na wengine haifai kutumia mbolea hizo bali ingekuwa ni najisi asingeacha mtume kuwabainishia umma wake.
Hata hajui anachoongea. Kabla ya kuongea unajisi wa pombe kwanza ungejua kuwa ni najisi au laa. Kwa qawli sahihi pombe sio najisi bali ni haramu. Na wala hapasemwi kuwa ukiingia pombe kwenye nguo eti ukajitwaharishe hizi fatāwa mmetoa wapi. Halafu kuna Qāíidah inasema "sio kila haramu ni najisi lakini kila najisi ni haramu" Hapa utagundua kuwa kuna vitu ni haramu kula au kunywa lakini si najisi, mfano punda kihongwe ni harām kula lakini sio najisi na Mtume swalawātu Allāhi wasalāmuhu álayhi alikuwa anampenda kwa safari zake na wala hakujitwaharisha kutokana na jasho la punda huyo wala mate. Someni jamani halafu ongeeni,
Kwenye dakika ya 13 hapoanaongea kuhusu kitu kukutana na nguruwe au mbwa kinakuwa kimenajisika. Allāhul Mustaáān: hii fiqhi ya ajabu sana: yaani muradi w kukutana tu. Sas tunauliza huyu mbwa kwa ufahamu wako yote ni najisi? Na je kuhusu wale wanaofundishwa kuwinda na wakakamata wanyama je wale wanyama kwanza unawatwaharisha halafu ndio uchinje au unfanyaje maana imekuja kwenye suwratul maaida kuhusu hawa mbwa, na kwenye hadīyth pia zimekuja kuhusu wawindaji. Yaani fiqhi dume inashida zake. Wameeleza wanachuoni kuhusu unajisi wa mbwa kuwa ni mwili wote au ipo mdomoni tu akiramba kitu au sehemu yoyote? Kutokana na hadīyth iliyothibitika kutoka kwa Imām Muslim Allāh amrahamu: im|leza kuwa Amesema Mtume álayhi salām kuwa atakaporamba mbwa kwenye chombo cha mmoja wenu basi aoshe mara 7.... Na wala hajasema akigusa wala kunusa wala kupisha akakugusa. Huu ndio ubaya wa kujisomea mwenyewe bila kuangalia uchambuzi wa wanachuoni wampitavipi kwenye hayo mas,ala.
Dini ya masuwfi wallahi ni mtihani sana.
Ina kanuni ambazo ukakaa na kujadiliana naye anajikuta anakanusha anachokikubali na kukubali anachokanusha
Wakati Mtume swalawātu Allāhi wasalāmuhu álayhi alipowaamrisha maswahāba zake wamwage pombe baada ya kushika aya inayokataza moja kwa moja haijaripotiwa hadīyth kuwa walitwaharisha vyombo hivyo. Na pia inasema kuwa Madina nzima ilikuwa inatiririka pombe na kama ingekuwa ni najisi basi tungelipata qawli ya mtume juu ya hilo.
Kwenye dakika ya 8 anasema kuhusu kutwaharisha ngozi za mbwa na nguruwe kuwa haritwahariki. Naám, ila huyu nguruwe kuna khilafu baina ya wanachuoni kuhusu unajisi wake.
Kuna baadhi ya wanachuoni wanasema kuwa ni najisi, na kuna baadhi wanasema kuwa sio najisi.
Ama wanaosema kuwa ni najisi hawa hawana dalili juu ya najisi yake yeye kama yeye sio kinyesi wala mikojo yake. Bali wameegemeza kwenye uharamu wake. Na ndio maana utasikia wakisema "ikiwa mbwa ni najisi na nguruwe hakutajwa unajisi wake kwenye quran je huyu nguruwe ambae ni haramu kula vipi asiwe ni najisi?"
Wanajibiwa na wake ambao wanasema kuwa nguruwe si najisi kwa maneno haya" laiti angelikuwa ni najisi basi Mtume swalawātu Allāhi wasalāmuhu álayhi asingeacha kuwabainishia umma wake kwasababu haijuzu kuchelewesha Bayani wakati wa haja"
Na laiti angelikuwa najisi na zama zake nguruwe walikuwepo angelisema, na kwanini hakumtaja, kwasababu sio najisi.
Na ndio maana wakaweka kanuni wanachuoni "sio kila haramu (mfano nguruwe) ni najisi lakini kila najisi ni haramu"
Ukizielewa kanuni hizi huwezi kuyumba.
"Yaani kitu kilichotupwa ndani ya pombe kinapata najisi kwa pombe hilo halafu pombe likabadilika likawa siki basi halitwahariki kwasababu kuna kitu ambacho ni najisi kilicho najisiwa na pombe"
Yaani haya maneno ni mageni sana na ya ajabu sana. Na ni kwasababu ashakosea tokea mwanzo kwenye hukmu ya unajisi wa pombe, na kinachoendelea pia hakiwezi kusalimika hapo.
