Kumpenda Mungu I kongamano la Roho Mtakatifu Jimbo la Njombe

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 22 жов 2024
  • MOYO WA KUMPENDA MUNGU (na Mwl Nelson Michael )
    Mathayo 22:34 - 40
    “Na mafarisayo waliposikia ya kwamba amewafumba kinywa wale masadukayo, walifanya shauri pamoja. Mmoja wao, mwana sharia, akamwuliza akimjaribu; mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo huu? Akamwambia, mpende Vwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii…..”
    Kila mtu anaweza kusema ya kuwa anampenda Mungu, hata wale tunao waona kama ni wadhambi, waganga, wachawi,washirikina, wauaji, mafisadi, wote ukiwauliza kama wanampenda Mungu, watajibu ndiyo.
    Lakini Mungu anataka tumpende kwa matendo yetu yaoneshe kuwa hakika tunampenda Mungu. Yesu anasema mafundisho yote ya Torati na manabii, yanalenga kuwafanya watu waelewe jinsi ya kumpenda Mungu. Kumpenda Mungu kuna hitaji kujitoa au kujizatiti.
    Luka 14:25
    ‘Mafarisayo walipo kuwa wanamfuata Yesu, aligeuka na kuwaambia kama mtu anataka kunifuata………………………”
    kwa kadiri ya neon tulilolisoma hapo juu, Yesu anaonesha vigezo vya kumpenda Mungu; yaani; Kumchukia Baba yako na Mama yako (wazazi walio kuzaa) na mke wako, uliye mtolea mahari na watoto wako na ndugu zako, waume na wake na hata nafsi yako mwenyewe.
    Nini maana ya neno hili?
    Yesu anasisitiza kuwa lazima uchukue msalaba wako na umfuate nyuma yake kiaminifu. Hapo ndipo utakapo kuwa mwanafunzi wake kwelikweli. Kumfuata Yesu ni lazima upige hesabu kwanza kujua gharama. Maana kuna gharama katika kumfuata Yesu. Ukisoma katika aya za bibilia hapo juu, utaona Yesu anatoa mifano miwili ya watu waliokuwa wanataka kumfuata Yesu, mmoja anayetaka kujenga nyumba , kwamba ni lazima apige kwanza gharama ajue iwapo anazo fedha za kutosha kuanza hadi kuikamilisha nyumba yake, ili asije akaishia njiani akachekwa na watu. Na wa pili ni yule mfalme aliyetaka kwenda vitani kupigana na ufalme mwingine, kwamba ni lazima apige hesabu iwapo watu alio nao wanatosha kwenda kushindana na watu elfu ishirini wa vita wa adui yake.
    Bwana Yesu hamaanishi kwamba tuwachukie kweli ndugu zetu wa karibu, bali kukataa mashauri yao mabaya yanayotuelekeza kutengana na Mungu wako.
    Yaani tuwapende na kuwaheshimu katika mambo yote. Tuwatii; isipokuwa tusiwafuate katika kutenda mabaya tusikubali. kumpenda Mungu sawa sawa ni lazima upige hesabu kati ya Kristo na malimwengu, ni yupi upate kumfuata. Chagua kumfuata Yesu Kristo na kumpenda yeye peke yake. Hakikisha kuwa kila mtu anaye kuzunguka anajua ya kuwa wewe unampenda Mungu kuliko kitu kingine chochote. Katekisim ya kanisa katoliki inatufundisha kuwa ;mungu alituumba ili tumjue, tumpende na mwisho tufike kwake Mbinguni.
    Unapoa amua kumpenda Yesu kwelikweli; watu watakuchukia, familia na marafiki watakucheka, wengine watakukatisha tamaa, lakini usijali, wewe songa mbele na Kristo. Ukishakuwa umepata elimu hii ya kumjua Mungu, wewe endelea tu kumpenda, waache wanadamu waseme watakavyo, maana Binadamu hana jema, wala baya ni lazima tu watazungumza, wewe kaza tu kumpenda Mungu wako.
    Mungu mara zote hawezi kutembea na mtu au kumbariki, kumtendea mambo makubwa ya Baraka maishani mwake, isipokuwa amempenda mtu huyo. Hapa tunaona kuwa kigezo ni upendo. Ukimpenda Mungu atakulinda na mabaya yasikupate; wachawi, nguvu za giza hawatakuweza, wala kukushambulia. Mungu anakuficha adui zako wasikuone.
    Amosi 3:3
    Je? Watu wawili wataweza kutembea pamoja wasipokuwa wamepatana?
    Yohane 21:15-19
    Yesu anamwuliza Simoni Petro kama anampenda? Mungu hampatii simon Petro nafasi ya kumtumikia paka amemhakikisha kuwa anampenda. Mungu anataka kukubariki, kukuponya, lakini je unampenda? Katika bibilia kuna mifano ya watu wengi ambao walionesha kumpenda Mungu kwa dhati. Ibrahimu baba wa Imani, Danieli na wenzake.
    Ibrahimu kwa namna alivyompenda Mungu, hakuruhusu mahusiano yake na mke wake, na watoto wake yazuie mahusiano yake na Mungu. Alificha siri juu ya ujumbe wa kumtoa Isaka kuwa sadaka ya kuteketezwa katika mlima wa Moria.
    Mtu mwenye upendo kwa Mungu, hawezi kuzuiliwa na kitu chochote. Mungu anataka umtolee kitu kilicho cha thamani kwake.
    Wako watu wengine kama Daniel, kwa vile walivyompenda Mungu, hawakuogopa Mfalme, Moto wala Simba. Ayubu alijaribiwa, lakini hakuweza kumwacha Mungu.

КОМЕНТАРІ •