Ripoti ya Uchumi wa Kidijitali 2024 | Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 9 лип 2024
  • Ripoti ya Uchumi wa Kidijitali 2024 inaangazia kuongezeka kwa athari za kimazingira za uchumi wa kidijitali.
    Uwekaji dijitali unawezesha ukuaji wa kimataifa lakini kwa gharama kubwa za kimazingira.
    Sekta ya teknolojia: +3.2% ya uzalishaji wa gesi za ukaa duniani.
    Kuongezeka kwa matumizi ya nishati na maji na kwa taka za kidijitali.
    Matumizi ya umeme yaliongezeka zaidi ya mara mbili katika vituo 13 vikuu vya data kutoka 2018-2022.
    AI huongeza matumizi ya maji na umeme.
    +30% taka za kidijitali, tani milioni 10.5 kila mwaka, kuanzia 2010-2022.
    Nchi zinazoendelea zinakabiliwa na sehemu kubwa ya athari za kimazingira.
    Nchi hizi hazinufaiki kwa usawa kutokana na uchumi wa kidijitali.
    Hii inaweza kubadilika.
    + 500% ya mahitaji ya madini muhimu kwa teknolojia za kaboni ya chini na za kidijitali kufikia 2050.
    Nchi zinazoendelea lazima zichukue fursa za mnyororo wa thamani wa kidijitali.
    Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo linatoa wito wa kuhamia kwa uchumi wa kidijitali wa mzunguko.
    Kutumia tena, kuchakata na kurejesha nyenzo za kidijitali kunatoa fursa za kiuchumi.
    Ni muhimu kuwekeza katika nishati mbadala na teknolojia za ufanisi wa nishati.
    Ushirikiano wa kimataifa unahitajika ili kuimarisha fursa za kidijitali kwa nchi zinazoendelea.
    Na ujumuishaji wa sera za kidijitali na za kimazingira kwa ukuaji endelevu.
    unctad.org/der2024

КОМЕНТАРІ •