Ukiambiwa "Nitumie CV Yako" Haimaanishi Umepata Kazi

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 19 вер 2024
  • Je, umewahi kuambiwa "Nitumie CV yako" na ukadhani utapata kazi? Hii kauli mara nyingi tunaielewa vibaya. Sio kila anayekwambia nitumie CV yako anataka kukupa kazi. Mara nyingi inakuwa mbinu ya kuondokana na wewe. Tena utasikia “nitumie tu kwa WhatsApp” sasa itaingiaje kwenye portal ya wanaoomba kazi.
    Kabla hujatuma CV yako kwa yeyote, jiulize maswali haya muhimu:
    1. Je, anayekuomba CV yako ana nafasi gani au network kubwa kiasi gani cha kukuweka sehemu?
    2. Baada ya kumpa CV yako, alikurudia na kukupa ushauri wowote kuhusu kuboresha CV yako? Utajuaje kaisoma?
    3. Ulimkumbusha kuhusu maendeleo, alikwambiaje? Kama alikwambia umtumie CV tena, jua hajaifanyia kazi!
    4. Je, wanaruhusu kupokea CV ambazo hazipiti kwenye portal ya ajira?
    5. Wakati unampa CV, alikuambia kama kuna nafasi ya kazi wakati huo? Je, kazini kwake wanahitaji mtu?
    6. Kama kuna mtu anahitajika kwenye nafasi fulani, amekushirikisha ili uone kama una uwezo na hiyo kazi?
    7. Tuseme kweli kazi ipo, kwanini asikwambie utume kabisa application?
    Kama mwombaji, jiulize pia:
    8. Je, huyo mhusika ni sahihi na unaweza kufanya kazi naye? Au ni zile za "mi naweza kufanya kazi yoyote"?
    9. Umeiangalia CV yako kuona kama inaendana na kinachotafutwa au ni ya kutumia CV moja kwa kila application?
    10. Kabla ya kumpa CV yako, ulikuwa na mahusiano gani na huyo mtu? Kama unamtafutaga tu unapokuwa na shida ya kazi au unavyomkumbusha kuhusu CV yako, hata yeye atakukumbuka muda huo tu!
    Kumbuka, jukumu la kupata kazi ni lako mwenyewe. Wengine wanasaidia tu wanapoweza na kwa jinsi wanayoweza na kujisikia. Wenye kazi wanatengeneza nafasi kwa mahitaji yao na uwezo wao wa kulipa, sio kwa kumwangalia mtu yeyote anayetafuta kazi. Mbali na hapo ni kukimbilia ajira za taasisi za umma au taasisi za dini.
    Tazama video hii ili upate uelewa zaidi juu ya kauli hii na jinsi ya kujipanga vyema kwenye soko la ajira.
    Jisajili kwenye chaneli yetu ‪@lenzi.michaelkamukulu‬ kwa ushauri zaidi kuhusu ajira na maendeleo ya taaluma yako.
    #Ajira #CV #UshauriWaKazi #MaendeleoYaTaaluma #Tanzania
    ---
    Hakikisha Unafuatilia kwenye mitandao ya kijamii kupitia
    - TikTok: @lenzi_michaelkamukulu
    - Instagram: @lenzi_mindset.podcasst
    Maoni Yako ni Muhimu:
    Tafadhali toa maoni yako na maswali kwenye sehemu ya maoni hapa chini. Tunapenda kusikia kutoka kwako!

КОМЕНТАРІ •