QASWIDA ya HARUSI YA NDUGU WAWILI ABUBBAKR NAE MUHIDDINI WATOTO WA SHARIFF HUSSEIN BADAWY

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 6 жов 2024
  • Leo Tunafurahiya
    Family ya sharifu Hussein
    Wawili wanofunga ndoa
    Abubbakar nae Muhiddini
    Namshukuru Rabana ∆∆∆ Kwa hini njema nafasi.
    Badawii wameona ∆∆∆ Wangie kwa idarusi.
    Pongezi mama Madina ∆∆∆ Mama wa hini harusi.
    Moyo wangu ubaridi ∆∆∆ Hili nalifurahiya.
    Na Leo ni kama idi ∆∆∆ Kwa Wana wa badawiya.
    Mama Fatuma Saidi ∆∆∆ Na wewe sherehekeya.
    Imenawiri baiti ∆∆∆ Kwa uturi yanukiya.
    Hini ni yetu bahati ∆∆∆ Mola 'metujaaliya
    Wana wa tuma masiti ∆∆∆ Nawapongeza Jamiya.
    Harusi jambo la suna ∆∆∆ Ameshanena Hashimu.
    Na Sisi budi hatuna ∆∆∆ Ila ni kuwakirimu.
    Karibu wifi Muzna ∆∆∆ Pamoja nawe Nasimu.
    Nyumba mumeinawiri ∆∆∆ Shahidi Mola Karima.
    Nyoyo zetu zimekiri ∆∆∆ Nyinyi ni viumbe vyema.
    Amefurahi Qamari ∆∆∆ Shekha na mwana halima.
    Natamka kwa ulimi ∆∆∆ Nyote nikiwaambiya.
    Amefurahi mtumi ∆∆∆ Na swalehe alawiya.
    Pongezi Nuru na ummi ∆∆∆ Amina nawe swafiya.
    Kwa baraka za Hashimu ∆∆∆ Jambo limeshatengeya.
    Ndio tumeiadhimu ∆∆∆ Harusi kuishashiya.
    Hongera kwa mariamu ∆∆∆ Rukia nawe Bahiya.
    Sote tumefurahiya ∆∆∆ Kwa kufika siku hini.
    Wazee Wana pamoya ∆∆∆ Na wote walo nyumbani.
    Na hata dada samiya ∆∆∆ Nae yupo harusini.
    Ilahi awadumishe ∆∆∆ Hawa wetu maarusi.
    Nyoyo azinawirishe ∆∆∆ Na jamii ya nufusi.
    Kizazi akipitishe ∆∆∆ Ilahi Mola mkwasi.
    Mwisho naomba zaidi ∆∆∆ Kwa Mola wangu Jaliya.
    Kwa Nuru yake Saidi ∆∆∆ Na Huseni badawiya.
    Atuhifadhi Wadudi ∆∆∆ Sisi Wana familia.

КОМЕНТАРІ • 4