Athari za Utawala wa U'Sultan wa Zanzibar kwenye Mwambao wa Pwani ya Kenya-Makala ya Kwanza.

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 20 січ 2025

КОМЕНТАРІ • 132

  • @hafsakirao398
    @hafsakirao398 18 днів тому +4

    Sema kweli japo ni uchungu. Wacha watu wajue na kuelewa what transpired. Shukran my brother Stambuli.

    • @w4058
      @w4058 12 днів тому

      Kwanini useme keshakufa alipokuwa hai uliufyata

  • @abdallahmasare3116
    @abdallahmasare3116 8 днів тому

    Ahsante star

  • @hanifwari206
    @hanifwari206 19 днів тому +2

    Maa Shaa Allah! Historia nzuri sana

    • @2002-h6c
      @2002-h6c 18 днів тому

      @@hanifwari206 Babu muongo kweli kweli huyu, miaka hiyo wazee wa Zanzibar hata kutoka Donge, Matemwe, Jambiani etc kuja mjini Zanzibar ilikuwa shughuli, hata kusoma na kuandika hawajui, sembuse eti kwenda Oman kuwaomba Wamanga waje kuwasaidia kumng'oa Mkoloni Mreno, huo uongo hata miti inashangaa 🤣🤣🤣

  • @mohammedsiga7202
    @mohammedsiga7202 16 днів тому

    Mashaa Allah
    TwaalaAllah umrak ✍🏾✍🏾

  • @mozakhamis7253
    @mozakhamis7253 18 днів тому +1

    amina. sema. wala. usiongope. chote. ishaalla mungu anakusikiya. mdhalimu yoyote hawawezi kusema ukweli

  • @b.truthful
    @b.truthful 18 днів тому +1

    Shukran Kaka kwa kweli ni muhimu sana kuwa na ufahamu huu wa eneo letu kumbe Wa Nubi pia wana mchango wao Pwani

  • @ahmedsharif2424
    @ahmedsharif2424 18 днів тому +1

    Sawa sawa

  • @SA-xj8hc
    @SA-xj8hc 18 днів тому +2

    I will share it to all good people❤

  • @tomgarama3401
    @tomgarama3401 17 днів тому +1

    Shukran kwa makala haya. Hawa viongozi walokuwa miaka ya 30- 60 ndio walioharibu kabisa maisha tunayoishi kama wapwani kwa sasa. Ukweli na usemwe, ni vizuri kama waakilishi ambao ni wazee kutoka kila kabila la kutoka mkoa wa pwani kuweza kuwakilisha jambo hili kwa serikali ya Kenya.

    • @stambuliwash.abdillahinass8123
      @stambuliwash.abdillahinass8123  17 днів тому

      Kwa ridhaa ya Mwenyezi Mgu, tunajaribu kushawishiana kuandaa kongamano amabalo tutajumuika na kujadili namna tutakavyoweza kukubaliana kuungana pamoja na kuwakilisha jambo hili. Du'a zenu (nyote) ni muhimu.

  • @MaryamSalim-yk3po
    @MaryamSalim-yk3po 18 днів тому +4

    Muarabu hakutesa mtu yoyote uliza ukweli unajisemeya maneno unaleta fitna

    • @moxasaidi3398
      @moxasaidi3398 17 днів тому

      Alietesa wazee wetu ashasema hakusema mwarabu

  • @Juleybibsalim
    @Juleybibsalim 19 днів тому +2

    Tuko pamoja sana sheikh

  • @aishathabit3732
    @aishathabit3732 17 днів тому +2

    Kama si waarabu mpaka leo Kenya na Tz mngekuwa chini ya Mreno
    Majina yenu yangekuwa
    Oribero orteriro
    Na huyu mzungumzaji angekuwa anaitwa Ornandir

  • @husseinnderu8268
    @husseinnderu8268 18 днів тому +2

    ❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤

  • @aishathabit3732
    @aishathabit3732 17 днів тому +1

    Huyu mwehu waahid
    Mada Znz ajabu anamalizia uzalendo wa Kenya wakakutane na Zakayo
    Teh teh tehe

