Kitabu cha Danieli | Sura ya 1 Hadi ya 12

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 5 кві 2020
  • #Danieli #daniel #bibliatakatifu #HolyBible
    Danieli ~ Sura ya 1 Hadi 12
    UTANGULIZI
    Mtu anayehusika sana katika kitabu hiki ni Danieli, mmoja wa wale watu waliopelekwa uhamishoni Babuloni katika mwaka wa 597 K.K.
    Lengo la mwandishi ni kuwatuliza watu. Anataka kuwapa watu matumaini kwamba Mungu atawaangamiza wadhalimu na kuwaweka huru na salama wale wanaodhulumiwa na kuonewa. Kitabu kinatia mkazo jambo la kuwa imara katika imani na kwamba watu wanaobaki wakimtegemea Mungu watakombolewa. Danieli ni kielelezo cha kuwa na imani thabiti.
    Kitabu chenyewe kwa muundo wake na namna yake ya kueleza mambo ni mojawapo ya vile vitabu kadhaa vya Biblia vinavyojulikana kama vya maandishi yahusuyo “Mambo ya Mwisho” au “Apokaliptiki.” Maandishi ya namna hiyo yanazungumzia kuangamizwa kwa tawala za mabavu duniani na kuanzishwa kwa utawala wa Mungu. Jambo hilo laelezwa mara nyingi kwa njia ya vielelezo na maono mbalimbali. Ufasaha au namna hiyo ya maandishi yatokea pia katika Isaya 24-27, katika sehemu ya Yoeli na Zekaria, na katika Kitabu cha Ufunuo katika Agano Jipya.
    Kitabu cha Danieli ni tofauti na vitabu vya manabii, na katika orodha ya vitabu katika Biblia ya Kiebrania kitabu cha Danieli hakimo katika fungu la vitabu vya manabii, bali kimeorodheshwa pamoja na vitabu vilivyojulikana kama “Maandishi.” Tazama pia utangulizi wa Agano la Kale.
    Sehemu mbili zabainishwa katika kitabu hiki:
    Sura 1-6. Simulizi juu ya mambo yaliyowapata Danieli na rafiki zake. Waliokolewa kutoka kwenye mikasa mbalimbali ya taabu kwa sababu ya tegemeo lao kwa Mungu na utii wao uliolingana na imani yao.
    Sura 7-12. Sehemu hii inatupa maono kadha wa kadha ya Danieli ambamo tawala kadhaa za ulimwengu wa nyakati hizo zinahusika: Babuloni, Medi, Persia na Ugiriki. Maono yote yanaelezwa kwa mifano na vielelezo.

КОМЕНТАРІ • 15

  • @BonnyBonny-bc8dw
    @BonnyBonny-bc8dw Місяць тому +1

    Lord be with you

    • @bibliatakatifu5723
      @bibliatakatifu5723  Місяць тому

      Mungu ni Mwema kwetu, Unaweza kuangalia video hii na kuisikiliza kwa Makini zaidi ua-cam.com/video/WVPyiDbdJok/v-deo.html
      Jiandae vyema kwaajili ya Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Amen

  • @user-ym4ks5un1j
    @user-ym4ks5un1j 5 місяців тому +1

    Asante sana umeturahisihia sisi wengine

    • @bibliatakatifu5723
      @bibliatakatifu5723  3 місяці тому +1

      ua-cam.com/video/7uVPTPPWcEI/v-deo.html
      Napenda kukukaribisha sana kwa Moyo wa Upendo ili uweze kushiriki kwenye masomo ya Biblia kwaajili ya WAUMINI, WACHUNGAJI, WAINJILISTI na VIONGOZI WA KIDINI ili tuweze kujua kwa usahihi kuhusu ujio wa pili wa Yesu na namna ya kujiandaa.
      Madarasa ya masomo ni mara 3 kwa wiki kwa muda wa miezi 10, unaweza ukapangilia mda wako vizuri ukahudhuria madarasa haya. Tunakukaribisha sana kwa moyo wa dhati.
      Kwa mawasiliano zaidi:
      0620 150 540

  • @annetvuseletse4509
    @annetvuseletse4509 Рік тому

    Haya mafundisho yananitia moyo wa kusikiza na kumufuata mungu barikiwa sana

    • @bibliatakatifu5723
      @bibliatakatifu5723  Рік тому

      Tujifunze wote kupitia Kitabu hiki cha Zaburi, kina hekima, maonyo, mafundisho na maelekezo katika maisha yetu. Karibu sana.
      ua-cam.com/video/wRUVaU8Zbkc/v-deo.html

  • @tajirilmole3092
    @tajirilmole3092 Рік тому

    Mungu akutie nguvu kueneza neno lake

    • @bibliatakatifu5723
      @bibliatakatifu5723  Рік тому

      Tujifunze wote kupitia Kitabu hiki cha Zaburi, kina hekima, maonyo, mafundisho na maelekezo katika maisha yetu. Karibu sana. Share kwa wengine Tujifunze pamoja.
      ua-cam.com/video/wRUVaU8Zbkc/v-deo.html

  • @mputaostin3077
    @mputaostin3077 Рік тому +1

    MUNGU AKUBARIKI MPAKA USHANGAE KWA HUDUMA HII.

    • @bibliatakatifu5723
      @bibliatakatifu5723  Рік тому

      Amen amen, Tujifunze wote kupitia Kitabu hiki cha Zaburi, kina hekima, maonyo, mafundisho na maelekezo katika maisha yetu. Karibu sana. Share kwa wengine Tujifunze pamoja.
      ua-cam.com/video/wRUVaU8Zbkc/v-deo.html

  • @naymahayola7828
    @naymahayola7828 2 роки тому

    Nimefulai mafundisho haya

    • @bibliatakatifu5723
      @bibliatakatifu5723  Рік тому

      Tujifunze wote kupitia Kitabu hiki cha Zaburi, kina hekima, maonyo, mafundisho na maelekezo katika maisha yetu. Karibu sana. Share kwa wengine Tujifunze pamoja.
      ua-cam.com/video/wRUVaU8Zbkc/v-deo.html

  • @weinnyasi5894
    @weinnyasi5894 Місяць тому

    Inatupa nguvu ya kiroho kila tunaposikiliza

    • @bibliatakatifu5723
      @bibliatakatifu5723  Місяць тому

      Mungu ni Mwema kwetu, Unaweza kuangalia video hii na kuisikiliza kwa Makini zaidi ua-cam.com/video/WVPyiDbdJok/v-deo.html
      Jiandae vyema kwaajili ya Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Amen

    • @bibliatakatifu5723
      @bibliatakatifu5723  Місяць тому

      Mungu ni Mwema kwetu, Unaweza kuangalia video hii na kuisikiliza kwa Makini zaidi ua-cam.com/video/WVPyiDbdJok/v-deo.html
      Jiandae vyema kwaajili ya Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Amen