MAMA ALIYEUAWA KWA KUNYONGWA NA MWANAYE KISA MALI MAJIRANI WAFUNGUKA' MTOTO ALIKUA KAMA KICHAA'

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 26 вер 2024
  • Ndugu na majirani wamesimulia namna walivyoguswa na kifo cha Adela Mushi (74), ayedaiwa kuuawa kwa kunyongwa na kisha kukatwa na shoka sehemu ya usoni na mwanaye, analiyekuwa akidai mali zilizoachwa na marehemu baba yake.
    Mwili wa mama huyo ulikutwa ukiwa umekufa Septemba 23, 2024 usiku wa saa 4, huku kulazwa kifudifudi maeneo ya Uru Okaseni, huku shingoni kukiwa kumefungwa kipande cha kanga.
    Wengi wameleza kuwa Adela alikuwa mtu mwenye upendo na msaada kwa jamii.
    "Alikuwa mama wa jumuiya mwenye huruma na mcheshi na aliyejitolea kusaidia kila mtu," alisema mmoja wa majirani. "Kifo chake kimetuacha na huzuni kubwa na maswali mengi," aliongeza.
    Mwili wa Adela umezikwa leo Ijumaa, Septemba 27, 2024, kijijini kwake Okaseni, kata ya Uru Kusini, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro kwenye makaburi ya familia.
    Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akieleza kuwa jeshi hilo linamshikilia mwanaume huyo kwa mahojiano zaid

КОМЕНТАРІ • 1

  • @Lily-rn6xc
    @Lily-rn6xc 4 години тому +1

    Tunaishi huku tunaishia ee Mungu tusaidie 😢