Shamba hub
Shamba hub
  • 81
  • 84 110
IFAHAMU MBEGU BORA YA MPUNGA II MKOMBOZI KWA MKULIMA NA BIASHARA
#farming #kilimo #agriculture #rice #mpunga #mchele
ONDOO MUHIMU ZA KILIMO CHA NYANYA CHENYE TIJA
1. Changua mbegu bora
Hiki ni kipengele muhimu na cha kwanza kabisa kuzingatia, kwa kuwa mavuno mengi kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na ubora wa mbegu uliyotumia.
Chagua mbegu yenye mavuno mengi, inayokubalika sokoni kwa vitu kama umbo la tunda, ukubwa wa tunda, ugumu wa tunda n.k, inayostahamili hali ya hewa, inayokomaa mapema yenye ukinzani dhidi ya magonjwa na wadudu waharibifu, na mwisho kabisa nunua kwenye kampuni moja kwa moja au kwa muuza pembejeo anayeaminika.
* Tumia mbolea
Zao la nyanya linahitaji mbolea kwa wingi, lipo kwenye kundi la mazao yanayohitaji mbolea ya kutosha (heavy feeders)
Tumia mbolea ya asili (samadi au mboji) iliyooza vizuri kiasi cha tani 10-15/ekari wiki 2-3 kabla ya kupanda/kuotesha.
Mbolea ya kiwandani kiasi cha gramu 10-15 kwa kila mmea kila unapoweka mbolea.
Mbolea inayowekwa kwa kiwango stahiki na kwa wakati itakusaidia kupata mavuno mengi.
* Hakikisha kwenye udongo kuna unyevunyevu muda wote
Hii itasaidia kwanza kuupoza mmea, kusafirisha virutubisho kutoka kwenye mizizi hadi kwenye mmea wote hivyo kuimarisha mfumo wa mmea, inazuia tatizo la tunda la nyanya kuoza kwenye ncha, inazuia mmea kudondosha maua/matunda kwa ajili ya stress ya maji.
Nimezungumzia unyevunyevu na si maji kutuama, kwa kuwa maji yakituama zaidi ya siku 2 au saa 48 ni hatari kwa zao la nyanya, kwa sababu mizizi itakosa hewa na hatimaye mmea kufa
* Dhibiti magonjwa na wadudu waharibifu kwa wakati
Tumia mbinu shirikishi za kudhibiti wadudu waharibifu na magonjwa, ikiwemo kukagua shamba lako mara kwa mara na ikibidi kila siku (scouting), hii itakusaidia kugundua tatizo mapema na kulipatia ufumbuzi kama kung’oa mmea ulioathirika ili isiambukize mingine, kilimo cha mzunguko(crop rotation), mbinu za kibaolijia (biological control), Mbegu zenye ukinzani (resistant varieties) n.k.
* Hali ya hewa
Zao la nyanya hustawi kwenye joto la wastani, si baridi sana wala joto sana kuanzia nyuzijoto 21-28 huwa zinaonekana kufaa.
Umbali kutoka usawa wa bahari 0-2000, ingawa sehemu za chini sana kama Dar es salaam kwa kawaida huwa zina joto sana hadi nyuzi joto 35 hivyo nyanya hupata stress ya joto na kudodosha maua/matunda, kwa maeneo kama hayo yanafaa kulima nyanya joto likipungua ama tumia aina mbegu inayostahamili stress ya joto (heat set variety).
* Kabla ya kulima tumia mpango biashara (business case) kujua gharama na mapato
nawapa hii ndoo muhimu ili ikusaidie kujua nikilima ekari moja ya nyanya nitatumia bei gani kwenye mbegu bora, maji ya kumwagilia, utafiti wa soko yaani wapi utauza zao lako likiwa tayari (usianze kutafuta soko baada ya kuvuna, anzia sokoni) fahamu kuhusu masoko makubwa ya nyanya na bei zake.