  • @NyumbaYaHekima
    @NyumbaYaHekima 18 днів тому +1

    Sheikh Stambuli mm huwa nakuskiliza, kijana mdogo ambae najifunza mambo ya watu wa mwambao. Katika tatizo tulonalo sisi kila mtu anajiona yeye alifaa ajitawale mwenyew mambo hayaendi hivyo. Mm nna wasiwasi watu wa mwambao wa kenya hawakutaka kuwa sehemu ya zanzibar, lau wangelitaka hivyo waengereza wangelipata tabu kufikia malengo hayo, wengine walitaka itokee waunde nchi yao wenyewe ya mwambao, na wengine wakitaka waunganishe na bara, leo munamlaumu sultani na Serekali ingwaje hamkuwa mkitaka kuwa chini yake, ama kwa sababu hamukuwa watu wakutawaliwa na serekali kutokea unguja. Matokeo yake waislamu wamekwenda kuingizwa kwenye pakacha ya wengine. Wachache katika watu wa mwambao wanaoona ilkuwa ni kheri kubakia chini ya ufalme maana hawakupendela. Kila mmoja anajitofautisha na mwengine kwa kabila lake na anajiona yy ni mstaarabu zaidi. Waislamu hatuwezi kwenda hivyo.

  • @mohammedlaabry5799
    @mohammedlaabry5799 12 днів тому

    KARUME alikushauri alipouza zanzibar kwa Mwalim Nyerere afadhali ya sultan aliuza Mombasa akabakiwa wa zanziba Karume engeuza chumbe tukabakiwa na Unguja na Pemba lakini yeye aliuza zanzibar na vilivyomo

  • @ahmedsharif2424
    @ahmedsharif2424 18 днів тому +2

    Twa taka kukubaliwa na wahindi na waarabu lakini twajapata katika tabu,

    • @stambuliwash.abdillahinass8123
      @stambuliwash.abdillahinass8123  18 днів тому +1

      Si mambo ya kutaka kukubaliwa na Waarabu na Wahindi, bali, hawa Waarabu na Wahindi ni wenzetu kama walivyo watu wengine wowote! Tunachosisitiza hapa ni kuwa kila Mkenya aelewe kuwa hata sisi tuna haki kama Mkenya mwengine yoyote (hatufadhiliwi, ni haki yetu)! Ni muhimu ifahamike kuwa tumenyanyaswa na kudhulumiwa kwa muda mrefu sana! Sasa tumeamka, na tunadai haki zetu.

  • @Masjidfirdous-onlinetv
    @Masjidfirdous-onlinetv 16 днів тому

    Assalamualaikum warahmatullah wabarakaut.Naomba kuuliza ni kwanini Huy Jemshid bun Abdullah hakurusiwa kuingia nchini Oman mpaka baada ya kifo cha Sultan qabous 2021??

  • @salimmachila5736
    @salimmachila5736 18 днів тому +1

    Stambuli ni kiungo muhimu mwambao wa pwani

  • @SalimMatano-r1c
    @SalimMatano-r1c 18 днів тому +1

    Viziri sana

  • @ramseyhusseinkhamis8258
    @ramseyhusseinkhamis8258 19 днів тому +1

    Assalamu alaykum sheikh Stambul: mie ningependa kujua Zanzibar ilikua na ukubwa gani na na ni maeneo gani hasa
    Asante sana

    • @abubakarrahim8482
      @abubakarrahim8482 18 днів тому +2

      Zanzibar maeneo maeneo yake ni kuanzia warsheikh ilioko somalia ama kwaurahisi mogadishu na ufuo wake pamoja na visiwa vyake mpaka kilwa ukiangalia map ya zamani utawaona ufuo wa pwani uliokuwa kwenye utawala wa zanzibar.

