Maisha Kamili
Maisha Kamili
  • 152
  • 12 357
Kumpendeza Mungu? Siri ya Mungu Kupendezwa na Watu Wake | Lesson 3 || 14/01/2025
Inawezekanaje kwamba Mungu wa ulimwengu wote apendezwe na wanadamu tu, matone ya muda mfupi ya sehemu hai za seli katika sayari moja ndogo katikati ya kile ambacho huenda ni ulimwengu usio na ukomo? Inawezekanaje kwamba wanadamu wanakuwa wa maana/ sana kwa Mungu, aliye na uweza wote na asiyehitaji chochote? Maswali haya yanaweza kuchanganuliwa katika vipengele viwili. Kwanza, Mungu Mwenyewe anawezaje kufurahishwa? Pili, wanadamu wanawezaje kumfurahisha, hasa kutokana na hali yetu ya dhambi? Kipengele cha kwanza cha maswali haya ni mada ya leo na kipengele pili ni mada ya kesho.
Soma Isaya 43:4; Zaburi 149:4; na Mithali 15:8, 9. Hutuambia nini kuhusu Mungu kupendezwa na watu Wake?
Kama tulivyoona kwa sehemu ya jana, Mungu anaweza kupendezwa na wanadamu kwa sababu Mungu anawapenda watu kwa namna ya kuzingatia masilahi yao ya juu kabisa, kama ambavyo mtu yeyote anayewapenda na kuwajali wengine.
Kinyume chake, Mungu huchukizwa na watu Wake wanapofanya maovu. Kwa kweli, Mithali 15:8, 9 inafundisha kwamba, ingawa “sadaka” na “njia” ya waovu ni “chukizo kwa BWANA,” “maombi ya mwenye haki ni furaha yake” na “Yeye humpenda [mtu] afuataye haki.” Siyo tu kwamba aya hii inaonesha kwamba Mungu anachukizwa na uovu, lakini huonesha kwamba anafurahia wema. Pia inaweka furaha na upendo wa Mungu katika uhusiano wa moja kwa moja wa kila kimoja kwa chenzake, kuonesha uhusiano wa kina kati ya upendo wa Mungu na furaha Yake, unaoonekana katika Maandiko yote.
Kulingana na Zaburi 146:8, “BWANA huwapenda wenye haki.” 2 Wakorintho 9:7 inaongeza, “Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.” Angalia, kwanza, kile ambacho aya hizi hazisemi. Hazisemi kwamba Mungu anawapenda waadilifu tu au kwamba Mungu anampenda tu atoaye kwa moyo mkunjufu. Mungu anampenda kila mtu. Hata hivyo, ili maandiko haya yawasilishe jambo, ni lazima yamaanishe kwamba Mungu anampenda “mwenye haki” na “atoaye kwa moyo wa ukunjufu” katika maana fulani ya pekee. Kile tulichoona katika Mithali 15:8, 9 kinatoa dokezo: Mungu anawapenda hawa na wengine katika maana ya kupendezwa nao.
Fikiria jinsi mbingu na dunia zinavyofungamana kwa ukaribu kiasi kwamba Mwumbaji wa ulimwengu wote, anaweza kujihusisha kukupa tumaini gani, hasa ikiwa unapitia wakati wa dhiki?
Переглядів: 3

Відео

Mwokozi Akishangilia: Sikukuu ya Wokovu | Lesson 3 || 13/01/2025
Переглядів 312 години тому
Ingawa ni vigumu kwetu kuelewa, Mungu anamwona kila mtu kuwa wa thamani isiyopimika, ndiyo maana anafurahia wokovu wa hata roho moja. Soma Sefania 3:17. Aya hii inafafanuaje mfano wa mwana mpotevu? Sefania 3:17 inaonesha kwa mkazo furaha ya Mungu juu ya watu Wake waliokombolewa. Karibia kila neno linalomaanisha furaha na shangwe katika lugha ya Kiebrania limetumiwa katika aya hii moja, likielez...
Wenye Thamani Kuliko Tuwazavyo: Watu Machoni pa Mungu | Lesson 3 || 12/01/2025
Переглядів 444 години тому
Kama tulivyoona katika somo lililotangulia, hakuna mtu -hata mwenye dhambi mbaya kabisa au mwovu kuliko wote-ambaye Mungu hampendi. Na kwa sababu Mungu anawathamini watu zaidi ya vile tunavyoweza kufikiria, anachukizwa na dhambi kwa sababu anatupenda na anajua dhambi inachotufanyia, pia. Soma Luka 15:11-32. Mfano wa mwana mpotevu unafunua nini kuhusu huruma na upendo wa Mungu? Unatoa onyo gani ...
