"HATA BIBILIA IMEANDIKA, NI WAJIBU WETU KUMTII RAIS SAMIA" -ALLY HAPI

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 3 жов 2024
  • "HATA BIBILIA IMEANDIKA, NI WAJIBU WETU KUMTII RAIS SAMIA" -ALLY HAPI
    Katibu Mkuu wa Umoja wa wazazi jumuiya ya CCM Taifa (MNEC) Ndg.Ally Hapi amewanyoshea kidole wanaopotosha umma katika mitandao ya kijamii juu ya suala la utekeji na watu kuuawa ambapo wapo baadhi ya watu hususani vyama vya upinzani kuandika mtandaoni kwa kumuhusisha Rais na Serikali jambo ambalo linasura ya kuichafua nchi.
    Hapi amesema hayo akizungumza na wanaccm katika Shina namba 11 tawi la Shilabela kata Pandagichiza Mathius Kashinje Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini ambapo amesema mambo yanayoandikwa mtandaoni na watu wa CHADEMA yanalengo la kuifarakanisha nchi na kutaka kuwagawa watanzania ambao wamejengwa katika misingi ya umoja na utu.
    Aliwataka wananchi kupuuza upotoshaji huo kwani serikali inavyombo vya kuhakikisha wananchi wanakuwa salama huku akieleza kuwa wanaoandika hivyo hawajafanya utafiti juu ya sababu zinazopelekea mambo hayo kutokea
    Hivyo amewataka wananchi kuwakataa kila wapojitokeza na hoja mfilisi kama hizo kwani zinasababisha taharuki kwa wananchi huku akieleza namna watu walivyobadilika kitabia kwa kukosa uvumilivu na kujichulia sheria mkononi bila huruma.

КОМЕНТАРІ • 4