MATESO YATOKANAYO NA VIFUNGO VYA FAMILIA - PASTOR SUNBELLA KYANDO

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 8 лют 2022
  • Zekaria 1:18 -21
    Nami nikainua macho yangu, nikaona, na tazama, pembe nne. Nami nikamwuliza yule malaika aliyesema nami, Nini hizi? Naye akanijibu, Hizi ndizo pembe zilizowatawanya watu wa Yuda, na Israeli, na Yerusalemu. Kisha BWANA akanionyesha wafua chuma wanne. Ndipo nikauliza Hawa wanakuja kufanya nini? Akasema kwamba, Hizi ndizo pembe zilizowatawanya watu wa Yuda, hata ikawa hakuna mtu aliyeinua kichwa chake; lakini hawa wamekuja kuzifukuza, kuziangusha pembe za mataifa, walioinua pembe yao juu ya nchi ya Yuda, ili kuwatawanya watu wake.
    Katika Yuda hakuna mtu aliyekuwa anaweza kuinua kichwa chake( kukua &kuongezeka) kwa sababu ya zile pembe.
    Hili jambo unaweza kuliona hata kwenye maisha ya kawaida. Kuna familia zinaweza kufika sehemu fulani (kimafanikio) lakini haziwezi kuvuka sehemu fulani.
    Mtu atachukua mkopo, atapata ushauri mzuri lakini utakuta mwenzake aliyepewa ushauri kama wa kwake anafanikiwa lakini yeye hata ajitahidi vipi hawezi kufanikiwa.
    Kwanini? - Kwasababu vita ya mwenzake sio kama vita yake. Mwenzake hakuna pembe iliyosimama kuhakikisha maisha yake hayaendi lakini yeye kuna pembe ambayo inahakikisha familia, ukoo wake HAUSOGEI.
    Kabla hujaumia kuwa kwanini HAUSOGEI mbali na jitihada unazoweka tafuta kujua ni kwanini/nini kinakuzuia kusogea.
    #PastorSunbella Kyando#Vifungo#Familia

КОМЕНТАРІ • 41

  • @joycekaje8755
    @joycekaje8755 2 роки тому +4

    Asante Pastor Sanbella, Mungu akupe maisha marefu utufungue. Nafuata mahubiri yako nikiwa Netherlands 🇳🇱, Nabarikiwa, najitambua ninastahili maombi ya namna gani,ili kufikia makusudi ya Mungu

  • @joshuamutua3727
    @joshuamutua3727 2 роки тому +2

    I like the instrumental background ...
    God bless you media pple....
    We are much blessed by this revalation

  • @salomemueni100
    @salomemueni100 2 роки тому +3

    Kwetu kenya..
    Nashukuru kujielewa baada ya kukusikiliza kwa huu ujumbe zacharia 1..pembe ambayo imetesa maisha yangu nimeigudua..hatua nitachukua..
    Asanti.
    AMEN

  • @superb1344
    @superb1344 2 роки тому +3

    Mtumishi ni kama umetumwa kwa ajili yangu

  • @ntulisuzan897
    @ntulisuzan897 Рік тому

    Asante Yesu Kwa Ufunuo unaouleta kipitia mtumishi wako nimebarikiwa🙏

  • @anethpalangyo6319
    @anethpalangyo6319 Рік тому

    Mungu azidi kuachilia mafuta zaidi juu Yako,viwango vya kukutumia viongezeke zaidi,umekuwa baraka sana kwangu

  • @faudhiasalum7279
    @faudhiasalum7279 Рік тому

    Ahsante daddy najifunza 🙌😢soma zuri sana tena kwa vitendo 🙌

  • @catherineaugustine7124
    @catherineaugustine7124 Рік тому +1

    Danu yako Y ESU INENE MEMA🙏🙏🙏

  • @amostinga770
    @amostinga770 Рік тому

    Namshukuru mungu katika magumu yangu najiona ndani ya mafundisho haya sawa naiman yatakwisha

