"Hakuna wa kunifukuza CCM, Mimi ni Jembe" Mpina aibua mapya

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 12 вер 2024
  • Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina amesema hawezi kuvuliwa uanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa sababu tu ya kuwataja hadharani aliowaita mafisadi na wala rushwa kwa kuwa hata chama hicho kimekuwa kikikemea vitendo hivyo.
    Mpina kwa sasa anatumikia adhabu ya kutohudhuria vikao 15 vya Bunge, baada ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kumkuta na hatia ya kudharau mamlaka ya Spika na mwenendo wa shughuli za Bunge.
    Mbunge huyo aliyepata umaarufu kwa kuwakosoa mawaziri mbalimbali, alisimamishwa Juni 24, 2024 na anatakiwa kurudi katika Bunge la Novemba 2024.
    Akizungumza jana katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mwaukoli Kata ya Kisesa, Mpina amesema CCM sio pango la wanyang’anyi hivyo kitendo cha kuwasema hadharani mafisadi na kuwatibulia mipango ya kufanya rushwa, dhuluma na wizi, sio sababu ya kumfanya aondolewe katika chama hicho.
    “Wengine wamekuwa wakifanya rushwa zao wanakimbilia katika ubavu wa CCM, nani aliyewaambia CCM ni pango la wanyang’anyi?” amehoji.
    Amesema chama hicho kimekataa rushwa, dhuluma na wizi katika katiba yake.
    “Wengine wanasema Mpina atafukuzwa CCM, hivi jembe kama Mpina lifukuzwe lipelekwe wapi, mimi nifukuzwe kwa kuwasema hadharani wezi?”amehoji.
    Aidha, amesema hayupo tayari kunyamaza kimya huku akiona wananchi wanaumia na kudhulumiwa haki na mali zao, kwa uzembe wa viongozi wanaojali masilahi yao binafsi.
    #samiasuluhuhassan #simbasc #yangasc #mashabiki #nbcpremeireleague #cafchampionsleague #cafconfiderationcup #ikulumawasiliano #entertainment #music #news #yangasc #simbasc #cafchampionsleague #mayele #highlights #cafconfiderationcup #riversunited #mashabiki #yangaleo #yanga #timuyawananchi #daimambelenyumamwiko #entertainment #music #news #magoliyasimba #magoliyayanga #magoliyote #magoliyamayele #mayele #aziziki #manara #manaraleo #ikulumawasiliano #magufuli #kikwete #mayele #singidabigstars #magoliyamayele #magoliyasimba #magoliyayanga #highlights #azamsportsfederationcup #chama #Shot #mamelodisundowns #alahlytv #alahlysc #miraj

КОМЕНТАРІ •