TUMAINI JIPYA DUNIANI TV
TUMAINI JIPYA DUNIANI TV
  • 384
  • 40 882

Відео

THE MINISTRY OF GIVING - HUDUMA YA UTOAJI (Chakula cha Hisani) By Ev. ARBOGAST KANUTI
Переглядів 542 місяці тому
THE MINISTRY OF GIVING - HUDUMA YA UTOAJI (Chakula cha Hisani) By Ev. ARBOGAST KANUTI
Somo: THAMANI YAKO NI KUBWA
Переглядів 4747 місяців тому
Somo: THAMANI YAKO NI KUBWA
Mwaka 2024 - Mwaka wa kuangaza
Переглядів 488 місяців тому
Mwaka 2024 - Mwaka wa kuangaza
Papa Francis, Atoa Msimamo wa Kanisa Katoliki kuhusu ndoa ya jinsia moja ni marufuku hata Kubariki.
Переглядів 1578 місяців тому
Papa Francis, Atoa Msimamo wa Kanisa Katoliki kuhusu ndoa ya jinsia moja ni marufuku hata Kubariki.
December 18, 2023
Переглядів 78 місяців тому
December 18, 2023
KUSANYIKO KUU
Переглядів 399 місяців тому
KUSANYIKO KUU
@rwizakakiza
Переглядів 3010 місяців тому
@rwizakakiza
Ukweli unapendwa, usikate tamaa (Subscribe, like and share for your favorite friends)
Переглядів 172Рік тому
Ukweli unapendwa, usikate tamaa (Subscribe, like and share for your favorite friends)
KONGAMANO LA ROHO MTAKATIFU, (Share and please SUBSCRIBE)
Переглядів 84Рік тому
KONGAMANO LA ROHO MTAKATIFU, (Share and please SUBSCRIBE)
MTOKO NA YESU
Переглядів 147Рік тому
MTOKO NA YESU
WIKI YA NEEMA
Переглядів 105Рік тому
WIKI YA NEEMA
WIKI YA NEEMA @Rwizakakiza
Переглядів 103Рік тому
WIKI YA NEEMA @Rwizakakiza
Emaus Prayer Group, tupo tayari kuipeleka Injili mahali popote, karibu tuungane pamoja.
Переглядів 75Рік тому
Emaus Prayer Group, tupo tayari kuipeleka Injili mahali popote, karibu tuungane pamoja.
Chanzo cha mwanadamu, mpaka WOKOVU wake
Переглядів 39Рік тому
Chanzo cha mwanadamu, mpaka WOKOVU wake
MUNGU NI MWEZA YOTE
Переглядів 37Рік тому
MUNGU NI MWEZA YOTE
JE UNAOGOPA NINI?
Переглядів 25Рік тому
JE UNAOGOPA NINI?
Mwaka wa kuongeza - Arbogast Kanuti
Переглядів 372 роки тому
Mwaka wa kuongeza - Arbogast Kanuti
Zabron Singers - Nakutuma Wimbo
Переглядів 1304 роки тому
Zabron Singers - Nakutuma Wimbo
USILAHUMU, CHUNGUZA KWANZA
Переглядів 354 роки тому
USILAHUMU, CHUNGUZA KWANZA
CREATE YOUR FUTURE
Переглядів 294 роки тому
CREATE YOUR FUTURE
Uje ROHO MTAKATIFU
Переглядів 3444 роки тому
Uje ROHO MTAKATIFU
Tafuta Ufalme wa MUNGU
Переглядів 3184 роки тому
Tafuta Ufalme wa MUNGU
NDOA YANGU 03.08.2019, ILINOGESHWA SANA NA JUMUIYA YA SALA YA EPG
Переглядів 1504 роки тому
NDOA YANGU 03.08.2019, ILINOGESHWA SANA NA JUMUIYA YA SALA YA EPG
Hofu inauwa kuliko corona
Переглядів 344 роки тому
Hofu inauwa kuliko corona
JUDGE
Переглядів 94 роки тому
JUDGE
HURUMA YA YESU KRISTO
Переглядів 254 роки тому
HURUMA YA YESU KRISTO
KWARESMA 2020
Переглядів 474 роки тому
KWARESMA 2020
SHANGWE TANZANIA
Переглядів 164 роки тому
SHANGWE TANZANIA
Mchungaji, Daniel Mgogo azungumzia Tamasha kubwa la SHANGWE TANZANIA
Переглядів 374 роки тому
Mchungaji, Daniel Mgogo azungumzia Tamasha kubwa la SHANGWE TANZANIA