Kwa bei ya soko la mbali nitauza sh ngapi kwa kreti na soko la karibu ni sh ngap, vitu kama gharama za usafirishaji zikoje n.k
Hi itakupa picha kamili na kujaribu kukisia kuwa nimekosa sana nitapata faida hii, nimepata vizuri nitaweka mfukoni bei gani.
Mwisho
vipengele vyote nilivyotaja hapo juu vinategemeana, kama mbegu ikiwa si bora hata ukiwa na mbolea nzuri, viuatilifu vyenye ubora havitasaidia sana utaishia kupata mavuno kidogo, kuna mbegu hata uihudumie vipi ndiyo kwanza imedumaa na inazaa matunda madogo yasiyokubalika sokoni. Pia ukitumia mbego bora, mbolea nzuri & viuatilifu vyenye ubora wakati hujui soko lako ukavuna bei ikochini sana bado utapata hasara pia.
Переглядів: 40

Відео

JE WEWE NI MKULIMA WA NYANYA CHUKUA HIZI DONDOO MUHIMU ZA KUZINGATIA
Переглядів 4719 годин тому
#farming #kilimo #agriculture #tomato #tomatoes #nyanya
DONDOO MUHIMU ZA KILIMO CHA MPUNGA II MAANDALIZI II MBOLEA II MAVUNO
Переглядів 9814 днів тому
#mpunga #rice #ricefarming #riceagriculture #kilimochampunga #kilimo #farming #agriculture
TAFITI ZA MBEGU ZILIZOFANYIKA TANZANIA | BUNGENI LEO | DAVID SILINDE | BENKI YA MBEGU ZA ASILI
Переглядів 4228 днів тому
Naibu Waziri wa Kilimo akijibu maswali ya Wabunge Bungeni, Tarehe 29.10.2024 #bungenileo #kilimo #farming #agriculture
MAABARA YA UZALISHAJI WA MBEGU ZA VIAZI MVIRINGO KWA NJIA YA CHUPA HAITUMII MCHANGA
Переглядів 626Місяць тому
MAABARA YA UZALISHAJI WA MBEGU ZA VIAZI MVIRINGO KWA NJIA YA CHUPA HAITUMII MCHANGA
TAZAMA WAKULIMA WALIVYOIBIWA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 200 "ALIYEHAMISHWA ARUDISHWE"
Переглядів 28Місяць тому
TAZAMA WAKULIMA WALIVYOIBIWA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 200 "ALIYEHAMISHWA ARUDISHWE"
FAIDA ZA KITALU NYUMBA | GREENHOUSE | TEKNOLOJIA YA KISASA KWENYE KILIMO
Переглядів 114Місяць тому
KILIMO CHA KITALU NYUMBA Faida za Kilimo cha Teknolojia ya Kitalu Nyumba (Greenhouse) 1: Kuzalisha mazao mengi katika eneo dogo. 2: Kuzalisha mazao yenye ubora zaidi. 3: Uwezo wa kudhibiti hali ya hewa (micro climate) ndani ya greenhouse hatimaye kutengeneza mazingira mazuri ya ukuaji wa mimea. 4: Kumwezesha Mkulima kuzalisha wakati wowote, kwa kuwa kitalu nyumba hutumia kilimo cha umwagiliaji....