  • @mahalawanamahalawana4019
    @mahalawanamahalawana4019 6 місяців тому

    Barikiwa sana mtumishi ❤

  • @charleskwiyukwa9186
    @charleskwiyukwa9186 2 роки тому +1

    Mungu azidi kukulinda mtumishi Sunbella

  • @pastorsamwelilusambo3517
    @pastorsamwelilusambo3517 Рік тому +1

    Amina

  • @catherineaugustine7124
    @catherineaugustine7124 Рік тому

    Mungu nataka umponye Claudius na maswaibu YALIYO mkuta, Mungu AMTENDEE na Damu ya Yesu ikanene mema

  • @holydanlow3291
    @holydanlow3291 Рік тому

    Amen karibu mombasa mtumishi wa mungu

  • @revinachingole6708
    @revinachingole6708 Рік тому

    Ni mimi akii Neema ya Mungu tu Pastor Sunbella ni mim nimechoka 24 years niko na madeni sijawahi kuonaa na saiv navo kwambia siko nyumbani watu zaid ya 20 hata sielew pesa zimeenda wap nimegomban na family nzima jamii inajua inavonichukulia sielew

  • @petermunuo1657
    @petermunuo1657 Рік тому +1

    Amen mtumishi barikiwa sana

  • @chengeson
    @chengeson Рік тому

    Mungu atusaidie tuna pitia mengi bila kujua chazno kilianzia wa

  • @nehemiahsima1389
    @nehemiahsima1389 2 роки тому

    Barikiwa sana mtumishi wa Mungu

  • @gaudensiagodwin3152
    @gaudensiagodwin3152 2 роки тому

    Amen mtumishi…tunaomba uje na mwanza

  • @victorvicent6036
    @victorvicent6036 Рік тому

    God bless you

  • @NeemaMgaya-ez9un
    @NeemaMgaya-ez9un 9 місяців тому

    Amina ubarikiwe

  • @user-yf9dd4rl8v
    @user-yf9dd4rl8v 6 місяців тому

    Amen

  • @bennamuchau6487
    @bennamuchau6487 2 роки тому

    Waiting

  • @heavenlight5084
    @heavenlight5084 Рік тому

    Mtumishi unayagusa maisha yangu

  • @christinamuherbwa4813
    @christinamuherbwa4813 2 роки тому

    Nayasubiri kwa moyo wangu mafundisho haya yamesaidiya sana spiritual life yangu nakuitambua vita ya familia yangu

  • @faudhiasalum7279
    @faudhiasalum7279 Рік тому

    Amen amen amen

  • @maribaisack2097
    @maribaisack2097 6 місяців тому +1

    Dah yani huyu ni mm kabisa yani 😢😢😢😢Mungu nisaidie

  • @mapenziluwa8061
    @mapenziluwa8061 Рік тому

    Mungu ni mkuu

  • @zakayomungai
    @zakayomungai 2 роки тому +2

    Neno la busara kwangu kujua mambo ya kiroho na vifungo

  • @FurahaSaidi
    @FurahaSaidi Рік тому

    Furaha

  • @peterjanuary7972
    @peterjanuary7972 Рік тому

    Duh umezungumza kitu kimoja kikubwaa sana..

  • @fionaalice9509
    @fionaalice9509 2 роки тому +2

    Huyu ni mimi kabisa,ilifunzu ni langu kabisa

  • @kknlghfblblanakere5946
    @kknlghfblblanakere5946 Рік тому

    Kwetu ziko zote nne pastor nsaidie kuomba umasikini, ndoa Elim etc plz mtumishi nsaidie ukweli nmefungwa nfungue pastor

  • @lifeinmiddleeast8179
    @lifeinmiddleeast8179 Рік тому

    Nina ushuhuda yaani napenda kukopa Sana hata bila sababu ya msingi na napenda kuuza rasilimali zangu na kuanza upya baadae najuta Sana , kwani nalipa madeni lakini kwa shida Sana na nikikopa nakosa Amani hata kama yule MTU hanidai cha kushangaza nikimkopesha mtu hanilipi na tunaishia kugombana

  • @bestinamaro7645
    @bestinamaro7645 2 роки тому

    Icho kimlio kingepungua kidogo wakati unaubiri

  • @enockmwasuluka8998
    @enockmwasuluka8998 Рік тому

    Naomba namba ya mtumishi Sunbela pls

  • @mankarichard5851
    @mankarichard5851 2 роки тому

    Please naomba mnilocate kanisan kwake

  • @elizabethmwachiti7987
    @elizabethmwachiti7987 2 роки тому

    Amina