TANZANIA BARA 0-2 KENYA: HIGHLIGHTS & INTERVIEWS ( FINAL: CECAFA WOMEN CUP - 25/11/2019)

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 27 вер 2024
  • Kenya wameibuka mabingwa wapya wa michuano ya CECAFA kwa wanawake mwaka 2019, wakiwapokonya tonge mdomoni, Tanzania Bara.
    Ubingwa huo ni baada ya kushinda mabao 2-0 kwenye mechi ya fainali iliyochezwe leo jioni Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Jijini Dar es Salaam.
    Jahazi la Tanzania Bara, limezama kwa magoli mawili yaliyofungwa na mshambuliaji hatari, Jentrix Shikangwa, katika dakika ya 71 kwa mkwaju wa penati na dakika ya 88 kwa shuti kali.
    Hivi ndivyo mechi ya fainali ilivyokuwa, na kisha Kenya wakakabidhiwa kombe, wakiivua Ubingwa Kilimanjaro Queens, ambayo ilikuwa imetwaa mara mbili mfululizo.
    Mara baada ya mchezo, Kocha wa Kenya David Ouma akaeleza kilichowapa ushindi leo, azungumzia sababu ya kumuanzishia benchi mshambuliaji wake Jentrix Shikangwa katika kila mechi.
    Kwa upande wa Tanzania Bara Kocha wa Kilimanjaro Queens Bakari Shime akieleza kilichoiangusha timu yake, awaomba radhi Watanzania akiwataka wasivunjike moyo huku akilia na mwamuzi "Ni fainali bora iliyokosa mwamuzi bora".
    #CecafaSeniorWomensChallengeCup

КОМЕНТАРІ • 194