MAPYA AJALI YA NDEGE ILIYOUA 179 KOREA KUSINI, SERIKALI YATANGAZA…

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 7 лют 2025
  • Summary: Ajali ya ndege ya Shirika la Jeju la nchini Korea Kusini ilitokea Desemba 29, 2024, na kusababisha vifo vya watu 179 huku wawili wakinusurika kifo.
    Seoul. Serikali nchini Korea Kusini imetangaza mpango wa kujenga mfumo wa Kamera zitakazowezesha kufuatilia mwenendo wa ndegepori wanaopita ama kukatiza karibu na maeneo ya viwanja ili kukabiliana na tishio la kuingia kwenye injini za ndege hizo.
    Mpango huo umetangazwa jana Alhamisi Februari 6,2025, na Serikali nchini humo zikiwa zimepita wiki tano tangu kutokea kutokea ajali ya ndege ya Shirika la Jeju la nchini humo, iliyoondoa uhai wa abiria na wahudumu 179, huku wawili wakinusurika.
    Mpango huo umetangazwa na Wizara ya Miundombinu na Usafirishaji wa Korea Kusini, kupitia taarifa yake kwa Umma, ambayo imesema unalenga kukomesha ajali za ndege zinazosababishwa zinazochangiwa na muingiliano wa ndegepori.
    Pia umechangiwa na ripoti ya awali uchunguzi wa ajali ya ndege hiyo iliyobaini kuwepo kwa mabaki ya damu yenye vinasaba vya ndegepori na manyoya ya ndege aina ya Kwelea wa Bluu katika injini ya ndege ya abiria iliyopata ajali.
    Ndege ya Shirika la Jeju aina ya Boeing 837-800 ilikuwa ikitokea Jijini Bangkok Thailand kwenda Muan nchini Korea Kusini ikiwa na abiria na wahudumu 181, ambapo kati yao 179 walifariki dunia katika ajali hiyo huku wawili pekee wakinusurika kifo.
    Ajali hiyo ilitokea Desemba 29, 2024, wakati abiria hao wengi wao raia wa Korea Kusini na Thailand walipokuwa wakitoka kusherehekea Sikukuu ya Krismasi jijini Bangkok. Ilipopata hitilafu hiyo ilitua kwa kutumia sehemu ya uvungu (tumbo) badala ya tairi kisha kuserereka na kwenda kugonga nguzo kisha kulipuka.
    “Viwanja vyote vya ndege kuanzia sasa vitafungwa Kamera maalum za kufuatilia mwenendo wa ndegepori na kutoa taarifa mapema kwenye Kituo cha Kuongozea ndege ya abiria ili kutoa mwanga kwa marubani kuchukua hatua stahiki na kuepusha madhara kwa abiria,” ilisema taarifa hiyo.
    Vifaa maalum vinavyohamishika kwa ajili ya kufukuza ndegepori pia vitafungwa kwenye viwanja vyote kufikia mwakani (2026) ili kuruhusu kushughulika na ndegepori wakubwa na wa kati.

КОМЕНТАРІ •