Hali ilivyo baada ya ziwa Tanganyika kufungwa, wafanyabiashara wahaha

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 10 вер 2024
  • Kigoma. Siku chache mara baada ya kufungwa kwa ziwa Tanganyika wananchi na wafanyabishara wa mazao ya samaki katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, wamelalamikia ugumu wa maisha hali inayosababisha kuwepo kwa hofu ya kuibuka kwa matukio ya uhalifu.
    Serikali za nchi nne zinazozunguka ziwa Tanganyika zilifikia hatua ya kusitisha shughuli za uvuvi kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Mei 15, 2024 hadi Agasti 15 kutoa nafasi kwa ukuaji wa mazao ya samaki kutokana na tafiti kuonesha kuwa idadi ya samaki imepungua.
    Mfanyabiashara wa samaki katika soko la Buzebazeba, Zainabu Malilo amesema kutokuwepo kwa mazao ya samaki katika ziwa Tanganyika imemfanya aanze biashara ya kusafirisha samaki wanaopatikana katika mito na mabwawa yaliyopo mkoani Tabora.
    Malilo amesema samaki hao wanapanga wanne kwa Sh4,000 ambapo awali kabla ziwa halijafungwa walikuwa wanawauza Sh2,000 ambapo walikuwa wanapanga watano hadi sita na hakuna mteja anakuja kuuliza hata bei biashara ya samaki.

КОМЕНТАРІ • 21

  • @NDEWARA
    @NDEWARA 3 місяці тому

    Hongera sana sana serekali. Hatua ya kulifunga ziwa ni ya muhimu sana kwa uvuvi endelevu. Muhimu sasa kuwekeza kwenye mabwawa ya kufugia samaki

  • @exaverysimon1064
    @exaverysimon1064 3 місяці тому +1

    MSITEGEMEE KAZ MOJA ANGALIEN FURSA NYINGINE HUO MJI N MKUBWA JE AMBAO HAWANA ZIWA WANAISHIJE

  • @majidalharthi4774
    @majidalharthi4774 3 місяці тому

    Mkoa wa kigoma ktk mwambao Tanganyika miezi mitatu ni mingi sanaa kuwafungia watu mimi na shauri mwezi wa saba mwishoni ziwa lifunguliwe maana mwezi wa nane dagaa inanza kupatikana kwa wingi ziwa Tanganyika ndio msimu wake huanzia hapo mimi nilikuwa nafanya kazi katika ziwa hili najua msimu wa kupata na kukosa kwahiyo na shauri hivyo

  • @Hakuzwe
    @Hakuzwe 3 місяці тому

    Tafuta kazi zingine.Mbone mahali kwengine hawana ziwa..wamekufa

  • @lameckbalekere1962
    @lameckbalekere1962 3 місяці тому

    Kalime mchicha

  • @user-xe8xv6so6s
    @user-xe8xv6so6s 3 місяці тому

    Mkiambiwa mbadilike hamtaki. Na bado

  • @robatimajwajwa7236
    @robatimajwajwa7236 3 місяці тому

    Ndugu zangu watanganyika poleni sana iyo ndooselikali yatanzania

  • @shehanimzee9953
    @shehanimzee9953 3 місяці тому

    Sahihi serikali iliangalie hili

  • @SelijusiMalambo-ur6cr
    @SelijusiMalambo-ur6cr 3 місяці тому

    Wavivu wafunge hata miezi 20

  • @AllySalum-h4j
    @AllySalum-h4j 3 місяці тому +2

    tulieni samaki wazaliane tuje tuanze kula migebuka yene minofu

    • @syliviakente9460
      @syliviakente9460 3 місяці тому

      Uelewa ndugu yangu

    • @AllySalum-h4j
      @AllySalum-h4j 3 місяці тому

      @@syliviakente9460 nakwambia dada zangu wao ni kupinga tu migebuka ilifikia hatua inataka kulingana na dagaa wa kigoma wale wa zani wawe na subra baada ya hiyo miezi3 watafurahia

    • @ahmadmasunda9892
      @ahmadmasunda9892 3 місяці тому

      SAWA FUNGENI TU NA HUKU BAHARINI MUJE KUFUNGA PIA ILI KUPATA UWIANO

  • @FilbertKalembe-fy4oq
    @FilbertKalembe-fy4oq 3 місяці тому

    Kufungwa ziwa nifaida yako siukalime mbona nyie binadamu hamshukuru

  • @HAPPYSULE
    @HAPPYSULE 3 місяці тому

    Hivi serekali kweli hivi ziwa linaishaga samaki kweli badala yakuwapa vifaa vya uvuvi vyakisasa et inafunga, Sasa inafunga ufukwe wa kigoma Zambia wanavua Kongo wanavua Burundi wanavua, au na huko wamefunga?, kwahiyo hata uvuvi wandoano hakuna?

  • @smallscaleminingsupplies9670
    @smallscaleminingsupplies9670 3 місяці тому

    Kilo 1 elfu 68,000 hatari na nusu, nani ananunua hao dagaa

  • @sebastiansalamba313
    @sebastiansalamba313 3 місяці тому

    Tulia wewe samaki waongezeke mnakuwa wajinga tu

  • @robatimajwajwa7236
    @robatimajwajwa7236 3 місяці тому +1

    Ndugu zangu watanganyika poleni sana iyo ndooselikali yatanzania