10 January 2025
Переглядів 349 годин тому
10 January 2025
Jibu Letu kwa Neema ya Mungu: Mmepewa Bure, Toeni Bure | Lesson 2 || 09/01/2025
Переглядів 8412 годин тому
Kama ambavyo mtumishi asingeweza kamwe kulipa deni lake kwa bwana wake, kamwe hatuwezi kumlipa Mungu. Tusingeweza kamwe kuufanyia kazi au kustahili upendo wa Mungu. “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi” (Rum. 5:8). Ni upendo wa ajabu kiasi gani! Kama vile 1 Yohana 3:1 inavyosema, “Tazameni, ni pendo la ...
Upendo ni Zawadi au Dhamana? Rehema Iliyopotezwa | Lesson 2 || 08/01/2025
Переглядів 3814 годин тому
Upendo wa Mungu ni wa milele na haustahiliwi. Hata hivyo, wanadamu wanaweza kuukataa. Tunayo nafasi ya kuukubali au kuukataa upendo huo, lakini kwa sababu tu Mungu anatupenda bila masharti kwa upendo Wake mkamilifu, wa milele kabla ya chochote tunachofanya (Yer. 31:3). Upendo wetu kwa Mungu ni mwitikio wa kile ambacho tayari tumepewa hata kabla hatujaomba. Soma 1 Yohana 4:7-20, ukiwa na msisiti...
Je, Tunaweza Kupoteza Upendo wa Mungu? Uhusiano Wenye Masharti | Lesson 2 || 07/01/2025
Переглядів 13716 годин тому
Mungu huita na kumwalika kila mtu katika uhusiano wa karibu zaidi wa upendo Naye (Tazama Mt. 22:1-14). Kuitikia wito huu inavyofaa kunahusisha utii kwa amri ya Mungu ya kumpenda Mungu, na kuwapenda wengine (tazama Mt. 22:37-39). Kwa mtu kupata manufaa ya uhusiano huu na Mungu inategemea ikiwa mtu ataamua kwa hiari kuukubali au kuukataa upendo Wake. Soma Hosea 9:15, Yeremia 16:5, Warumi 11:22 na...
Kuingia Bila Masharti, Lakini Si Bila Masharti Kubakia: Upendo wa Kiagano | Lesson 2 || 06/01/2025
Переглядів 5919 годин тому
Mara nyingi Biblia inaelezea uhusiano wa pekee wa upendo wa Mungu nasi kwa kutumia sitiari za familia au uhusiano wa damu, hasa sitiari za upendo kati ya mume na mke au wa mama mwema kwa mtoto wake. Sitiari hizi hutumiwa hasa kuelezea uhusiano maalum kati ya Mungu na watu Wake wa agano. Huu ni uhusiano wa upendo wa kiagano, ambao hauhusishi tu upendo wa Mungu kwa watu Wake lakini pia matarajio ...
Mungu Anapenda Kila Mtu: Upendo wa Mungu wa Milele | SS Lesson 2 || 05/01/2025
Переглядів 4821 годину тому
Maandiko yako wazi: Mungu anampenda kila mtu. Aya maarufu zaidi ya Maandiko, Yohana 3:16, inatangaza ukweli huu: “ ‘Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.’ ” Soma Zaburi 33:5 na Zaburi 145:9. Aya hizi zinafundisha nini kuhusu jinsi fadhili, huruma na rehema za Mungu zilivyo pana? Wengine wanaweza ...
Mungu wa Upendo na Haki: Tafakari Zaidi na Jadili Nasi | SS Lesson 1 || 03/01/2025
Переглядів 56День тому
Soma Ellen G. White, “ ‘To Meet the Bridegroom,’ ” ukurasa wa 405-421, katika kitabu cha Christ’s Object Lessons. “Giza linaloifunika dunia ni kutokuelewa Mungu. Watu wanakosa kumjua Mungu jinsi alivyo. Wamekuwa wakimkosoa na kumtafsiri vibaya. Wakati huu ujumbe kutoka kwa Mungu unapaswa kutangazwa, ujumbe wenye nguvu ya kuokoa na kuangaza. Tabia Yake inapaswa kujulikana. Mwangaza wa utukufu Wa...
