Kamati yaijia juu Wizara ya Maliasili na Utalii kisa ongezeko la fedha za matumizi

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 12 вер 2024
  • Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeeleza kuwa haridhishwi na matumizi ya nyongeza ya fedha ya Sh19 bilioni zilizopelekwa Wizara ya Maliasili na Utalii, hivyo itapeleka mabadiliko ya matumizi ya fedha hizo.
    Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mwenyekiti, Timotheo Mnzava leo Mei 30, 2024 amesema kamati ilipokea taarifa kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii imeongezewa bajeti kwa kiasi cha Sh19 bilioni ili kupunguza baadhi ya changamoto zinazosababishwa na ufinyu wa bajeti.
    Amesema katika fedha hizo, kamati ilijulishwa kuwa wizara imepanga kutumia Sh14 sawa na asilimia 74 ya nyongeza katika matumizi mengineyo na Sh5 bilioni sawa na asilima 26 kwa ajili ya matumizi ya Maendeleo
    Amesema kamati haikuridhishwa na mgawanyo wa nyongeza hiyo kutokana na sababu mbalimbali.

КОМЕНТАРІ • 2