KUELEKEA SIKU YA Mwanamke DUNIANI, Halotel WAFANYA JAMBO SEKONDARI YA KISARAWE II

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 18 вер 2024
  • KUELEKEA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI, HALOTELI WATOA MSAADA SEKONDARI YA KISARAWE II
    Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya Halotel ikiwa ni sehemu ya jamii ya Tanzania inaendelea kujali na kuchangia katika maendeleo ya nchi kupitia nyanja mbalimbali.
    Mbali na huduma ya mawasiliano ya simu, Kampuni imekuwa pia ikichangia maendeleo katika sekta ya huduma za jamii kama vile afya na elimu.
    Akiongea na waandishi wa Habari leo wakati wa kukabidhi vifaa hivyo katika shule hiyo Jijini Dar es salaam, Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Sakina Makabu, amesema Tukiwa tunaelekea kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Halotel imeona ni muhimu kuadhimisha siku hiyo kwa kuchangia katika sekta ya elimu katika kusaidia juhudi za Serikali za kuendeleza sekta hiyo kwa maendeleo ya nchi kwa ujumla.
    Kupitia sera yake ya kurudisha sehemu ya faida kwa jamii (CSR), kampuni imechangia vifaa vya shule kwa shule ya sekondari ya Kisarawe II (A-level) iliyoko wilayani Kigamboni, ikiwa ni kuendana na kusherehekea Siku ya Wanawake duniani.

КОМЕНТАРІ • 1