Miwani ya Machinga yatajwa kuwa chanzo cha magonjwa ya macho

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 12 вер 2024
  • Mtaalamu wa macho ameonya tabia ya watu kununua miwani holela na kuivaa kwa kile alichoeleza kuwa hali hiyo huweza kupunguza uwezo wa macho mvaaji.
    Badala yake kabla ya kuvaa miwani, mtu anatakiwa kupimwa na wataalamu ili kujua aina ya miwani anayopaswa kuvaa mtu kwa sababu miwani hiyo huwa na namba ambayo inapaswa kutumika kulingana na nguvu ya macho ya mvaaji husika.
    Ametoa kauli hiyo katika hafla ya uzinduzi wa upimaji macho na kugawa miwani bure kwa wanafunzi wa shule za msingi Tanzania uliofanyika katika shule ya msingi Kilamba iliyopo Mbagala jijini hapa.

КОМЕНТАРІ • 1