RC SERUKAMBA: AMUAGIZA DED KILOLO KUTENGA FEDHA ZA NDANI KWA AJILI YA KUWEKA CHUJIO LA KUCHUJA MAJI

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 29 вер 2024
  • Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo, kupitia mapato ya ndani kutenga fedha kwaajili ya ununuzi wa Chujio ili wananchi kutoka Kata ya Ruaha Mbuyuni waweze kupata Maji safi na salama.
    Hayo yamejili Septemba 27,2024 wakati alipofanya ziara ya kusikiliza kero za wananchi katika kata ya Ruaha Mbuyuni ambapo Wananchi wa Eneo hilo watoa kero ya kuwa maji wanayoyatumia sio safi na salama hivyo wamemuomba Mkuu wa Mkoa kuwasaidia kutatua changamoto hiyo ambayo imepelekea watu kupata magonjwa.
    Akizungumza katika Mkutano huo Mhe. Serukamba amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kutenga fedha kwenye mapato yake ya ndani kwaajili ya Chujio ili wananchi hao waweze kupata maji safi na salama na kutokomeza magonjwa ya mlipuko katika eneo hilo.
    Pia amewaagiza Wakala wa Maji vijijini RUWASA kuhakikisha wanasimamia vizuri miundombinu ya maji na kufikisha maji katika kila kijiji na kila kitongoji
    Ziara ya kusikiliza kero za wananchi imeanzia katika Halmashauri ya wilaya ya kilolo na itaendelea katuka Halmashauri zingine.

КОМЕНТАРІ •