JOKATE SEKONDARI KUVUNJA REKODI KIDATO CHA SITA

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 29 сер 2024
  • Wakati wanafunzi wa kidato cha sita nchini wakiwa katika maandalizi ya mwisho mwisho wa kufanya mitihani ya kuhitimu masomo yao May 2 mwaka huu, walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari JOKATE MWEGELO iliyopo Kisarawe Pwani wamesema wameajindaa vyema kuhakikisha shule yao inapata ufaulu mkubwa kwa wanafunzi wote watakaofanya mitihani huo ili kutimiza adhma ya uanzishwaji wa shule hiyo iliyokua na lengo la kutokomeza zero wilayani Kisarawe.
    Akizungumza ofisini kwake mara baada ya kumalizika kwa mahafali ya kidato cha sita Mkuu wa shule ya sekondari JOKATE MWEGELO Bi. MARIAM MPUNGA amesema kutokana na maandalizi mazuri waliyoyafanya ukilinganisha na mitihani ya majaribio shuleni hapo, majaribio waliyofanya kwa kushikrikiana na shule marafiki na hata ile mitihani ya kujipima ya kiwilaya kimkoa na kitaifa maarufu moku inatoa taswira kwamba wanafunzi wake watakwenda kufanya maajabu katika mtihani wao wa mwisho.

КОМЕНТАРІ •