    • @ramseyhusseinkhamis8258
      @ramseyhusseinkhamis8258 18 днів тому +2

      Asante sheikh, napenda sana kusikiliza Darssa zako kuna mengi napata kujifunza.
      Allah atakulipa inshaAllah!

    • @stambuliwash.abdillahinass8123
      @stambuliwash.abdillahinass8123  18 днів тому +2

      @@abubakarrahim8482 Inshaa'Allah, tutayaeleza kwa kina kwenye makala wakati wa kuyaeleza ukifika .

    • @NyumbaYaHekima
      @NyumbaYaHekima 18 днів тому

      Asli, zanzibar ni kisiwa cha unguja tu, mpka waomani wanakuja kutawala, huu mwambao ulikuwa ukitawaliwa na wareno na kila pahala pakiwa na watawala wake wakienyeji. Walipokuja walipokuja waomani ndio jina zanzibar likabeba maeneo yote ya mwambao wanayoyatawala. Ingawaje mda mwengine kwenye nyaraka ilionyesha Zanzibar ni kisiwa cha unguja tu. Lkn nje ya mwambao likawa ni jina linalowakilisha maeneo yote ya utawala wao, kwa vile makao makuu yao yapo unguja, na jina linasadifu maeneo yote ya karibu.

    • @abubakarrahim8482
      @abubakarrahim8482 18 днів тому

      @@stambuliwash.abdillahinass8123 inshaa Allah tunakuombea uzima na afya professor wetu tunapata faida sana mashaa Allah

  • @lenniefei6710
    @lenniefei6710 18 днів тому +2

    Waarabu tangu jadi ni watu wakuenda kinyume na mambo ndio maana waliletewa mitume mingi ili kuwanyoosha lakini bado wamepinda hadi leo......Wameshika utawala sehemu za watu na kuziuza bila khiari ya wenyeji, kuweka mikataba na wasiokua waislamu eti kuwalinda na ziadi ya hayo wamehusika pakubwa katika kuanguka kwa Khilafa mwaka 1920s.
    Ubaguzi wa kirangi kwao ndio destruri licha ya Mtume Mohammad (S.A.W) kukemea sana upuuzi na ujinga huu !....DINI KWAO NI DESTURI TU WALA SIO IMANI !

    • @rayaalhabsi1725
      @rayaalhabsi1725 18 днів тому

      Walio kuwa waki letewa mitume ni mayahudi sio waarabu nenda kasome na upate elimu

    • @lenniefei6710
      @lenniefei6710 18 днів тому +1

      @rayaalhabsi1725 Hud.. Saleh...Shuaib....Mohd. Wangapi hao ?!

    • @rayaalhabsi1725
      @rayaalhabsi1725 18 днів тому

      @lenniefei6710 MOHAMMAD SAW pekee ndio alikuwa ni mwarabu na ametumwa kwa wote duniani sio kwa warabu tu.pamoja wewe. Na hao ulio wataja pamoja huyo mnae mwita yesu wali tumwa kwa makabila yao only

    • @NassorOmarDadi
      @NassorOmarDadi 18 днів тому

      Mitume walio waarabu ni wachache sana kuliko Mitume ambao wazungu. Kwa hio Mitume wazungu ni wengi kuliko Mitume ambao ni waarab jua hivo

    • @lenniefei6710
      @lenniefei6710 18 днів тому +1

      @NassorOmarDadi Mitume wazungu ndio wepi ?!....Tafuta Qur'an walau ya tafsir ujielimishe kwanza kuliko kujiaibisha bure !

  • @lenniefei6710
    @lenniefei6710 18 днів тому +1

    Serikali ya kenya hakuna isilolijua katika maswala ya Mwambao hata moja, na kuna wengi baina ya waMwambao wanaonufaika katika hali ilivyo baada ya 8 October 1963.......YASHAMWAGIKA HAYO.....Twendeni nalo !!!