КОМЕНТАРІ

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza 5 днів тому

    Somo: MAJIRA NA NYAKATI ZIMEBEBA MAISHA YAKO °°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°° Fuatilia UA-cam. Https://youtube.com/@Rwizakakiza Sehemu 18: ‭""Kwa KILA JAMBO kuna MAJIRA yake, Na WAKATI kwa KILA KUSUDI chini ya mbingu"" .....Mhubiri 3:1..... 7. 2. NAMNA BORA YA KUTAMBUA MAJIRA NA NYAKATI MAISHA YAKO. Ukweli mwanadamu yeyote hawezi kujua yajayo asipowezeshwa kujua majira na nyakati na MUNGU anachokiwaza katika majira na nyakati za mwanadamu. Ukweli ni kwamba ili kujua MUNGU anachomwazia mwanadamu, ni MUNGU pekee ajuaye na Roho yake ikaayo ndani yake yaani ROHO MTAKATIFU. .....Maana ni nani katika binadamu AYAJUAYE mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na MAMBO ya MUNGU HAKUNA AYAFAHAMUYE ila ROHO wa MUNGU. .....1Korintho 2:11.... Kwa hiyo ili uweze kutambua kilichopo ndani ya majira na nyakati na MUNGU anachokiwaza kwa ajili yako na kusudi lake lazima UJENGE MAHUSIANO BINAFSI NA ROHO MTAKATIFU. Kujenga uhusiano na ROHO MTAKATIFU ni kujenga URAFIKI wa karibu na ROHO MTAKATIFU na kujiachia mikononi mwake, ukimwamini, ukimtegemea na maisha yako kufa na kuanza kuishi kwa ajili ya YESU KRISTO tu yaani kutokuwa na amri na maisha yako ila MUNGU awe na amri na maisha yako. Kwa njia hiyo ROHO MTAKATIFU ni rahisi kuzungumza na kukuelekeza kufikia hatima yako njema na yenye kutimiliza kusudi la MUNGU na ni rahisi kutembea na MUNGU Popote kama Yusufu .....Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake? ....Mwanzo 41:38..... ZINGATIO: Katika hitimisho hili lazima ujue kwamba.....Huwezi kutambua majira na nyakati, Bila ROHO MTAKATIFU.....Kumbuka ROHO MTAKATIFU ndiye anayejua KILICHOMO NDANI YA MOYO WA MUNGU. Na jambo la pili lazima utambue ROHO MTAKATIFU ndiye mwenye kufunua mafumbo ya MUNGU na kufunua kilichomo kwenye majira na Nyakati zilizopita, zilizopo na kufunua yajayo. ....."ROHO MTAKATIFU atakapokuja, huyo ROHO wa KWELI, ATAWAONGOZA awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote ATAKAYOYASIKIA atayanena, na MAMBO YAJAYO ATAWAPASHA HABARI yake".... .....Yohana 16:13..... MUNGU AKUBARIKI SANA ........... Mwisho............. Mada ijayo:- TABIA 15 HATARISHI NA ZIEPUKE KWENYE MAISHA YAKO. ....Tutaendelea.... Rejea "When He, the SPIRIT of Truth, comes, He will guide you into all the truth [full and complete truth]. For He will not speak on His own initiative, but He will speak whatever He hears [from the FATHER-the message regarding the Son], and He will disclose to you what is to come [in the future]" .....John 16:13...... Ev. Erasmus Pascrates Kakiza +255 782 546 914 @2024 The year of my shining.❤

  • @felixmushi3354
    @felixmushi3354 5 днів тому

    SIFA NA UTUKUFU NI KWA MUNGU 🕯️💦

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza 6 днів тому

    MUNGU awabariki sana wapenzi Wafuatiliaji na Watazamaji wa TUMAINI JIPYA DUNIANI TV, kote ulimwengu. Tunaomba radhi kukosa Ubora wa sauti siku ya leo.

