Dk Biteko awataka wafanyabiashara wa kemikali za kuchenjua madini kuuza kwa kufuata bei elekezi

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 10 вер 2024
  • Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amesema kuwa, Serikali imeanza kuchukua hatua kwa wafanyabiashara wa kemikali ya kuchenjua madini ya dhahabu ( Sodium Cyanide) ambao hawatendi haki kwa wachimbaji wadogo.
    Hayo yamebainishwa Januari 7, 2023 katika kikao cha pili cha wadau wanaojihusisha na uingizaji na usambazaji wa Sodium Cyanide nchini inayotumika katika shughuli za kuchenjua madini ya dhahabu iliyofanyika katika ukumbi wa TMDA Buzuruga Jijini Mwanza
    Amesema, amepokea malalamiko mengi kutoka kwa wachimbaji wadogo kuwa kemikali ya kuchenjua madini ya dhahabu aina ya “Sodium Cyanide” inauzwa bei ya juu kwa shilingi laki nane (800,000) kwa dumu moja tofauti na bei iliyoelekezwa na Serikali ambayo ni shilingi laki sita (600,000) kwa dumu.
    Amesema, Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan haiko tayari kuona wachimbaji wadogo wanakwamishwa kwa hali yoyote hivyo amemuelekeza Mkemia Mkuu wa Serikali kuwafuatilia na kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote wanaouza kemikali hizo kinyume na bei elekezi.

КОМЕНТАРІ • 1

  • @chakubanga1
    @chakubanga1 Рік тому

    Yoyote yule ambae anataka kununua chemicals, kwanza lazima awe na cheti cha kemikia kutoka University inayodeal na mafunzo hayo.
    Amasivyo, tutakuja kuona vijiji vimekutwa na maiti.. Carbon monoxide poisoning