NATAKA NISIMAME By MOSES TSUMA and The Ibada Band

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 23 гру 2020
  • #mosestsuma #pananeema #ibadaband
    This song sends us back to repentance, uprightness and to purity in Christ. It cautions us to make sure we stand holy before the Lord in the day of judgment.
    This video features the Ibada band, it was done at Likoni in Mombasa.
    NATAKA NISIMAME LYRICS
    Nataka nisimame safi eeehh eh eh eeh.
    Nataka nisimame safi mbele zako..ooh X2
    Najua nyote mnafahamu ipo siku inakuja, tutakapotoa hesabu ya talanta na huduma tulizo pewa.
    Kama ile historia ya wale walio pewa talanta, yasemekana aliporudi mwenyewe aliuliza mlizifanyia nini.
    Lakini jambo moja niwakumbushe wapendwa, lakini neno moja niwakumbushe rafiki.
    Mioyo hii mioyo mioyo yetu mioyo oo, mioyo itachunguzwa, mioyo itakaguliwa.
    Haijalishi umefanya huduma namna gani duniani, haijalishi umetenda kazi za namna gani kanisani.
    Kama moyo wako si safi, Ni bure huduma
    Kama nafsi yako inahukumu, Ni bure huduma
    Kama huna msamaha wa dhambi, Ni bure huduma
    Kama utakufa ndani ya dhambi, Ni bure huduma.
    Ooo, ili niombi langu baba unisikie.
    Nataka nisimame safi eeehh eh eh eeh.
    Nataka nisimame safi mbele zako..ooh X2
    Isije ikawa siku hiyo ninapo simama mbele ya kiti cha hukumu, ijapofika ni zamu yangu kueleza yote niliyo fanya ulimwenguni X2.
    Niseme niliimba sana, nikauza kanda,
    redio televisheni, nikasifika sana X2.
    Zaidi ya yote, naombaa..aa
    Nataka nisimame safi eeehh eh eh eeh.
    Nataka nisimame safi mbele zako X2.
    Itakapofika nizamu yako ndugu…ei eeh, siku hiyo ukisimama mbele zake Bwanaaa.
    Akuulize ulichofanya duniani dadaaa, utakapotoa hesabu yako baba weweee.
    Itakapofika nizamu yako dada…ei ee, siku hiyo ukisimama mbele zake Bwanaaa.
    Akuulize ulichofanya duniani mamaaaa, utakapotoa hesabu yako dada weweee.
    Useme nilifunza neno, nikahubiri sanaaa
    Useme nilitoa pepooo, watu wa kakombolewa.
    Useme nilitoa pesaaa, nikanjenga kanisaaa.
    Sadaka fungu la kumi, na mfuko wa mchungajii..iii.
    Naomba, hili ni ombi langu kwako,
    (Bwana Yesu asisimame aseme sikujui, Bwana Yesu asisimame aseme ondokaa )X2
    Hili ni ombi langu kwakooo…oooh.
    Naomba usimame safi eeehh eh eh eeh,
    Naomba usimame safi mbele zakee..eeh.
    Sote tusimame safi eeehh eh eh eeh,
    Sote tusimame safi mbele zakee..eeh.
    Tusimame mbele zake Bwana, tunapokwenda mbele zake tumpendeze yeye..aah
    (Lyrics by Stephen Ndine)

КОМЕНТАРІ • 30