Dam dam -Rukia Ramadhani
Вставка
- Опубліковано 18 вер 2024
- #viral
#taarab
#oldisgold
#swahili
#swahilimusic
#swahilitotheworld
#zanzibar
DAM DAM -RUKIA RAMADHAN
Huyo mnaenambia , Ni wangu kweli jamani
Wala sitojichimbia, Wazi takuonesheni
Nae kwangu kaamua, Sasa tujifiche nini
Kwa wale wanoumia, Naomba vumilieni
Anipenda nambenda, kwa dhati sio utani
Sitokhalifu kutenda, Akitakacho mwandani
Mimi pete yeye chanda, Sibanduki kidoleni
Wabaya mtasarenda, Kabisa hatuachani
Pendo letu ni bayana, Si siri iliyondani
Na nyie mnotuona, Msisite chungueni
Hatujalli mnaonena, Tangazeni hadharani
Kama kosa kupendana, Twendeni mahakamani
Kweli wangu muadhamu, Nakiri nnae ndani
Mimi nae dam dam, Tumeshibana nyoyoni
Mengi anayonikimu, Ya raha na burudani
Kuachana ni vigumu, Katu hatufarakani
Mimi nae dam dam, Wenyewe tunapendana
Kwa heshima na nidhamu, mahaba tunapeana
Yeye anipenda sana, Mapenzi yamenibana
Mimi bibi yeye , bwana
Mimi nae dam dam, Wenyewe tunapendana
Mahaba yetu matamu , Kwa usiku na mchana
Kutwa mimi nna hamu , kwa mpenzi muungwana
Mimi nae dam dam, Wenyewe tunapendana
Mapenzi yetu adimu, Kutwa twabembelezana
Wanotaka kuhujumu, Nafasi hiyo hatuna
Mimi nae dam dam, Wenyewe tunapendana
Hadhi yake muadhamu, Sijui wapi kasoma
Naomba penzi lidumu, waumie wanoumwa
Mimi nae dam dam, Wenyewe tunapendana
Mimi nae dam dam, Wenyewe tunapendana
Kwa heshima na nidhamu, mahaba tunapeana
#ZANZIBAR #TAARAB #yalaiti #sabah salum #ASILIA #ZAKALE DHAHABU #ASILI YA LADHA ZA PWANI
NApenda sana nyimbo zako mama
Nice ❤
Mama uko vizur
Asante😊
asante
Twashkr
ua-cam.com/video/5vnAq2DhvMI/v-deo.htmlsi=3yspXFUh63IvNx_L