    • @stambuliwash.abdillahinass8123
      @stambuliwash.abdillahinass8123  18 днів тому

      Kwa hakika, wako wengi miongoni mwa waliowahi kutawala na wanaotawala nchini Kenya ambao hawayajui mengi miongoni mwa tunayojadili hivi sasa. Lakini, naamini, kwa radhi za Mwenyezi Mngu, wengi wataelewa.

  • @omarkapula588
    @omarkapula588 18 днів тому

    Kuna watu wanaojiita gumzo la ghasan ni vibaraka wa sultan wao wanaona hakuna mwenye haki ya kuitawala zanzibar zaidi ya Jamshed shukran sana bwana Stambuli kwa makala yako sasa tutapumua kutoka kwa hao vibaraka wa sultan

    • @moxasaidi3398
      @moxasaidi3398 17 днів тому

      Wewe kichwa kibovu na hujamuelewa bado alie kuja kuitawala zanzibar ni muengereza na sio muoman kwasababu muomani alikuwa ni kibaraka tuu mwenye nguvu zote za kupanga alikuwa ni muengereza

    • @jumaseifjuma4185
      @jumaseifjuma4185 16 днів тому

      Wenye haki ya kuitawala Zanzibar ni Watanganyika kama tuonavyo hivi. Gumzo la Ghasan ni watoa taaluma tu kama huyu wewe isikukere, hutaki usimsikilize lkn Historia siku zote huwezi kuipindisha ukweli utabakia kuwa ni ukweli tu.

  • @mussajuma7460
    @mussajuma7460 18 днів тому +2

    Mzee wetu si ukubali kusema kweli tu kwamba Mombasa ilikuwa ni sehemu ya Zanzibar

    • @b.truthful
      @b.truthful 18 днів тому

      Ilikuwa ni sehemu moja

    • @solomonadams6337
      @solomonadams6337 18 днів тому

      Hakuna asie jua kwamba Mombasa ilikua ni sehemu ya Zinjibar.

    • @NyumbaYaHekima
      @NyumbaYaHekima 18 днів тому

      @@mussajuma7460 hii hawaitaki, hawataki kuambiwa wao ni sehemu ya zanzibar. Watu wa zanzibar si sawa na wao. Wao wamestaarabika zaidi. Na inaonekana maamuzi ya mwambao kutenguliwa zanzibar ni maamuzi ya watu wenyew wa mwambao, ni wachache ndio walitaka mwambao ubaki ndani ya zanzibar.

  • @ahmedsharif2424
    @ahmedsharif2424 18 днів тому +1

    Huyo shehe aongea yalio tupata na mateso yalio tuathiri mpaka Leo hii

    • @AhmedZahor
      @AhmedZahor 18 днів тому

      @@ahmedsharif2424 umeathirika na nini hebu tuambie lililokuathiri huyo babu nadhani ni mtu wa Mambasa na Mombasa Kenya ipo mikononi mwao hicho kilokuathiri nini

  • @RecapAI
    @RecapAI 19 днів тому +4

    Kwenye kitabu cha the Portuguese time in east africa. Kinasema kuwa walipokuja ni kwasababu tuliwasaliti kimkataba baina yao na otoman. Maana aliposhuka mportuguese alikuta waturuki. Je tulikuwa na uhusuano na ottoman kabla ya sultan wa oman?

    • @stambuliwash.abdillahinass8123
      @stambuliwash.abdillahinass8123  19 днів тому +4

      Kwa hakika, tulikuwa na uhusiano mwema na watu wote wa ulimwengu wa kwanza (First World) kwa kuwa huo ulimwengu wa kwanza ulikuwa ni sehemu ya bara Arabu, Ghuba la Uajemi (Persia), bara Hindi, China na sehemu kubwa ya Mashariki ya mbali (Far East) pamoja na huku kwetu.