KILIMO BORA CHA VITUNGUU MAJI I MAMBO YA KUZINGATIA | MBEGU BORA ZA VITUNGUU | KILIMO CHA KISASA
Переглядів 1,5 тис.Місяць тому
Fahamu taratibu za Msingi katika Kilimo cha Vitunguu maji. 01. Maandalizi ya Shamba na eneo (Udongo) 02. Vipimo katika Kulima 03. Uchaguzi wa Mbegu 04. Namna ya Upandaji 05.Muda wa kuandaa mbegu 06. Kuandaa matuta na kupanda 07. Kupalilia, Aina ya Mbolea etc. #farming #kilimo #agriculture #onion #vitunguu #mbeya #tanzania
UZALISHAJI WA MBEGU ZA VIAZI MVIRINGO II MBEGU BORA, TAZAMA MAAJABU YA MBEGU HII
Переглядів 1,1 тис.Місяць тому
#farming #kilimo #viazi #potato
KILIMO CHA CARROT NA TARATIBU ZAKE
Переглядів 4332 місяці тому
#CARROT #farming #kilimo #karoti #agriculture
KILIMO BORA CHA VIAZI MVIRINGO NA MBINU ZAKE - AINA MPYA YA MBEGU ITAKAYOKUSHANGAZA
Переглядів 6492 місяці тому
#farming #kilimo #potato #viazi #viazimbatata #agriculture #viazimviringo
KILIMO BORA CHA KABICHI NA TARATIBU ZAKE II KILIMO BIASHARA
Переглядів 8602 місяці тому
#kabichi #kabeji #cabage #kilimo #ufugaji
JE UNATAKA KUKUZA KIPATO CHAKO KUPITIA KILIMO CHA MATANGO I MBEGU BORA
Переглядів 5502 місяці тому
#matango #tango #cucumber #farming #agriculture #shambahubtz Karibu ufahamu na ujifunze kuhusu kilimo cha matango kutoka kwa msimamizi msaidizi ya vitaru nyumba kutoka Chuo cha Kilimo na Kituo cha Uwasilishaji wa Teknolojia Bora za Kilimo.
TAZAMA MAAJABU YA AINA HII YA NYANYA I FAIDA KUBWA SEHEMU NDOGO I MTI MREFU
Переглядів 2163 місяці тому
#agriculture #farming #farmer #tomato #kilimo #trending Mtazamaji wa Shamba Hub Leo tunakuletea Makala haya ya Kilimo cha Nyanya Kutoka katika chuo cha kilimo na kituo cha uwasilishaji wa teknolojia bora za kilimo kwa Wakulima Uyole Mbeya Tanzania. Karibu tujifunze mbinu mbalimbali zitakazotupatia faida kubwa.
KINACHOENDELEA KWENYE MRADI WA BBT (BUILDING A BETTER TOMORROW - DODOMA)
Переглядів 605Рік тому
Tazama kinachoendelea katika mafunzo ya Mradi wa Vijana wa Building A Better Tomorrow Bihawana Dodoma. Karibu katika Mitandao yetu ya Kijamii kufahamu zaidi: Twitter : shambahubtz Instagram : shambahub_tz #kilimobiashara #buildingabettertomorrow #bbt #dodoma #kilimo #songwe #Tanzania #technology
MFAHAMU BILIONEA WA ZAO LA KAHAWA KUTOKA MKOANI SONGWE
Переглядів 2,3 тис.Рік тому
MFAHAMU BILIONEA WA ZAO LA KAHAWA KUTOKA MKOANI SONGWE
#FAHAMU UGONJWA UNAOATHIRI KAHAWA CBD | DAWA ZA KUZUIA NA KINGA | KAHAWA YA VIKONYO
Переглядів 613Рік тому
#FAHAMU UGONJWA UNAOATHIRI KAHAWA CBD | DAWA ZA KUZUIA NA KINGA | KAHAWA YA VIKONYO
