KIFURUSHI KIPYA CHA MUMBAI

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 12 вер 2024
  • Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kwa kushirikiana na Hospitali ya Kokilaben iliyopo Mumbai, India inapenda kuwajulisha wateja wao kuwa imezindua kifurushi cha safari na afya kuanzia tarehe 16 Julai hadi 16 Oktoba, 2024.
    Kifurushi cha safari na afya kitawawezesha wagonjwa kufanyiwa vipimo kwenye mashine zinazotumia teknolojia ya juu kabisa kwa gharama nafuu.
    Kifurushi hiki kitajumuisha gharama za tiketi ya kwenda na kurudi, maombi ya visa, usafiri wa kumchukua mgonjwa kuanzia uwanja wa ndege wa Mumbai hadi Hospitali ya Kokilaben na kkumrejesha, malazi ya mgonjwa na mhudumu wake, kumuona daktari bingwa "Oncologist" pamoja na kipimo cha kisasa cha PET-CT.
    Kifurushi hiki cha safari na afya kinapatikana kwa dola za kimarekani $1050 kwa safari ya kuanzia DAR/Mumbai/DAR, $1150 Nairobi/Mumbai/Nairobi na $1055 Entebbe/Mumbai/Entebbe.
    Ili kufaidika na kifurushi hiki, tafadhali piga simu: +255748773900 au tembelea Ofisi za Air Tanzania.
    #foryou #flyairtanzania #airtanzania

КОМЕНТАРІ •