Ishara Ya Upendo wa Mungu: Alisulubiwa Kwa Ajili Yetu | SS Lesson 1 || 02/01/2025
Переглядів 67День тому
Mungu anawakaribisha watu wote katika uhusiano wa upendo naye, lakini wale tu wanaokubali mwaliko huo kwa hiari ndio wanaofurahia matokeo ya milele. Kama inavyoonekana katika mfano wa karamu ya harusi, wengi ambao mfalme aliwaita " 'hawakutaka kuja' " (Mathayo 22:3). Kwa hiyo, muda mfupi kabla ya kusulubiwa kwake, Kristo aliomboleza: " 'Ee Yerusalemu, Yerusalemu, mwauwaji wa manabii na mwarogi ...
Wengi Wameitwa, Wachache Wamechaguliwa | SS Lesson 1 || 01/01/2025
Переглядів 45День тому
Mungu si tu anawapenda watu kwa hiari Yake, bali pia anawaalika wampende. Ukweli kwamba anawapa uhuru wa kuchagua kumkubali au kumkataa unaonekana wazi katika mfano wa karamu ya arusi (Mathayo 22:1-14). Mfano wa karamu ya arusi una maana gani? Katika mfano huo, mfalme aliandaa karamu ya arusi kwa mwanawe na kutuma watumishi wake kuwaita wageni. Lakini walikataa kuja (Mathayo 22:2-3). Mfalme ali...
Jinsi Mungu Asivyolazimika Kutupenda: Upendo Usio na Masharti | SS Lesson 1 || 31/12/2024
Переглядів 6814 днів тому
Upendo Wake Ni Zawadi Tupu Mungu aliendelea kuwapenda Waisraeli licha ya uasi wao mara kwa mara. Vivyo hivyo, Mungu anaendelea kutupenda sisi, hata tukiwa watenda dhambi. Hatuustahili upendo Wake, wala hatuwezi kuupata kwa kujitahidi. Zaidi ya hayo, Mungu hatuhitaji sisi. Biblia inasema Mungu haitaji kitu chochote (Matendo 17:25). Upendo Wake kwetu ni zawadi ya bure. Linganisha Ufunuo 4:11 na Z...
Mungu Hupenda Hata Wanaomlipa Mabaya: Upendo Usiolipa Mabaya | SS Lesson 1 || 30/12/2024
Переглядів 4514 днів тому
Mfano wa kushangaza wa upendo wa Mungu kwa wanadamu walioanguka unapatikana katika hadithi ya Hosea. Mungu alimwamuru nabii Hosea, “ ‘Nenda, ukachukue mke wa uasherati na watoto wa uasherati, kwa maana nchi imefanya uzinzi mkuu kwa kuondoka kwa Bwana’ ” (Hos. 1:2, NKJV). Hosea na mkewe asiye mwaminifu walikuwa kielelezo hai cha upendo wa Mungu kwa watu wake, hata licha ya ukafiri wa Israeli na ...
Mungu Anapenda Watu: Zaidi ya Matarajio ya Kawaida || SS Lesson 1 || 29/12/2024
Переглядів 6014 днів тому
Zaidi ya Matarajio ya Kawaida Mungu hatuulizi tu, "Je, wanipenda?" bali Mungu mwenyewe anampenda kila mtu, na anafanya hivyo kwa uhuru. Kweli, anatupenda wewe na mimi na kila mtu mwingine zaidi ya tunavyoweza kufikiria. Na tunaujua upendo huu kupitia jinsi alivyotenda katika historia ya watu wake. Soma Kutoka 33:15-22 na utafakari muktadha wa mistari hii na masimulizi yanayojitokeza. Je, kifung...