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza 6 днів тому

    Somo: MAJIRA NA NYAKATI ZIMEBEBA MAISHA YAKO °°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°° Fuatilia UA-cam. Https://youtube.com/@Rwizakakiza Sehemu 17: ‭""Kwa KILA JAMBO kuna MAJIRA yake, Na WAKATI kwa KILA KUSUDI chini ya mbingu"" .....Mhubiri 3:1..... 7. HITIMISHO. Hapa tutaangalia mambo mawili yaani:- (Faida na namna bora ya kutambua majira na nyakati kwenye maisha yako yote) 7. 1. FAIDA /UMUHIMU WA MAJIRA NA NYAKATI. Zipo faida nyingi, lakini sehemu hii tunaangalia faida kuu ya majira na nyakati kwenye maisha yako ambayo ni KIBALI KWA MUNGU NA KWA WATU. ......Kibali ni upendeleo, kibali ni kupewa nafasi, kibali ni kukubalika kwa MUNGU na kwa watu. Kabla ya kupata kibali ipo NEEMA ya MUNGU kwanza inayokubeba, alafu ukifanya vizuri kupitia neema hiyo unapata kibali. Wote mnaweza kuwa na huduma moja, lakini KINACHOWATOFAUTISHA ni BIDII /JUHUDI BINAFSI, unavyojibidiisha na kujitoa kwa ajili ya Neema MUNGU aliyokupa (Yaani huduma), Jitihada zako ndizo zinazojenga nafasi ndani ya moyo wa MUNGU au ndani ya mioyo ya watu, na Nafasi hiyo ndiyo kibali. Mfano. Kaini na Habili wote wawili, MUNGU aliwapa neema ya kumjua MUNGU na huduma yao kuu ilikuwa ni UTOAJI. Kilichotokea ni Habili kujiongeza /kujibidiisha /kufanya cha ziada. Ndio maana MUNGU alipomtokea Kaini alimuuliza ukijibidiisha /ukitenda mema hautapata kibali?. Lakini Kaini akaona Wivu na wivu ukajenga Chuki na Chuki ikazaa mauaji kwa nduguye. ......Je Kaini UKITENDA VYEMA, hutapata KIBALI? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. .....Mwanzo 4:7.... Wote mmebarikiwa kupata kazi, Je unatambua kwanini umebarikiwa? Je MUNGU aliyekubariki unatambua ndiye mwenye vyote?, hata ukimpa vyote ni vyake ila juhudi za KUMPENDA katika kile ninachokitoa ndizo zitanipatia kibali. Usimwonee mwingine wivu, bali Ongeza bidii katika kutenda. Majira na nyakati zinakupatiaje kibali, Kumbuka majira na nyakati ni kutambua cha kutenda ndani ya muda sahihi kulingana na kusudi lililoko kwenye muda huo. Usipofanya kwa majira na nyakati sahihi utapata hasara. Mfano Ni wakati wa kuvuna, Wewe ndio unapanda, Wakati wa kufunga Wewe ni chakula muda wote, Mahitaji ya lazima kwenye familia unakimbilia kununua nguo, Wakati wa mshahara, Unafanya anasa na Matumizi yasiyo lazima, badala ya KUWEKEZA kwa ajili ya uzeeni, usiwasumbue watoto wako. ......Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji; mnajivika nguo lakini hapana aonaye moto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka-toboka. ......Hagai 1:6..... Ukitambua uko kwenye majira na nyakati gani na unapaswa ufanye nini UTAPATA KIBALI KWA MUNGU, NA KWA WATU (Tena kwa watu wakuu yaani wenye vyeo, na wadhifa kubwa). Mfano. YUSUFU Yusufu alikuwa na ndoto na ili ikamilike ndoto yake, alitambua majira na nyakati cha kufanya, hakubaki na MALALAMIKO kwamba Kwanini ndugu zangu waliniuza kwa Wamisril?. Kwanini MUNGU ameniacha mpaka nikasingiziwa na mke wa Potifa kwamba nimebaka?. Siri ya Yusufu ni HAKULALAMIKA bali ALINYENYEKEA na unyenyekevu wake MUNGU akampenda akawa pamoja na Yusufu, hata kwenye Gereza, MUNGU akampa kibali. .....‭BWANA akawa pamoja na Yusufu, akamfadhili, akampa kibali machoni pa mkuu wa gereza. ......Mwanzo 39:21.... Pamoja na kibali, Yusufu analenga kutimiza ndoto yake ambayo imempitisha kwenye majira hayo. Hivyo aliangalia ANAPOELEKEA hakuangalia ANAPOPITIA. Kupitia ROHO MTAKATIFU, Yusufu anajulishwa majira na nyakati zinazokuja juu ya nchi yote ya Misri kwa kutafsiri ndoto ya Farao ambayo hata wakuu wake hawakuelewa na hatimaye bidii ya kuangalia anapoelekea inamsaidia kumpa kibali kwa wakuu mpaka anapewa Uwaziri mkuu. ......Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye ROHO ya MUNGU ndani yake? Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe. Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu, na kwa neno lako watu wangu watatawaliwa. Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe. Farao akamwambia Yusufu, Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri. Mimi ni Farao, na bila amri yako (Yusufu), Mtu asiinue mkono wala mguu katika nchi yote ya Misri. ......Mwanzo 41:38 - 44..... Ukielewa vizuri Habari ya majira na nyakati, utafika mahali ambapo hukutarajia. Watu wengi wanatamani kujua maisha yao ya kesho itakuwaje, Biashara /kazi zao zitakuwaje, Ndoa /familia zao zifanye nini nk. Majibu yote yapo kwenye majira na nyakati, ukitambua utapata kibali na kibali hicho kitakufikisha kwenye ndoto zako, Amina. 7. 2. NAMNA BORA YA KUTAMBUA MAJIRA NA NYAKATI MAISHA YAKO. ....Tutaendelea.... Rejea So Pharaoh said to his servants, “Can we find a man like this [a man equal to Joseph], in whom is the DIVINE SPIRIT [of GOD]?” ......Genesis 41:38..... Ev. Erasmus Pascrates Kakiza +255 782 546 914 @2024 The year of my shining.❤

  • @felixmushi3354
    @felixmushi3354 7 днів тому

    SIFA NA UTUKUFU NI KWA MUNGU 💦

  • @felixmushi3354
    @felixmushi3354 7 днів тому

    SIFA NA UTUKUFU NI KWA MUNGU 💦

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza 8 днів тому

    ❤MUNGU awabariki sana kutoka duniani kote Watu wa mkoa wa Mtwara, Dar es Salaam ni mikoa ambayo imekuwa na Wafuasi wengi yaani Wasikilizaji hasa (live streaming) ❤❤❤