Kanuni haisemi kuwa kuingiza kitu ndani ya pombe ndiko ambako kunasababisha isitwaharike. Bali kinachosemwa ni kuifanyia hila hiyo pombe ili ibadilike huku hakutofaa, bali ibadilike yenyewe bila ya kuingizwa kitu, au kuwekwa sehemu ambayo kwakujua khasa inaharakisha kubadilika.
Hii ni nukta nyengine ya makosa.
Kufanyia dibaghi, hata kama kwa najisi eti inafaa. Nani kakutangulia kwenye hili. Hivi vitabu mnavyoona vinakupotezeni kiasi kwamba hata qaaida hamtumii na sijui kama unazijua.
Na Hii ndio asli ya ujinga na kinachoendelea hapo ni kufanya tarjama ya maneno ya kiarabu tu hata hajui usahihi wake.
Usahihi ni kwamba: chukua msingi huo: "kila najisi ni haramu na si kila haramu ni najisi" kanuni hii imeshatangulia hapo nyuma.
Mfano huwezi ukatumia najisi kusafishia kitu halafu kikawa twahara.
Na juu ya usahihi ni kuwa ilichokitaja hapo "kinyesi cha ndege" usahihi wake ni kwamba " ikiwa ndege au mnyama analiwa basi kinyesi chake wamehukumu wanachuoni kuwa sio najisi wala damu yake, wala mikojo yake" na ikiwa kuwa haliwi basi itazingatiwa kuwa ni najisi ikiwa imekuja dalili juu ya hilo.
Mfano tu mikojo ya ngamia Mtume swalawātu Allāhi wasalāmuhu álayhi aliwaamuru baadhi ya wagonjwa waliokuja kwake na hali duni kuwa wanywe na maziwa yake, kuna maswahāba wanasimulia kuwa walichinja na wakaswali hali yakuwa na damu kwenye nguo zao na wala hawajaamrishwa kurejea swala zao, na kuna wengine wameswali wakiwa na damu za majeraha na wala hawajaamrishwa kurejea swala. Basi kwa hadithi hizi zinajumuisha kuwa wale wenye kuliwa kinyesi chao mikojo yao na damu zao sio najisi juu ya kauli yenye nguvu.
Na tukitumia msingi wa kuwa najisi ni haramu basi haifai kutumia kitu cha haramu, kama vile mbolea za wanyama kama ng'ombe, mbuzi na wengine haifai kutumia mbolea hizo bali ingekuwa ni najisi asingeacha mtume kuwabainishia umma wake.
Hata hajui anachoongea. Kabla ya kuongea unajisi wa pombe kwanza ungejua kuwa ni najisi au laa.
Kwa qawli sahihi pombe sio najisi bali ni haramu. Na wala hapasemwi kuwa ukiingia pombe kwenye nguo eti ukajitwaharishe hizi fatāwa mmetoa wapi.
Halafu kuna Qāíidah inasema "sio kila haramu ni najisi lakini kila najisi ni haramu"
Hapa utagundua kuwa kuna vitu ni haramu kula au kunywa lakini si najisi, mfano punda kihongwe ni harām kula lakini sio najisi na Mtume swalawātu Allāhi wasalāmuhu álayhi alikuwa anampenda kwa safari zake na wala hakujitwaharisha kutokana na jasho la punda huyo wala mate.
Someni jamani halafu ongeeni,
Kwenye dakika ya 13 hapoanaongea kuhusu kitu kukutana na nguruwe au mbwa kinakuwa kimenajisika.
Allāhul Mustaáān: hii fiqhi ya ajabu sana: yaani muradi w kukutana tu. Sas tunauliza huyu mbwa kwa ufahamu wako yote ni najisi? Na je kuhusu wale wanaofundishwa kuwinda na wakakamata wanyama je wale wanyama kwanza unawatwaharisha halafu ndio uchinje au unfanyaje maana imekuja kwenye suwratul maaida kuhusu hawa mbwa, na kwenye hadīyth pia zimekuja kuhusu wawindaji.
Yaani fiqhi dume inashida zake.
Wameeleza wanachuoni kuhusu unajisi wa mbwa kuwa ni mwili wote au ipo mdomoni tu akiramba kitu au sehemu yoyote?
Kutokana na hadīyth iliyothibitika kutoka kwa Imām Muslim Allāh amrahamu: im|leza kuwa Amesema Mtume álayhi salām kuwa atakaporamba mbwa kwenye chombo cha mmoja wenu basi aoshe mara 7....
Na wala hajasema akigusa wala kunusa wala kupisha akakugusa.
Huu ndio ubaya wa kujisomea mwenyewe bila kuangalia uchambuzi wa wanachuoni wampitavipi kwenye hayo mas,ala.