Maisha ya Mwenye Heri Yosefu Allamano (kiswahili)

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 21 лис 2024
  • Yosefu Allamano alikuwa ni padre wa Jimbo la Torino. Amezaliwa kijijji cha Castelnuovo Don Bosco (nyakati hizo kikiitwa Castelnuovo d'Asti) tarehe 21 Januari, Mwaka 1851.
    Kwa miaka 46 amekuwa Mkurugenzi/Gombera wa Kanisa la Hija la Bikira Maria Consolata pale Torino. Padre huyu ni mwanzilishi wa Mashirika ya Kimisionari: Mwaka 1901 alianzisha Shirika la Mapadre na Mabradha wa Consolata na mwaka 1910 alianzisha shirika la Masista wa Consolata.
    Mnamo tarehe 7 Oktoba, mwaka 1990 alitangazwa kuwa Mwenyeheri na Baba Mtakatifu Yohane Paulo II. Tarehe 20 Oktoba, mwaka 2024, siku ya Misioni Duniani, Baba Mtakatifu Francis atamtangaza kuwa Mtakatifu.
    Video hii imetengenezwa na timu ya mawasiliano ya Shirika la Consolata.

КОМЕНТАРІ •