    • @RecapAI
      @RecapAI 19 днів тому

      @stambuliwash.abdillahinass8123 asante kwa ufafanuzi mwafaka

    • @kuzonga222
      @kuzonga222 19 днів тому

      Pamoja sana twafwatilia kwa makini

    • @salimmachila5736
      @salimmachila5736 18 днів тому

      Watu wa Mombasa tumetawaliwa na wachwana 😮😮

    • @AliMohamed-w3b
      @AliMohamed-w3b 18 днів тому

      ​@@salimmachila5736hapana, tumetawaliwa na kulala kwetu

  • @SalimMatano-r1c
    @SalimMatano-r1c 18 днів тому +1

    Stambuli miminaona nikweli maana adi Sasa akujabadili mambomingi yanafaywa bila ya sisi wapwani

  • @SaadSameer-r9u
    @SaadSameer-r9u 17 днів тому

    Makala mzuri yenye kusisimua na kusikitisha. Lakini ni vipi ije baada ya Sultan wa mwisho kufa?

  • @NoelNjementi
    @NoelNjementi 19 днів тому

    Hahaaaa mkuu kwaiyo pwani yafaa jitenga badara yakuungana

    • @stambuliwash.abdillahinass8123
      @stambuliwash.abdillahinass8123  18 днів тому

      Kwa hakika, mimi sijasema hayo! Nnaloomba mimi ni kila anayenisikiza atumiye masikio yake vyema (astumiye moyo kunisikiliza)! Kisha, akishasikiza kwa makini, atumiye akili yake kupima nnayoyaeleza, na hatimaye, akate shauri kuhusu aliyoyasikia. Si sawa kusikiza ninayosema, kisha, unasema mambo amabayo sikuyasema (unadhaniya tu).

  • @SalimMatano-r1c
    @SalimMatano-r1c 18 днів тому +1

    Afadhali tugebaki na wareno mambo yasigekua ivi

  • @2002-h6c
    @2002-h6c 18 днів тому +1

    Hata kiswahili wee babu hikijui, kisha unajifanya Mzanzibari, kazi kweli kweli 😂

    • @NyumbaYaHekima
      @NyumbaYaHekima 18 днів тому

      unaonekana siasa za watu wa pwani huzijui wala hujayafahamu mazungumzo, mana huyo mzungumzaji kabisa haonekani kuridhishwa mombasa ilkuwa sehemu ya Zanzibar

    • @2002-h6c
      @2002-h6c 17 днів тому

      @NyumbaYaHekima Pwani pwani !!! watu tunaijua Zanzibar na Pwani kuliko wewe , usitake ufanye kuijua wani au Zanzibar ati lazima mtu awe na fikra kama zako, fikra za kukataa asili yako na kujipendekeza kwa watu wenye asili nyengine.

    • @NyumbaYaHekima
      @NyumbaYaHekima 17 днів тому

      @@2002-h6c mm nakuona wewe ndio unataka niwe na fikra kama zako, ivi unamchagulia mtu asemee yeye ni nani!, na ntakuwa na mahusiano naye ni maamuzi yangu sio yako. Watu wa bara asli yao wakiishi kwa makabila, hili suala la kuona watu wa pwani wameishi na wageni bado hamligahamu linawezekana vipi kwa sababu si katka asli yenu kuishi na watu wa kabila tofauti. Kwaio usinambie mie kuhusu asli yako. Keep it to yourself. Ni asli yetu kuishi na watu.

    • @2002-h6c
      @2002-h6c 17 днів тому

      @NyumbaYaHekima Hiyo ndo shida yako, nani kakwambia mie ni mtu wa bara ? yaani wewe ukiona mtu ana mawazo ya kizalendo ya kuupenda Uafrica wake, basi unaona huyo ni mtu wa bara na siyo Muislam, that's not right , and that's why I think you need to change your pescepltion on people , especially Zanzibaris

    • @NyumbaYaHekima
      @NyumbaYaHekima 17 днів тому

      @@2002-h6c hilo si kosa langu, hakuna kuwa mzalendo wa rangi yako na kabila lako kuliko kuwa mzalendo wa Uislamu. Tumekubali kuwa waislanu tuzikubali fikra za uislamu na tuachane ni izo takataka za urangi na ukabila. Hakun uafrika mbele ya uislamu. Uislamu kwanza. Na ukiwa na fikra izo za kimakabila hujaukubali uislamu sawaswa, kama kuna makosa yanafanywa na waarabu ni jukumu letu kama waislanu kuelekezana tuachane na tabia mbovu sio kuvunja udugu wetu kwa sababu ya rangi zetu.

