SIKILIZA SHAIRI ZURI ZA KUHUSU HARUSI YA NDUGU WAWILI WATOTO WA SHARIFU HUSSEIN BADAWY huko Mamburui
Вставка
- Опубліковано 27 гру 2023
- Mwanzo naanza isimu ∆∆∆ Ya Mola wangu Jaliya.
Kiswalia na Hashimu ∆∆∆ Kipenzi tumwa Nabiya.
Na Ali zake Kiramu ∆∆∆ Na swahaba nao piya.
Nyuso leo zimeng'ara ∆∆∆ Kwa hili jambo la shani.
Nami kwenye msafara ∆∆∆ Sina budi kuwa ndani.
Kwetu ndio siku bora ∆∆∆ Ilomridhi Manani.
Ni bwana abubakari ∆∆∆ Na nduguye muhidini.
Wameianza safari ∆∆∆ Ya kuingia ndoani.
Naomba iwe ya kheri ∆∆∆ Kwa baraka za amini.
Pongezi wenye harusi ∆∆∆ Mambo yenu yamefana.
Kwa nguvu zake Qudusi ∆∆∆ Wana wamependezana.
Mola atawanafisi ∆∆∆ Kwa mahaba kushibana.
Ni kwako Abu alama ∆∆∆ Mja ulo na hisani.
Kwa kweli ulisimama ∆∆∆ Nae Sayidi Huseni.
Kwa wema na kwa huruma ∆∆∆ Mukajenga utu ndani.
Kazi tumeshuhudiya ∆∆∆ Uliyoifanya ndani.
Bidii na yako niya ∆∆∆ 'Metowa tunda mtini.
Leo chombo chaoleya ∆∆∆ Kimakini baharini.
Safari waloiunda ∆∆∆ Mola aijaze kheri.
Na chombo walichopanda ∆∆∆ Kisiingie dosari.
Kweli moyo ukipenda ∆∆∆ Roho haina khiari.
Ya Ilahi ya Rabana ∆∆∆ Ulo juu arshini.
Waruzukiye na wana ∆∆∆ Tena wakupenda dini.
Wasikiapo adhana ∆∆∆ Waende msikitini.
Hapa nitasema basi ∆∆∆ Mbele sitoendeleya.
Famili ya idarusi ∆∆∆ Na Huseni badawiya.
Yawashukuru unasi ∆∆∆ Nyote mulohudhuriya. - Розваги
Mashaallah
A.a ntaipata Vp Hizi Instromental Za Mashairi Broo
Mashaallah kaka