MNADA WA ZAO LA MBAAZI MAMBO MOTO/ BEI YA JUU 1,920 NA BEI YA CHINI 1,870 / RUNALI NA TMX

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 15 вер 2024
  • Wakulima wa Chama Kikuu cha Ushirika kinachohudumu wilaya ya Ruangwa, Nachingwea na Liwale - RUNALI wamefanya mnada wa kwanza wa zao la Mbaazi katika Kijiji cha Mkonjera chini ya chama cha Amcos cha Ndangalimbo kilichopo Kata ya Mnero Miembeni wilaya ya Nachingwea.
    Mnada huo umefanyika leo, 18 Augusti 2024 kwa Mfumo wa Mauzo na Manunuzi Mtandaoni maarufu Tanzania Mercantile Exchange (TMX) ambapo bei ya juu ni Tanzania Shilingi 1,920 na bei ya chini 1,870 katika kila kilogramu moja ya Mbaazi, pia jumla ya tani 6,255 zilizouzwa.
    Aidha Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea aliyekaimiwa na Afisa Tarafa wa Kata ya Nambambo Ndg, Christopher Mkuchika ameongea na wakulima wawe na utu katika kulinda mali na mazao yao ili pasiwepo na suala la wizi kwa mazao yao.
    Pia wakulima wamepongeza jitihada zinazofanywa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya awamu ya sita kwa kuwajali wakulima na kuwatafutia soko lenye tija la mazao yao ya kilimo, pia wamewaomba wanunuzi walipe kwa wakati malipo yao ili wafanye shughuli za kimaendeleo kupitia fedha zitokanazo na mauzo ya mazao.
    Kwa taarifa zaidi endelea kutufuatilia katika kurasa zetu ‪@_don_media‬
    #donmediatv #like #comment #share #newupdate #donmedia #nahapanikwetu

КОМЕНТАРІ • 6