  • @muhammednassor3569
    @muhammednassor3569 18 днів тому

    Waliwaghalibu au walikuwa hawawezi kujiendesha

  • @salimaloufi6470
    @salimaloufi6470 17 днів тому +1

    WAINGEREZA NDIO WALOGAWA MATAIFA DON'T FORGET DIVIDE AND RULE GO BACK AT HISTORY , DON'T SPOIL HISTORY

    • @febamohammed2989
      @febamohammed2989 15 днів тому

      Elewa kwanza kabla ucomment,,alieitawala pwani ya kenya ni mkoloni muarabu muengereza alikua anapeana ulinzi tu maana walieke mikata ya ulinzi,,na utawala wa waarabu ulikua wakibaguzi kama ule uliokua afrika kusini,,watu wa mombasa waligaanywa makundi matatu waarabu,waswahili na wanyika au makafiri,,walioktaa utawala wa waarabh waliitwa wanyika na makafiri na hawakuruhisiwa kutangamana na ndugu zao waliotaka kujipendekeza na waarabu hata shule wadigo walikatazwa kusoma maana walijulikana kama wanyika

  • @AliMohamed-w3b
    @AliMohamed-w3b 18 днів тому

    Serikali ya Kenya haiwezi kukubali majadiliano haya Bro

  • @ArsenalThegunnerz
    @ArsenalThegunnerz 19 днів тому

    Karne moja tokea kuanguka kwa othman empaire sai dola inarudi kama ilivyoanza makkah sai ni quds

  • @aishathabit3732
    @aishathabit3732 17 днів тому

    Huyu ni mbaguzi sana anachuki na waarab kwa msukumo wa Iran
    Anajifanya mjuzi wa historia lakini hathubutu kuwalaani watawala wa kweli wa Znz ambao ni waingereza na waarab walikuwa matarishi tu kwa waingereza

  • @NyumbaYaHekima
    @NyumbaYaHekima 18 днів тому

    Assalaam alaikum,
    Mimi kwa kiasi naona tuna tatizo tunavyoyajadili mambo haya kwa kufanya utawala wa usultani kama kwa watawala si katika sisi. Ni kweli kuna makosa yamefanyika lkn mbona mizani hatutumii sawasawa, sheikh unafahamu kabla ya ujio wa waomani watawala wakienyeji wa baadhi ya sehemu za mwambao kama lamu na unguja walikuwa na ushirika na wareno, mpk mda mwengine wakiwapa msaada kuwapiga ndugu zao hao wenyeji, je haya yalikuwa sawa kwa sababu ni wenyeji. Utakuta kufahamiana kwa watawala wa kienyeji na wereno kumeleta maafa makubwa kwa wenyeji kuliko hayo ya waomani na waengereza, lkn kwenye kujadili ya waomani ndio huwa makubwa kuliko mengine, waislamu wote ni sawa, na kama kuna makosa yote yahisabiwe sawa. Lkn tatizo lipo kwenye umimi.

    • @Nehemiaayo-b8c
      @Nehemiaayo-b8c 18 днів тому

      tatizo lako udini

    • @NyumbaYaHekima
      @NyumbaYaHekima 18 днів тому +1

      @Nehemiaayo-b8c nimezingumza kama muislamu na nimezungumza na muislamu, subiri mazungumzo yanayokuhusu ndio uchangie

  • @salimaloufi6470
    @salimaloufi6470 17 днів тому

    JUST TO REMIND THE GENTLEMAN'S HISTORY AT 1800 THERE'S NO COUNTRY CALLED RAS ALKHAIMAH OR DUBAI OR ABUDHABI WHICH NOW CALLED UNITED ARAB EMIRATES THIS ESTABLISHED AT 1970😂

  • @azizamri1522
    @azizamri1522 18 днів тому +1

    Soma huo ukweli badala ya kutia fitna. Wewe WaOmani wamefunya nini hata unatapakaza chuki kila siku? Twambie ukwell!