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza 8 днів тому

    Somo: MAJIRA NA NYAKATI ZIMEBEBA MAISHA YAKO °°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°° Fuatilia UA-cam. Https://youtube.com/@Rwizakakiza Sehemu 16: ‭""Kwa KILA JAMBO kuna MAJIRA yake, Na WAKATI kwa KILA KUSUDI chini ya mbingu"" .....Mhubiri 3:1..... 6. AINA 2 ZA MAJIRA NA NYAKATI KATIKA MAISHA YAKO. 6. 2. MAJIRA NA NYAKATI ZA MUNGU Haya ni majira na nyakati ambazo mwamuzi wa mwisho ni MUNGU ingawa hata kama mwanadamu atashirikishwa na MUNGU bado maamuzi ya mwisho ni ya MUNGU mwenyewe. Mwamuzi wa mwisho kwenye majira na nyakati ni MUNGU pekee. Hata kama giza au watu au mamlaka au adui amekuamria Mabaya yaje juu yako, LAKINI YUPO MUNGU MWAMUZI WA MWISHO ANASEMA.... (i). HAUTAKUFA BALI UTAISHI. MUNGU hataki mtu yeyote afe kabla ya majira na nyakati zake, maana akifa kabla ya wakati wake, kuna makusudi ya MUNGU hayatimiza, hutakuwa na kusimulia, Tambua majira na nyakati za MUNGU kwenye maisha yako. Yupo Roho Mtakatifu afunuaye mambo yajayo, ana uwezo wa kukwambia lini utaondoka, ukiwa na uhakika huo hata kama Ikitokea leo mtu anakwambia utakufa, Wewe kwa uhakika utamwambia..... ......Sitakufa bali nitaishi, Nami nitayasimulia matendo ya BWANA. .....Zaburi 118:17..... (ii). HAUTAKUWA TASA BALI UTAZAA WATOTO. Ni kweli wewe ni tasa kwa kila kitu hakuna unachozalisha iwe ni mali au vitu au watoto hata ukizalisha vinakufa. Lakini yapo majira na nyakati za MUNGU ambazo ndio leo, MUNGU anasema hivi... .....Hapatakuwa na mwenye KUHARIBU MIMBA , wala ALIYE TASA, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako NITAITIMIZA. .......Kutoka 23:26...... Ni Ahadi ya MUNGU ujenge nyumba Ukae ndani yake, Na ndani ya nyumba uwe na Uzalishaji na kula matunda ya uzalishaji wako, ambaye hujaoa au kuolewa chukua hatua ya imani. Leo ni wakati wako wa kudai haki yako majira na nyakati za MUNGU kwako zimefika, MUNGU anasema...... ......JENGENI nyumba, MKAKAE ndani yake, KAPANDENI bustani, MKALE MATUNDA yake; OENI wake, MKAZAE wana na binti; KAWAOZENI wake wana wenu, mkawaoze waume binti zenu, WAZAE wana na binti; MKAONGEZEKE huko wala MSIPUNGUE. ......Yeremia 29:5-6..... (iii). HAUTAKUWA MASKINI, BALI TAJIRI. Ni kweli ulizaliwa kwenye umaskini mpaka sasa wewe ni maskini lakini haimaanishi utaendelea kuwa maskini. Ongeza bidii katika kutenda kazi iliyo halali na huku ukikumbuka Neno hili kwamba.... .......Umejua neema ya BWANA wetu YESU KRISTO, jinsi alivyokuwa MASKINI kwa ajili yako, ingawa alikuwa TAJIRI, ili kwamba WEWE UPATE kuwa TAJIRI kwa umaskini wake. .......2 Korintho 8:9....... Unavyoendelea kujibidiisha katika utendaji MUNGU anaachilia NGUVU YA UTAJIRI ndani yako, Sasa ni nyakati na Majira ya kuaga umaskini umefika Ongeza bidii, ila usimsahau BWANA YESU. .......Hapo usiseme moyoni mwako, NGUVU ZANGU na UWEZO wa MKONO wangu ndio ULIONIPATIA UTAJIRI huo. Bali utamkumbuka BWANA, MUNGU wako, maana NDIYE akupaye NGUVU za KUPATA UTAJIRI; ili alifanye imara AGANO lake alilowapa baba zako, kama hivi leo. ......Kum 8:17-18..... (iv). SITAKUACHA KAMWE. Ni kweli umeachwa, unateseka, unanyanyaswa na umetengwa mpaka unaona dunia imekuacha na MUNGU hakukumbuki, Yote hayo yalikuwa ni majira na nyakati tu, kuanzia leo ni wakati wako wa kukumbuka hata na wale waliokusahau na MUNGU Hawezi kukuacha na hatakuacha kamwe nawe usimwache upo kiganjani mwake. .....Wewe umesema, "YEHOVA AMENIACHA, BWANA AMENISAHAU. Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, HAWA WAWEZA KUSAHAU, lakini MIMI SITAKUSAHAU WEWE. Tazama, NIMEKUCHORA katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima. ......Isaya 49:14-16...... (v). NJOO ULIVYO NA DHAMBI ZAKO. Ni ukweli usiopingika kwamba wewe ni mdhambi na watu wote tunajua wewe ni mdhambi na MUNGU anajua wewe ni mdhambi, Lakini leo majira na wakati wa MUNGU umefika, MUNGU anakuita njoo.... .....Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zako zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. Kama UKIKUBALI na KUTII leo utakula mema ya nchi". ......Isaya 1:18-19..... Sisi tumekuona huwezi kusamehewa lakini kumbuka mwamuzi wa mwisho ni MUNGU, leo ni majira na wakati wa MUNGU kwa ajili yako kubadilika ili kuishi na MUNGU upya. (vi). WEWE NI WATHAMANI, NA MWENYE HESHIMA. Ni kweli umekosa heshima, huthaminiwi, hupendwi na hukumbukwi tena. Lakini haimaanishi MUNGU hakuoendi. MUNGU anakupenda sana sana kwa sababu wewe ni wa THAMANI kubwa kwake na mwenye heshima kubwa kwa MUNGU. Ni majira na nyakati za MUNGU kutambulisha heshima na thamani yako kwa ulimwengu maana anakupenda, nawe jipende na ujithamini na kujiheshimu. ......Kwa kuwa wewe ni wa THAMANI machoni pangu, na mwenye KUHESHIMIWA , nami NIMEKUPENDA; kwa sababu hiyo NITATOA watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako. ......Isaya 43:4.... (vii). ULIYECHOKA NA KUKATA TAMAA NJOO. Maisha yamekuchosha, watu wamekuchosha, kazi imekuchosha, Huduma imekuchosha, familia imekuchosha, maneno yamekuchosha, Magonjwa, taabu na mateso vimekuchosha na kadhalika, Ni kweli umechoka na umekata tamaa. Leo Neno moja tu la YESU mtwike hayo yote yalikuchosha na YESU atakupumzisha ili upate raha nafsini mwako. BWANA YESU anasema hivi.... .......Njoni kwangu, ninyi nyote MSUMBUKAO na wenye KULEMEWA na MIZIGO, nami NITAWAPUMZISHA. Jitieni NIRA yangu, MJIFUNZE kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi MTAPATA RAHA NAFSINI mwenu". ...... Mathayo 11:28-29..... (viii). MWENYE AIBU, WEWE NI JASIRI NA HODARI. Kuna mambo ukiyatazama unaona aibu inakujia, Mengine ukiyasema ni aibu, imekuwa ni siri yako mwenyewe lakini yamegeuka kuwa mateso kwa sasa. Mwingine hadhi yako uliyonayo na kufanya kitu cha kawaida unaona ni aibu, Umefirisika unawaza watu watanionaje watanicheka. Wengine ni aibu ya kuachwa, kusimama mbele za watu, nk. Umekuwa mtumwa wa aibu kumbuka YESU aliidharau aibu, akajivika ujasiri na Uhodari akashinda. Ni majira na nyakati za MUNGU kuondolewa aibu yako, kubali na chukua hatua uwe shujaa, aibu itakufedhehesha kwa muda lakini utapata heshima ya kudumu. .......Tukimtazama YESU, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya FURAHA iliyowekwa mbele yake ALIUSTAHIMILI MSALABA na KUIDHARAHU AIBU, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha MUNGU. .....Ebrania 12:2.... (ix). ULIYESHINDWA, INUKA ANZA UPYA. Naongea na wewe uliyekata tamaa kwa sababu UMESHINDWA kufikia malengo yako. Kila ukipanga unashinwa, kila mipango haikamiliki, masomo umeishia katikati, Biashara ni hasara unatamani uachane nayo, Mahusiano unaona hayana mwelekeo, mwenzi wako humwelewi unatamani mwachane. Majira na wakati wa MUNGU umefika inuka tena upya mara pili ule (Neno la MUNGU la leo hii) songa mbele mpaka ufike kwenye mafanikio yako (mlima Horebu) yapo mema mbele usikate tamaa. ......Malaika wa BWANA akamwendea mara ya pili, akamgusa, akasema, INUKA, ULE; maana SAFARI hii ni KUBWA MNO kwako. Akainuka, akala, akanywa, AKAENDA katika NGUVU za CHAKULA hicho siku arobaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa MUNGU. .....1Falme 19:7-8..... (x). USIOGOPE. Kuweza kutimiza vyema majira na nyakati za MUNGU ONDOA HOFU ya kesho yako. (iwe ni kifo, Magonjwa, madeni, vitisho, mateso, aibu, kufeli, kuzomewa, kuachwa, nk), usiogope shikamana na MUNGU mwenye hatima na maamuzi ya mwisho kwenye maisha yako yote. .....USIOGOPE, kwa maana Mimi MUNGU ni pamoja nawe; USIFADHAIKE, kwa maana mimi ni MUNGU wako; NITAKUTIA NGUVU, naam, NITAKUSAIDIA, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu". .....Isaya 41:10..... Ni swala la majira na wakati wa MUNGU tu, Wewe sio wa kawaida, Yupo mwaamuzi wa mwisho, MUNGU ambaye hashindwi na chochote, ndiye mwenye hatima yako, mwamini YESU ili kitu au mwanadamu yeyote asikupangie hatima yako, usipomwamini YESU KRISTO mwenye hatima ya maisha yako, utapangiwa majira na nyakati za kuishi. Hitimisho. ....Tutaendelea.... Rejea “Indeed, I have inscribed [a picture of] you on the palms of My hands; Your city walls [Zion] are continually before Me". .......Isaiah 49:16....... Ev. Erasmus Pascrates Kakiza +255 782 546 914 @2024 The year of my shining.❤

