Hawa ndio Waliodhulumiwa roho zao 1972, nchini Zanzibar
Вставка
- Опубліковано 28 вер 2024
- Mnamo mwishoni mwa mwaka wa 1970, Serikali ya Mavamizi ya Zanzibar kama kawaida yake iliwakamata wananchi wengi sana kwa singizio lao hilo hilo la kila siku "kutaka kuipindua Serikali ya Wananchi"!!
Miongoni mwa waliyokamatwa wakati huo, walikuwemo, Mabwana hawa:
Salim Ahmed Busaidi
Abdalla Suleiman Riyami
Othman Soud
Azizi Bualy
Hemed Said
Mohammed Juma
Mohammed Hamza
Musa Ali
Said Hamoud.
Wananchi hao baada ya kukamatwa na kuwekwa kizuwizini, walipelekwa mbele ya mkutano wa hadhara uliyoandaliwa makusudi kwa ajili yao katika uwanja wa Maisara, Unguja, kati ya mwaka wa 1971. Serikali ya Mavamizi ya Zanzibar, kwa kutaka kudanganya Ulimwengu na wananchi wa Zanzibar, walileta katika mkutano huo bunduki na silaha nyengine ndogo ndogo kuwa ati wamekamatwa nazo wananchi hao.
Pia pamoja na hizo silaha, ililetwa bendera na kusemwa kwamba bendera iyo ndiyo
walitaka wakamatwa hao iwe bendera ya Nchi baada ya kufuzu hayo mapinduzi yao! Hayo hayakutosha, bali Serikali ya Mavamizi, iliwatumilia baadhi ya maofisa wake wa kijeshi wengi wao wakiwamo hao wenye kujiita, "progressives" kuja kusema uwongo wa kuwahilikisha wananchi wenziwao kwa ajili ya
kutafuta maslahi ya nafsi zao. Maofisa hao waongo, walisema mbele ya umma kuwa ati hao wananchi waliokamatwa walikuwa wakipanga pamoja nao mipango ya kuipindua Serikali ya wananchi.
Bali wao, yaani hao maofisa waongo, walikuwa wakiripoti kwa wakubwa wao kila khatua zilizokuwa zikifanyika. Mpaka ulipofika wakati, ndipo ilipoarifiwa Idara ya Usalama na kutakiwa wafanye kazi yake. Idara ya
Usalama iliwakamata wote pamoja na silaha zao ambazo ndizo hizo hapo!! Kilaaliyekuwepo katika mkutano huo na kila aliyesikia hadithi hizo, ila aliyekuwa hana akili timamu au amezidiwa na chuki, aliweza kutambua kuwa yote hayo yalikuwa ni mazingaombwe ya uwongo uliyokuwa umepangwa na baadhi ya wakuu maalumu wa Serikali ya Mavamizi kwa makusudio yao maalumu.
Baada ya kusemwa uwongo huo, Karume aliwasimamisha baadhi ya hao wadhulumiwa mbele ya umma uliokuwepo hapo na aliwanazii kwa matusi, na aliwakejeli kwa kiasi alichopenda mwenyewe. Baada ya hapo, alitoa hukumu ya kuwaweka gerezani. Kazi zao alizokuwa amezitangaza mbele ya mkutano huo, zilikuwa za "Kuchunga n'gombe" huko Hanyegwa Mchana. Baada ya kuuliwa Karume, April 7, 1972 na kutawalishwa AlHajj Aboud Jumbe, wananchi hao wadhulumiwa, wote walichukuliwa kutoka magerezani na kwenda kuuliwa kwa kupigwa marisasi siku moja. Baada ya kuuliwa, wote walitumbukizwa katika shimo moja.
Yale yaliyofanyika hivi karibuni huko Ruwanda si ajabu kuwa wameyaiga kwa yaliofanyika Zanzibar. Kuiga maovu ni rahisi! Baadhi ya hao maofisa waliokubali kusema uwongo kuwazulia ndugu zao wakati huo, hivi sasa baada ya kuwa na wao yeshawafika ya kuwafika kwa matokeo ya kuuliwa Mzee Karume, ati ndio wanasema kwa
sauti za majuto na za kusikitika kuwa, "Yale yote tulioyasema siku ile mbele ya mkutano ule yalikuwa ni maneno ya kupangiwa na wakubwa wetu tuyaseme, kwa hakika yote yalikuwa ni maneno ya uwongo"!!
Hao ndio "progressives" wetu, wapenda maendeleo. Wametumiliwa kuivamia Serikali ya halali iliyochaguliwa na wananchi kwa uchaguzi wa kidemokrasi wa "One Man One Vote". "Progressives" hao hao ndio waliotumiliwa kwa maslahi ya nafsi zao kwa kusema uwongo uliopelekea kuuliwa kwa
wananchi wenziwao bila ya kuwa na makosa yoyote. "Progressives" hao hao ndio waliotumiliwa tena, mara hii katika mipango ya kumuuwa Karume!! Si ajabu kuwa hivi sasa "progressives" hao hao wamo mbioni wakitumiliwa, wakijuwa au bila ya kujuwa, katika mipango na njama za kuleta vurugu kupitia huu "Mfumo wa Vyama Vingi" tulioletewa, bali na katika mengineyo. Watu kama hawa khatari kuwanao.
Daima yafaa kuepukwa. #HistoriaYaZanzibar
So sad
Wanzanzibar leo et mnasherekea siku ya mapinduz hamjui kuwa siku hiyo zilipotea roh za watu tena waislam wenzetu ndio walouliwa mujuwe t mukisherekea bc munasherekea damu za watu namutawalip zoho zao sk ya sik
ALLAHU AKBAR
ulikuwa kwa upanga utakufa kwa upanga ndiomaneno mazito ya qanitukufu
Innalillah Wainna Ilaiyh Raji'uun. Kwa hakika Zanzibar tokea 1964 mpaka hii ni kama moto ambao unawaka ndani ya pango. Zanzibar inahitaji kufanyiwa visomo vizito damu za watu zimemwangwa sana.
The sultans never did this.
Marxism socialism communism brutal and dictatoship of Nyerere
Hemu asimame kiongozi mkuu wa nchiii hiii kisha atueleze kinaga ubaga hichi kilicho tokea hapa haswa kilikua nini na kinamaana gani na tafsiri yake ni nini kimsingi
Wazanzibar wanachukiana wao kwa wao kuliko hata wanavyotichukia Tanganyika. Wakipta nafasi ya kujitawala basi damu itamwagika sana Zanzbar na inaweza isiwe nchi inayotawalika kwa miaka mingi sana
Inna lillah wainna ilayhi 😭😭😭😭
Innallilah wainna ilaih rajiun hawa wanaouliwa ni waislamu wenzetu duuh
Waislam wanakufa syria lebanon na Gaza
Mombasa na maneno yalio tammkwa Siku Sonko alishinda kesi Mombasa, Inna mapishi ya ukatili Kama huo.... Kama Kenya itaendelea na mfumo ya kura za kabila kubwa kutawala
Katiba ya maskizano iitwao Bomas Draft lazima iwe ndio njia ya kupeleka inchi
Najisi mkubwa Malawi 🇲🇼 huna uzanzubari mchwara
Mh watu wanauliwaa
Allah Akbar
Hee watu wanauliwa wao wanafurahia
Dhulma tuuu nchi hiii