#LIVE

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 11 гру 2024

КОМЕНТАРІ • 4

  • @ikupamercykabigumila1377
    @ikupamercykabigumila1377 2 роки тому +2

    NAMNA MUNGU HUINUA WATU.
    Pastor Dickson Cornel Kabigumila.
    Lengo la somo:
    Kuonyesha baadhi ya njia ambazo Mungu anatumia kumuinua mtu bila kujali elimu, familia anayotoka, anajua nini au hajui nini. Ilimradi, baada ya kujua njia hizi, nianze kuzifanya kuwa maisha yangu na tabia yangu na Mungu ataniinua.
    Mungu hana watu maalum.
    God does not have special people. Everyone who is available can become special.
    Njia Mungu anatumia kuinua Watu:
    Kupitia Neema Maalum. 1 Wakorinto 15:9, 10. Kuna Neema maalum inayofanya Mungu achague mtu ambaye hakustahili ambaye hana vigezo. Kugundua hii Neema ya kuinua wasio stahili mimi pia nina fuzu kunufaika nayo. 1 Wakorinto 1:27. Ukuu kwenye jambo au eneo fulani ni Neema. Neema hii inafanya kazi kwenye eneo la bidii. Ili Mungu anipe Neema hii maalum ya kunipa kitu ambacho kikawaida nisingeweza kuwa nacho, au uwezo wa kufanya jambo ambalo nisingefanya ni lazima niwe mtu wa bidii. Kigezo kikubwa cha kupata Neema maalum ni bidii. Mithali 21:5. Je ninafanya nini sirini kinachoweza kumshawishi Mungu? Mungu ananiinua anapojiridhisha nami. Mungu kabla ya kumuinua mtu anamfanyia mazoezi mengi. Kumbukumbu la Torati 8:1-3. Mwanzo 22:17.
    Kupitia Roho ya Hekima na Akili. 1 Wafalme 4:29; 3:11. Kila kitu ambacho Mungu amekitoa kwa wengine ni hundi wazi kwamba hilo jambo kwa Mungu lipo na anaweza kutoa na kwangu pia. 1 Wafalme 3:16-23; 10:1-10. Hekima ya Mungu na Akili za kimungu zinanipa uwezo wa kutatua kila swali, kila changamoto. Hekima inapaswa kujibu maswali na kutatua mafumbo. Kipimo ya kwamba nimeanza kutembea katika hekima na akili ya Mungu ni kuanza kutatua mali katika jamii. Hekima sio kitu cha kujificha(cha rohoni tu), sio maneno tu, inapaswa ihame toka rohoni iwe matokeo, iwe kitu kinachoonekana, kiwe kitu chenye uwezo wa kuleta masuluhisho na majibu.
    Hekima ni uwezo wa kufanya vitu kwa usahihi.
    Hekima ni uwezo wa kuwa na masuluhisho.
    Hekima inapimwa kwenye maeneo yafuatayo: Ulaji, Uvaaji, Mazungumzo, Uwezo wa kuweka akiba, Kujitenga na dhambi.
    Success is when an opportunity meets preparation.
    You dress how you want to be addressed.
    The best way to be promoted is to seek the Spirit of Wisdom and Understanding.
    Watu ambao Mungu amewainua kupitia platform ya Hekima na Akili:-
    ✓. Suleiman. 1 Kings 10:1-10
    ✓. Yusuphu. Mwanzo 41:33-44
    Mtu anayeweka akiba ni ushahidi kwamba anaona zaidi ya leo. Mtu mwenye imani kwaajili ya maisha marefu anafanya vitu vinavyozidi leo.
    NAHITAJI ROHO MTAKATIFU ANAYEPIMWA KWA MATOKEO.
    Kama ilivyokuwa kwa Yusuphu.
    NAHITAJI ROHO YA HEKIMA MAALUM INAYOJENGA VITU VINAVYOONEKANA NA KUSHIKIKA.
    ✓. Daniel. Danieli 1:1-20
    Kujitenga na uovu kunaongeza akili.
    Kumcha Mungu, kujitenga na dhambi, kunazalisha akili safi na njema.
    Psalm 111:10

  • @janemdulla8191
    @janemdulla8191 2 роки тому

    Ameeeen

  • @marygadau4443
    @marygadau4443 2 роки тому

    Eeh, baba dickson ana hekima kwakweli

  • @rehemasareyo1793
    @rehemasareyo1793 2 роки тому

    Ninajifunza