World Contraceptive Day Celebration in kakamega County

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 22 жов 2024
  • Afisa Mkuu wa Afya ya Umma wa Kaunti, George Mukodo, katika hafla ya kuadhimisha siku ya upangaji uzazi katika hospitali ya shibwe eneo bunge la Ikolomani aliwahimiza wanaume kukumbatia mipango ya uzazi, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wanandoa kwa ustawi wa familia zao.
    Mukodo alieleza kuwa ni muhimu kwa jamii kupata taarifa sahihi kuhusu huduma zinazofaa za kupanga uzazi kwa kila familia.
    Alibainisha kuwa mpango wa uzazi ni muhimu kwa kuhakikisha kuwa familia zinapata watoto ambao wanaweza kuwalea kwa mazingira bora.
    Mwenyekiti wa Kamati ya Afya katika Bunge la Kaunti ya Kakamega, Gladys Mukongolo, pia alisisitiza umuhimu wa kushiriki wanaume katika mijadala ya kupanga uzazi alitaka elimu maalum kutolewa kwa wanaume ili kuondoa hofu na dhana potovu zinazohusishwa na uzazi wa mpango.
    Wakati huo huo, Jacinta Oluoch kutoka idara ya kupanga uzazi ya kaunti hiyo, pamoja na Mkurugenzi wa Afya wa Kaunti, waliwarai wanaume kupuuza dhana potovu kuhusu kupanga uzazi na kushirikiana na wake zao kujenga familia ambazo wana uwezo wa kuzihudumia.
    Kaunti ya Kakamega Yarekodi Kupungua kwa Visa vya Mimba za Utotoni.
    Kaunti ya Kakamega imerekodi kupungua kwa idadi ya mimba za utotoni, kutoka visa 12,000 hadi 9,000 kwa sasa. Mke wa Gavana wa Kakamega, Janet Barasa, amesema kuwa mafanikio haya yametokana na mipango ya kuwahusisha wavulana na wasichana katika masuala ya afya ya hedhi.
    Janet alieleza kuwa wanapanga kupunguza zaidi visa hivi kwa kuendelea kuhusisha wavulana, na vilevile kuhakikisha kuwa wasichana na wavulana wanabaki shuleni kwa muda wote wa masomo.
    Aidha, wafadhili waliokuwepo katika hafla hiyo walisisitiza azma yao ya kuhakikisha wasichana wanahudhuria shule bila kukosa ili kutimiza malengo yao ya maisha.

КОМЕНТАРІ •