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza 8 днів тому

    ❤❤ ❤ 🎉🎉🎉

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza 13 днів тому

    Somo: MAJIRA NA NYAKATI ZIMEBEBA MAISHA YAKO °°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°° Fuatilia UA-cam. Https://youtube.com/@Rwizakakiza Sehemu 15: ‭""Kwa KILA JAMBO kuna MAJIRA yake, Na WAKATI kwa KILA KUSUDI chini ya mbingu"" .....Mhubiri 3:1..... 6. AINA 2 ZA MAJIRA NA NYAKATI KATIKA MAISHA YAKO. 6. 1. MAJIRA NA NYAKATI YA MWANADAMU. Haya ni majira na nyakati zinazopangwa na Mwanadamu kwa utashi, uwezo, Ugunduzi na mamlaka aliyopewa na MUNGU. Ni uwezo wa kutambua majira na nyakati na namna ya kuenenda kwa nyakati zenyewe ili kuendesha maisha yake ya kila siku na maisha ya mwingine pia. Mwanadamu huyu katika majira yake na nyakati zake za kibinadamu anaweza kupanga aishije (vibaya au vyema). Kutokana na anavyopanga kuishi anaweza kusaidia mapenzi ya MUNGU kutumia au akakwamisha mapenzi (makusudi) ya MUNGU yasitimie kwa muda sahihi. Tujifunze jambo kwa Bikira Maria na Nabii Eliya. (i). BIKIRA MARIA. .....‭ Malaika akaingia nyumbani kwa Bikira Mariamu akasema, "Salamu, uliyepewa neema, BWANA yu pamoja nawe". "Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa MUNGU". "Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita YESU". Mariamu akamuuliza malaika, "Litakuwaje neno hili, maana sijui mume?" Malaika akajibu akamwambia, "ROHO MTAKATIFU atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa KITAKATIFU, Mwana wa MUNGU". kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa MUNGU". Mariamu akasema, "Tazama, mimi ni mjakazi wa BWANA; na iwe kwangu kama ulivyosema". Kisha malaika akaondoka akaenda zake. .....Luka 1:28 - 38...... Hapo unaona Mariamu alikuwa tayari ameposwa, kwa lugha nyingine alikuwa na MIPANGO au makusudi yake kimaisha ataishije, na inaonekana yupo kwenye maandalizi ya kuolewa akiwa amejitunza (tofauti na mabinti wa sasa wanaishi na wanaume kabla ya ndoa takatifu). Lakini katikati ya maandalizi MUNGU anampa majira na nyakati zake Kwanini Mariamu alimuumba. Ashukuriwe MUNGU Mariamu alikubali. Bikira Maria alikuwa na uwezo wa kukataa ndio maana MUNGU hakumvamia Mariamu alafu ajikute ana mimba, alielezwa na Mariamu akakubali kutekeleza majira na nyakati za MUNGU. (ii). NABII ELIYA. .....Yezebeli akampelekea Eliya mjumbe, kusema, "Miungu wanifanyie hivyo na kuzidi, nisipokufanya roho yako kesho, panapo wakati huu, kama roho ya mmojawapo wa hao (Manabii). Eliya akakimbia, akaendelea katika jangwa mwendo wa siku moja, akaenda akaketi chini ya mretemu. AKAJIOMBEA ROHO YAKE AFE, akasema, Yatosha; sasa, Ee BWANA, uiondoe roho yangu; kwa kuwa mimi si mwema kuliko baba zangu" BWANA akamwambia, Enenda, urudi njia ya jangwa la Dameski; UKIFIKA , MTIE MAFUTA ELISHA mwana wa Shafati wa Abel-Mehola mtie AWE NABII MAHALI PAKO. .....1Wafalme 19:2 - 16.... Eliya pamoja na utumishi uliotukuka alioufanya makusudi ya MUNGU hayakutimia kupitia yeye, alikwamisha Majira na nyakati za MUNGU kwa hofu ya kumwogopa Yezebel. Je wewe unaruhusu mapenzi ya MUNGU yatendeke au wewe ni chanzo cha kukwamisha makusudi ya MUNGU yasifanyike kwa muda sahihi?. ZINGATIO. Mwanadamu anapotumia vibaya majira na nyakati zake, anakwamisha kusudi la MUNGU lisitimie kwa wakati. Pili anakuwa chanzo cha kuleta au kusababisha majira na nyakati za taabu na mateso kwa wengine au hata kwake mwenyewe. Mfano. BWANA YESU anasema ....."MSIWAOGOPE WAUUAO MWILI, WASIWEZE KUIUA na ROHO; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum". ......Mathayo 10:28..... Kwa lugha hiyo sio kila kifo ni mpango wa MUNGU, ila kuna vifo vingine ni MIPANGO ya wanadamu. Maana anasema Usiogope mtu anayeua mwili, mwenye uwezo wa kuua Roho ni MUNGU pekee, lakini tukubaliane watu au mtu ana uwezo wa kukutenganisha mwili wako na Roho yako yaani kwa kukuua kabisa kimwili. Hivyo mwanadamu ana uwezo wa kuharibu majira na nyakati zake mwenyewe (kwa kujiua /madawa ya kulevya na Ulevi /Uzinzi /ushoga, nk) au kuharibu majira na nyakati za mtu mwingine (kwa kumwaribia maisha /kusingizia /Ubakaji /ulawiti /kulipiza visasi /Chuki, nk). Lakini pia majira na nyakati zako unaweza kuzifanya zikawa za furaha, amani na upendo na wengine pia wakafurahia majira na nyakati zao kwa sababu yako na mpango wa MUNGU ukawa rahisi kutimia kwako na kwao. Je majira na nyakati zako na wengine ni zipi?. 6. 2. MAJIRA NA NYAKATI YA MUNGU ....Tutaendelea.... Rejea “I assure you and most solemnly say to you, whatever you bind [forbid, declare to be improper and unlawful] on earth shall have [already] been bound in heaven, and whatever you loose [permit, declare lawful] on earth shall have [already] been loosed in heaven". ......Matthew 18:18..... Ev. Erasmus Pascrates Kakiza +255 782 546 914 @2024 The year of my shining.❤

