MBINGUNI KUTAKUWA RAHA (OFFICIAL VIDEO) - St Paul's Students' Choir - University of Nairobi
Вставка
- Опубліковано 10 лют 2025
- Available on all Platforms: album.link/i/1...
Performers: St Paul's Students' Choir - University of Nairobi
Producer: Verony Productions Ltd.
Composer: Joseph Shomaly
Copyright ©Verony Productions Ltd.
Nakiri kuwasimulieni na kuwapa siri hii hakika
Mbinguni kutakuwa raha kwa wale wote watakaofika
Hili jambo labidi nitamke kwani nimefikiria hakika
Hakutakuwa rushwa hongo, hirizi wala mlango wa kona,
Heri waliochaguliwa kufurahi na Mwanakondoo
Waliovumilia shida, starehe na anasa za nchi
Ole wenu (ole), ole wenu (ole) ole wenu mnaocheka sasa
Mtalia (nyinyi) mtalia (nyinyi) mtalia na kuomboleza
Ole wenu (ole) Ole wenu (ole) ole wenu mpiganao sasa
Fainali yake inakuja mshahara ni mauti
Ole wenu ole wenu nyinyi mpendao rushwa
Siku zinakuja nayo rushwa pia itakuhukumu
Ole wenu ole wenu nyinyi mpendao wizi
Siku zinakuja vyote ulivyoiba utarudisha
Furahini furahini nyinyi mpendao haki
Siku zinakuja mtakuwa wakuu wa wafalme
Furahini furahini mtesekao kwa dhiki
Siku zinakuja ufalme wote utakuwa ni wenu.