Jifunze zaidi & Jadili Nasi | Hitimisho: Kumjua Yesu & Neno Lake || Somo 13 || 27/12/2024
Переглядів 3814 днів тому
Jifunze zaidi & Jadili Nasi | Hitimisho: Kumjua Yesu & Neno Lake || Somo 13 || 27/12/2024
Siri ya Ukuaji Kiroho: Kukaa Ndani ya Yesu || Mwongozo wa Kujifunza Biblia | Somo 13 || 26/12/2024
Переглядів 4614 днів тому
Siri ya Ukuaji Kiroho: Kukaa Ndani ya Yesu || Mwongozo wa Kujifunza Biblia | Somo 13 || 26/12/2024
Njia ya Kumjua Mungu: Teolojia Toka “Juu” au Toka “Chini” || Kujifunza Biblia: Somo 13 | 24/12/2024
Переглядів 5214 днів тому
Njia ya Kumjua Mungu: Teolojia Toka “Juu” au Toka “Chini” || Kujifunza Biblia: Somo 13 | 24/12/2024
Chaguo Kati ya Uzima na Mauti: Nuru na Giza || Mwongozo wa Kujifunza Biblia | Somo 13 || 24/12/2024
Переглядів 4821 день тому
Chaguo Kati ya Uzima na Mauti: Nuru na Giza || Mwongozo wa Kujifunza Biblia | Somo 13 || 24/12/2024
Swali Lisilo Sahihi na Jibu la Yesu: Kudumu Kumtaza Yesu || Somo 13 || 23/ 12/ 2024
Переглядів 6921 день тому
Swali Lisilo Sahihi na Jibu la Yesu: Kudumu Kumtaza Yesu || Somo 13 || 23/ 12/ 2024
Kukutana Huko Gallilaya: Kutoka Uvuvi hadi Huduma || Somo 13 | 22/ 12/ 2024 || Pr Enos Mwakalindile
Переглядів 8021 день тому
Kukutana Huko Gallilaya: Kutoka Uvuvi hadi Huduma || Somo 13 | 22/ 12/ 2024 || Pr Enos Mwakalindile
Kumjua Yesu na Neno Lake: Utata na Utatuzi Wake || Somo 13 | 21/ 12/ 2024 || Pr Enos Mwakalindile
Переглядів 5221 день тому
Kumjua Yesu na Neno Lake: Utata na Utatuzi Wake || Somo 13 | 21/ 12/ 2024 || Pr Enos Mwakalindile
Saa ya Utukufu: Msalaba na Ufufuo || Mjadala wa Somo 12 | 19/ 12/ 2024 || Pr Enos Mwakalindile
Переглядів 3921 день тому
Saa ya Utukufu: Msalaba na Ufufuo || Mjadala wa Somo 12 | 19/ 12/ 2024 || Pr Enos Mwakalindile
Yesu na Mariamu: Kutoka Huzuni hadi Furaha || Somo 12 | 19/ 12/ 2024 || Pr Enos Mwakalindile
Переглядів 6621 день тому
Yesu na Mariamu: Kutoka Huzuni hadi Furaha || Somo 12 | 19/ 12/ 2024 || Pr Enos Mwakalindile
Kaburi Tupu: Ushuhuda wa Kaburi la Yesu || Somo 12 | 18/ 12/ 2024
Переглядів 4221 день тому
Kaburi Tupu: Ushuhuda wa Kaburi la Yesu || Somo 12 | 18/ 12/ 2024
"Imekwisha": Machozi, Ukweli & Tamko la Ushindi | | Somo 12 | 17/ 12/ 2024
Переглядів 11128 днів тому
"Imekwisha": Machozi, Ukweli & Tamko la Ushindi | | Somo 12 | 17/ 12/ 2024
Mtazameni Mtu Huyu! Yesu Mbele ya Mahakama ya Umma | | Somo 12 | 15/ 12/ 2024
Переглядів 8628 днів тому
Mtazameni Mtu Huyu! Yesu Mbele ya Mahakama ya Umma | | Somo 12 | 15/ 12/ 2024
Kweli ni Nini? | Swali la Pilato & Jibu la Yesu | Somo 12 | 15/ 12/ 2024
Переглядів 8128 днів тому
Kweli ni Nini? | Swali la Pilato & Jibu la Yesu | Somo 12 | 15/ 12/ 2024
Saa ya Utukufu: Msalaba na Ufufuo | Somo 12 | 14/ 12/ 2024
Переглядів 5328 днів тому
Saa ya Utukufu: Msalaba na Ufufuo | Somo 12 | 14/ 12/ 2024
Jifunze Zaidi & Jadiliana Nasi | Baba, Mwana, na Roho | Somo 11 | 13/ 12/ 2024
Переглядів 67Місяць тому
Jifunze Zaidi & Jadiliana Nasi | Baba, Mwana, na Roho | Somo 11 | 13/ 12/ 2024

КОМЕНТАРІ