    • @NyumbaYaHekima
      @NyumbaYaHekima 18 днів тому

      mimi husema watu wa mwambao wamepatwa na virus ileile iliosababisha mauwaji unguja, kuona waarabu hawakufaa kutawala hapo kwao, wakisahau ktk uislamu suala la utawala halina rangi. mtawala wa waliojikubali kuwa waislamu anaweza kuwa yoyote ambae atatunza uslama wa watu na haki zao bila ya kujadili asli yake. leo wanamsingizia sultani kauza mwambao, lkn ukweli waseme wasione haya, wao ndio walikata shauri hilo, na sultani akjuilishwa hivyo, tena walitaka sultani afanye vipi?! hisabu zao ilkuwa ni kuja kutengeneza nchi yao kando, lkn wamejikuta hawaganduki kwenye mikono ya watu wengine. ni wachache ndio walikubali kubaki chini ya sultani.

  • @ahmedsharif2424
    @ahmedsharif2424 18 днів тому

    Wacheni matusi kwahisani zenu

  • @febamohammed2989
    @febamohammed2989 15 днів тому

    Na mbona huwa unasema mijikenda walikuja miaka 300 iliopita kumbe kuna wadigo waliokwenda kuita waarabu kusaidia kumtoa mreno,,au kwa tafsiri yako mdigo sio mijkenda?

  • @NyumbaYaHekima
    @NyumbaYaHekima 18 днів тому +2

    Jambo lengine ni kwamba waislamu wa mwambao kudhani kwamba serekali ya kenya inaweza kukubali iwaache wajitenge eti kwa kuzungumza nao, hilo suala tulitowe kweny vichwa vyetu, hakuna mtu anaachia mamlaka kwa mazungumzo, mazungumzo yanafanya kazi baina wa watu wawili wenye nguvu zenye kulingana au kwa external influence inayoweza kuwasaidia, si kwa kusema mukae na serekali ya kenya muwaeleze, hakuna kitu watawaeleweni hapo.

    • @stambuliwash.abdillahinass8123
      @stambuliwash.abdillahinass8123  18 днів тому

      Kwa hakika, hakuna fikra hiyo ya kujitenga hapa. Lililoko ni watu kujadili na kukubaliana kwamba watu wa Pwani wana haki kama Mkenya mwengine yoyote (iwapo si zaidi) kutokana na kuwa wamekuwako kwenye ufuo huu wa Mwambao wa Pwani kwa muda mrefu kuliko Wakenya wengi kuwako kwenye sehemu nyengine za nchi inayojulikana kuwa Kenya hivi leo!

    • @NyumbaYaHekima
      @NyumbaYaHekima 18 днів тому

      ​@@stambuliwash.abdillahinass8123maneno haya hayajanyooka kwa mtu mwenye akili timamu. Tuache kutafunatafuna maneno. Mwambao kutenganishwa na Zanzibar kuunganishwa na bara ilkuwa ni kosa kubwa tulikubali. Tusione haya kusema. Eti haki maalum kwa watu wa mwambao, siku wakiwafahamu bila ya shindikizo mumshukuru mungu.

    • @NyumbaYaHekima
      @NyumbaYaHekima 18 днів тому

      @@stambuliwash.abdillahinass8123 unatka kusema, kulikuwa na tatizo mombasa kuwa sehemu ya zanzibar lkn ni sawa kuwa sehemu ya kenya?!! ni kwamba mupewe usawa tu!