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza 14 днів тому

    Somo: MAJIRA NA NYAKATI ZIMEBEBA MAISHA YAKO °°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°° Fuatilia UA-cam. Https://youtube.com/@Rwizakakiza Sehemu 14: ‭""Kwa KILA JAMBO kuna MAJIRA yake, Na WAKATI kwa KILA KUSUDI chini ya mbingu"" .....Mhubiri 3:1..... 5. JE, MAJIRA NA NYAKATI ZINABEBAJE MAISHA YAKO? Au KUNA UMUHIMU GANI WA MAJIRA NA NYAKATI KWENYE MAISHA YAKO? 5. 2. KUSUDI LIMEFUNGWA KWENYE MUDA. Makusudi yote yawe ya kibinadamu au yawe ya Kimungu yanafungamanishwa na muda wako wa uhai wako. MUNGU anapoamua kukuleta duniani, ujue majira yamefika na majira hayo yanaambatanishwa na kusudi au lengo la kuumbwa kwako. BWANA YESU hakuja tu ila alikuja kwenye wakati timilifu ili abebe hilo kusudi ndani ya muda uliopangwa. ‭.......Hata ULIPOWADIA UTIMILIFU wa WAKATI, MUNGU alimtuma YESU KRISTO ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria. ......Galatia 4:4..... Kupitia andiko hilo YESU KRISTO alitumwa na BABA kwa wakati uliopangwa na kwenye Mazingira yaliyopangwa ambayo ni Mazingira ya sheria. Kwanini azaliwe chini ya sheria? Kwa sababu atuweke huru mbali na sheria zote. Jina lake lilisadifu kusudi alilolijia kulifanya, Malaika alipomtokea Yusufu (Mme mtarajiwa wa Bikira Maria) alimwambie hivi... .......‭"Maria atazaa mwana, nawe (Yusufu) utamwita jina lake YESU, maana, yeye (YESU) ndiye ATAKAYEWAOKOA WATU WAKE na DHAMBI ZAO. Hayo yote yamekuwa, ili LITIMIE NENO lililonenwa na BWANA kwa ujumbe wa nabii akisema, Tazama, Bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, MUNGU pamoja nasi". ........Mathayo 1:21-23..... Nafikiri umeona Yusufu hakumwita tu jina kwa sababu ya kupenda kwake ila alisikiliza MUNGU alichomwambia kwamba mtoto amwite nani na unaona anamwita jina lililobeba kusudi aliloumbiwa yaani Wakovu wa watu kutoka kwenye dhambi zao. (Leo hii tunawaita majina watoto kutokana na majina maarufu ya Wachezaji! Waigizaji /Wasanii /wachungaji au Watakatifu fulani sio vibaya, Lakini Je hilo jina ndilo limebeba kusudi la kuumbwa kwake au umembebesha kusudi la mtu mwingine?.) Kwenye maisha yako lazima utambue hujaja bure, haijalishi ulizaliwa kwenye mazingira gani, Yawe ya uzinzi, au Ubakaji au kutelekezwa au ndoa takatifu, na kadhalika, MUNGU ana kusudi na wewe, lazima ugeuke kwa MUNGU uliza Habari ya majira na nyakati zako umebeba nini. Ndugu yangu kila mwaka, mwezi, wiki, saa, dakika, machozi au furaha na kadhalika vyote vimebeba ujumbe (kusudi fulani). Muda ukipita na kusudi lililoko kwenye muda huo linaondoka. Usipoteze muda kuangaika kutimiza makusudi ya watu ambayo hayalengi kukamilisha kusudi lako. Simama na MUNGU, unganika na watu sahihi kutimiza malengo yako na malengo ya MUNGU kwenye maisha yako, Amina. 6. AINA ZA MAJIRA NA NYAKATI KATIKA MAISHA YAKO. ....Tutaendelea.... Rejea “When [in GOD’s plan] the proper time had fully come, GOD sent His Son, born of a woman, born under the [regulations of the] Law". .....Galatians 4:4..... Ev. Erasmus Pascrates Kakiza +255 782 546 914 @2024 The year of my shining.

