DKT. MPANGO AELEZA SABABU ZA KUTOENDELEA NA UMAKAMU
Вставка
- Опубліковано 11 лют 2025
- Dkt. Mpango afichua siri ya kutoendelea na Umakamu
Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango kwa mara ya kwanza ameweka wazi sababu za kutotaka kuendelea na nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza katika kikao kazi cha tano cha Serikali Mtandao kinachofanyika mkoani Arusha, Dkt. Mpango amesema watanzania wengi kwa sasa umri wao ni wa ujana, na kwa umri wake anaamini huu ni wakati wa kukipa nafasi kizazi kipya.
“Mheshimiwa Simbachawene ni mchokozi, lakini labda niseme kidogo. Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, wataalamu wanasema takribani asilimia 77 ya watanzania sasa ni vijana. Mimi nimetumika serikalini kwa muda wa kutosha, na sasa ifikapo mwezi Julai nitakuwa na miaka 68,” amesema Dkt. Mpango