  • @Dr.zaidi4
    @Dr.zaidi4 18 днів тому +3

    Mwaarabu ni msaliti mpaka kesho.
    Anatupumbaza kwa Kutufunika na dini

  • @ahmedsharif2424
    @ahmedsharif2424 18 днів тому +2

    Shehe umekubali waarabu wametusaliti, mpaka Leo hii wanakula na wazungu neema za mafuta. Sijasikia waarabu wametoa Msaada WA pesa kuwasaidia waafrica

  • @AliMohamed-w3b
    @AliMohamed-w3b 18 днів тому +4

    Waarabu wametuuzia Mombasa yetu bila ya kutushauri, kwao hawaoni dhambi kufanya hivyo sababu wameshefanya worst zaidi ya hilo, yaani kuuza Binadamu

    • @HusseinMustafaParmar
      @HusseinMustafaParmar 18 днів тому

      Waarabu sio wote wana ubaya

    • @AliMohamed-w3b
      @AliMohamed-w3b 18 днів тому +4

      @HusseinMustafaParmar hata mimi pia nimuarabu lakini Mtume S.A.W. amesema ukweli usemwe hata kama ni uchungu

    • @AhmedZahor
      @AhmedZahor 18 днів тому

      @AliMohamed-w3b Wacheni Ujuha moi ekubali tu kuitoa Mambasa Na aloiuza Zanzibar jee pia Mwarabu

    • @AhmedZahor
      @AhmedZahor 18 днів тому

      @AliMohamed-w3b wacha Ujinga ilipotoka mombasa mtawala alikua Muengereza zanzibar ilikua chini ya Muengereza na aloitoa nchi kwa wa mrima ulishauriwa

    • @AliMohamed-w3b
      @AliMohamed-w3b 18 днів тому

      @AhmedZahor kwanza kajifunze kiswahili, pili wapi Moi alikubali? tatu zanzibar walifanya mapinduzi kufukuza hiyo sultanate lakini waingereza wacaoccupy baadae

  • @joachimmahoo9786
    @joachimmahoo9786 18 днів тому

    Waarabu waliwaona wa afrika kama tumbili ( renea horuna ya samia kwa jeshi la polisi) CCP Moshi October 2024

    • @joachimmahoo9786
      @joachimmahoo9786 18 днів тому

      Wali peleka wa afrika ütüme anı na kuwaondoa koro donu imi wa izah na kuş ha uchaguzi ndani ya ardhi yao. Ushauri tunao

  • @BarakaTsama
    @BarakaTsama 19 днів тому

    Ni nini hasa chanzo cha usiqwata pwani,kisha ajabu ukisikia mtu amevunjiwa makaazi yake,mwenye kumiliki,sanasana utapata eti shamba ni ya mwarabu ama kuna dhuluma bado ya mwarabu kudhulumu mijikenda kama walivyo wafanya watumwa na kuwauza zama za mababu

    • @mwambaowapwanichannel8572
      @mwambaowapwanichannel8572 19 днів тому +1

      shida ya mijikenda hajui nani amemyaganya ardhi waitiki ni muarabu?
      shamba la makonge vipingo limenyakuliwa na waarabu?
      nenda chakama hadi marafa tafuta nani anamiliki mother title,

    • @lenniefei6710
      @lenniefei6710 18 днів тому

      Hakuna Mmijikenda yeyote aliyepokonywa ardhi na waarabu na kama yupo asimame mmoja tu ! Hizo ardhi wanazasema ziliporwa zote zina mother Titles za tangu jadi na hakuna Mmijikenda aliekua anaishi humo hadi juzijuzi tu ndio wamezivamia na kujidai ni zao !

  • @SalimMatano-r1c
    @SalimMatano-r1c 18 днів тому

    Stambuli miminaona nikweli maana adi Sasa akujabadili mambomingi yanafaywa bila ya sisi wapwani

  • @salimaloufi6470
    @salimaloufi6470 17 днів тому

    WAINGEREZA NDIO WALOGAWA MATAIFA DON'T FORGET DIVIDE AND RULE GO BACK AT HISTORY , DON'T SPOIL HISTORY