SIRI IMEVUJA: Ijue Sababu ya Prof. Jay Kuchelewa Kuoa

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 2 гру 2024
  • SUBSCRIBE NOW / uwazi1
    Nicholaus Haule A.K.A Black Rhyno, ambaye ni mdogo wa Prof Jay, amefungukia harusi ya kaka yake, akieleza jinsi familia ilivyolipokea suala la ndoa ya Prof Jay na jinsi alivyomshawishi kaka yake huyo kuoa.
    Akizungumza na Global TV Online kwenye Ukumbi wa Mlimani City ilikofanyia shereha hiyo, Black Rhyno amefunguka kwamba yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kuoa kwenye familia yao, ambapo alifunga ndoa miaka mitano iliyopita akiwa ndiye mdogo kuliko wote kwenye familia.
    SUBSCRIBE NOW / uwazi1
    Joseph Haule 'Profesa Jay' amefunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi, Grace Mgonjo. Ndoa ya Prof Jay ambaye ni Mbunge Jimbo la Mikumi kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ilifungwa mchana wa Jumamosi, JULAI 08, 2017, katika Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar na usiku mpango mzima ulihamia kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar ambapo mastaa kibao akiwemo Diamond Platnumz na waheshimiwa wengine kibao walijumuika.
    “Namshukuru Mungu nimetimiza ahadi ya ndoa kwa mchumba wangu ambaye tumepitia mabonde na milima,” alisema Profesa Jay baada ya kutoka kanisani hapo.
    Profesa Jay, kabla ya ndoa hiyo, yeye na Grace wamejaliwa mtoto mmoja wa kike.
    Shoo ya Diamond kwenye harusi hiyo ilibamba mno na kuwafanya wanakamati wawe na kazi ya ziada ya kutuliza watu watulie kwenye siti zao.
    #Global TV Online, kwa kushirikiana na TBC 1, wanakuletea taarifa ya habari iliyosheheni matukio mbalimbali nchi nzima.
    Visit globalpublishe..., Subscribe / uwazi1
    Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya…
    / uwazi1
    / uwazi1
    / uwazi1
    WEBSITE: globalpublishe...
    FACEBOOK: / globalpublishers
    TWITTER: / globalhabari
    INSTAGRAM: / globalpublishers

КОМЕНТАРІ • 19