#FAHAMU KILIMO CHA KAHAWA | SHAMBA DARASA | JINSI YA KUPANDA KWA VIPIMO | MBOLEA KUPANDIA NA KUKUZIA
Переглядів 4,5 тис.Рік тому
#FAHAMU KILIMO CHA KAHAWA | SHAMBA DARASA | JINSI YA KUPANDA KWA VIPIMO | MBOLEA KUPANDIA NA KUKUZIA
FAIDA ZA ZAO LA KAHAWA KWA WAKULIMA WADOGO | MRADI WA PACE | SOLIDARIDAD | TaCRI | SHAMBA DARASA
Переглядів 177Рік тому
FAIDA ZA ZAO LA KAHAWA KWA WAKULIMA WADOGO | MRADI WA PACE | SOLIDARIDAD | TaCRI | SHAMBA DARASA
#FAHAMU KILIMO CHA KAHAWA | FAIDA | MBEGU ZA COMPACT/ CHOTARA | SIFA ZAKE | AFYA YA UDONGO |MAGONJWA
Переглядів 867Рік тому
#FAHAMU KILIMO CHA KAHAWA | FAIDA | MBEGU ZA COMPACT/ CHOTARA | SIFA ZAKE | AFYA YA UDONGO |MAGONJWA
MKUTANO WA PROGRAM YA BUILDING A BETTER TOMORROW | USHIRIKI WA MASHIRIKA BINAFSI | DODOMA
Переглядів 109Рік тому
MKUTANO WA PROGRAM YA BUILDING A BETTER TOMORROW | USHIRIKI WA MASHIRIKA BINAFSI | DODOMA
MICHE YA KAHAWA COMPACT | KILIMO CHA KAHAWA | PASSPORT TO COFFEE EXPORT | PACE | SOLIDARIDAD
Переглядів 20Рік тому
MICHE YA KAHAWA COMPACT | KILIMO CHA KAHAWA | PASSPORT TO COFFEE EXPORT | PACE | SOLIDARIDAD
KILIMO CHA MAHINDI NA MPUNGA |LIMA KISASA | MATUMIZI YA ZANA BORA ZA KILIMO | AGRICOM TANZANIA
Переглядів 3 тис.Рік тому
KILIMO CHA MAHINDI NA MPUNGA |LIMA KISASA | MATUMIZI YA ZANA BORA ZA KILIMO | AGRICOM TANZANIA
KILIMO CHA KAHAWA | SOLIDARIDAD | MRADI WA PACE | MBEYA | SONGWE | SEHEMU YA PILI
Переглядів 45Рік тому
KILIMO CHA KAHAWA | SOLIDARIDAD | MRADI WA PACE | MBEYA | SONGWE | SEHEMU YA PILI
KILIMO CHA KAHAWA | SOLIDARIDAD | MRADI WA PACE | MBEYA | SONGWE
Переглядів 39Рік тому
KILIMO CHA KAHAWA | SOLIDARIDAD | MRADI WA PACE | MBEYA | SONGWE
RAIS SAMIA SULUHU HASSAN | FOOD 2 DAKAR SUMMIT | FOOD SUMMIT | TANZANIA | KENYA | PRESIDENT UTO
Переглядів 80Рік тому
RAIS SAMIA SULUHU HASSAN | FOOD 2 DAKAR SUMMIT | FOOD SUMMIT | TANZANIA | KENYA | PRESIDENT UTO
MFUMUKO WA BEI YA CHAKULA TANZANIA NINI KIFANYIKE | ZUHURA YUNUS | WAZIRI BASHE |WAANDISHI WA HABARI
Переглядів 208Рік тому
MFUMUKO WA BEI YA CHAKULA TANZANIA NINI KIFANYIKE | ZUHURA YUNUS | WAZIRI BASHE |WAANDISHI WA HABARI
MATEMBEZI MRADI WA TANPAC DODOMA
Переглядів 191Рік тому
MATEMBEZI MRADI WA TANPAC DODOMA
BASHE:TANZANIA INAHITAJI WASTANI WA TANI MILIONI 13-15 ZA CHAKULA KWA MWAKA
Переглядів 89Рік тому
BASHE:TANZANIA INAHITAJI WASTANI WA TANI MILIONI 13-15 ZA CHAKULA KWA MWAKA
WIZARA YA KILIMO YAJA NA MIKAKATI KUKUZA KILIMO CHA MBOGAMBOGA KATIKA MAUZO HADI KUFIKIA DOLA BIL1.2
Переглядів 82Рік тому
WIZARA YA KILIMO YAJA NA MIKAKATI KUKUZA KILIMO CHA MBOGAMBOGA KATIKA MAUZO HADI KUFIKIA DOLA BIL1.2

КОМЕНТАРІ