  • @agripinamsolomoka
    @agripinamsolomoka 15 днів тому

    Atukuzwe sana KRISTO ❤

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza 16 днів тому

    Somo: MAJIRA NA NYAKATI ZIMEBEBA MAISHA YAKO °°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°° Fuatilia UA-cam. Https://youtube.com/@Rwizakakiza Sehemu 13: ‭""Kwa KILA JAMBO kuna MAJIRA yake, Na WAKATI kwa KILA KUSUDI chini ya mbingu"" .....Mhubiri 3:1..... 5. JE, MAJIRA NA NYAKATI ZINABEBAJE MAISHA YAKO? Au KUNA UMUHIMU GANI WA MAJIRA NA NYAKATI KWENYE MAISHA YAKO? 5. 1. UNACHOKITAFUTA KIPO KWENYE MAJIRA NA NYAKATI. Kila hitaji la Mwanadamu limefungamanishwa kwenye majira na wakati wa huyo mtu. Ndio maana tunaambiwa kila jambo lina majira yake ya kutimia, na kinachotimizwa kimefungwa kwenye muda maalum. Hakuna unachokitafuta hapa duniani ambacho hujapangiwa, kama huna uhitaji nacho usingekitafuta. Na unachokitafuta unajua hakika ni chako yaani una haki zote kukipata. Na Kwanini unakitafuta? Kwa sababu ulikipoteza kwenye majira na nyakati ulizopoteza kwa kujua ama kutokujua. Daima tunatafuta kilichopotea au kupungua kwako, hautafuti ulichonacho tayari. Tunamtafuta MUNGU kwa sasa kwa sababu tulipoteza Mahusiano na MUNGU kwa sababu ya dhambi, ikatupelekea macho yetu kufa, tukabaki kumtafuta kwa kupapasa papasa, kuangaika na kumtafuta hata sehemu ambapo hayupo, na kisha kuangukia miungu mingine. Wengine kubaki kudai MUNGU hayupo kwa sababu hajulikani. ......Kwa sababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona mambo ya ibada yenu, naliona madhabahu iliyoandikwa maneno haya, KWA MUNGU ASIYEJULIKANA. Basi mimi nawahubirini habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua. Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha KUWAWEKEA NYAKATI ALIZOZIAMURU tangu zamani, na mipaka ya makazi yao; ili WAMTAFUTE MUNGU, ingawa ni kwa KUPAPASA-PAPASA, WAKAMWONE, ijapokuwa HAWI MBALI na KILA MMOJA wetu. .......Mdo 17:23-27..... Kumpoteza MUNGU yaani kuvunja mahusiano naye, inasababisha kuvuruga majira na nyakati na kushindwa kuzitambua na kutokutambua huko utaanza kuishi kwa kupishana na majira na nyakati, kwa sababu umempoteza MUNGU ambaye ulipaswa kuishi ndani yake na kuwa hai ndani yake ......Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake. ......Mdo 17:28..... Kwa kupoteza mawasiliano na MUNGU, tuliwekewa mipaka na kikomo yaani hapo ndipo tulipowekewa kila kitu kikabebwa ndani ya majira na nyakati. Na majira hayo yakipita yamepita na baraka zake. Majira yaliamriwa yabebe kila kitu chako baada gharika, alipofutilia watu na kubakiza kizazi cha Nuhu. ......Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma. ......Mwa 8:21-22...... Kama umesoma vizuri Nuhu alichokifanya ili majira na nyakati ziendelee kuwepo ingawa kwa kufungamanishwa na maisha ya mtu, Nuhu alimjengea MUNGU Madhabahu na akatoa sadaka ya KUREJESHA mahusiano na mawasiliano na MUNGU na MUNGU akaridhia sadaka yake ndio maana akaweka majira na nyakati zibebe maisha ya mtu. ......Nuhu akamjengea BWANA madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu. BWANA akasikia harufu ya kumridhisha; BWANA akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya. .....Mwa 8:20-21..... Kwa hiyo namna bora ya KUREJESHA uwapo wa MUNGU kwenye maisha yako, pamoja na kufanya maombi, Unahitaji KUMJENGEA MUNGU MADHABAHU KWA SADAKA. Ukweli ni kwamba Mwanadamu yoyote anatoa matoleo, ila Matoleo yanageuka sadaka yanapounganika na sadaka kuu ya YESU KRISTO msalabani. BWANA YESU alifanyika Madhabahu na wakati huo huo akawa sadaka ya kuteketezwa afanyike KIPATANISHO kati ya mtu aliyepotea mawasiliano na MUNGU wake. .....Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda MUNGU, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa KIPATANISHO kwa dhambi zetu. ......1Yoh 4:10...... Kujitoa Sadaka na kuunganika na YESU kutakusaidia kutopoteza majira na nyakati na kurejeshewa baraka zilipotea wakati wa ujinga kwa sababu kila unachokitafuta kipo kwenye majira na nyakati na mwenye majira na nyakati ni YESU mwenyewe ukiwa naye umepata vyote, Amina. 5. 2. KUSUDI LIMEFUNGWA KWENYE MUDA ....Tutaendelea.... Rejea “‭We have CONFIDENCE and FULL FREEDOM to ENTER the HOLY PLACE [the place where GOD dwells] by [means of] the blood of JESUS". ......Hebrews 10:19..... Ev. Erasmus Pascrates Kakiza +255 782 546 914 @2024 The year of my shining.❤

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza 17 днів тому

    Somo: MAJIRA NA NYAKATI ZIMEBEBA MAISHA YAKO °°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°° Fuatilia UA-cam. Https://youtube.com/@Rwizakakiza Sehemu 12: ‭""Kwa KILA JAMBO kuna MAJIRA yake, Na WAKATI kwa KILA KUSUDI chini ya mbingu"" .....Mhubiri 3:1..... 4. JE KAMA NIMEPOTEZA MAJIRA NA NYAKATI NIFANYE NINI ILI KUFIDIA NA KUTOKUPOTEZA TENA? 4. 4. ONGEZA BIDII, JUHUDI NA MAARIFA KUPATA MAJIRA NA NYAKATI. Namna bora ya kupata majira niliyopoteza, lazima nipate maarifa kujua nimepoteza nini, kina thamani gani, kitanisaidia nini na ningekuwa wapi. Hayo ni baadhi ya maswali ambayo yatakufanya uwe na bidii, na juhudi za kupata maarifa juu ya ulichopoteza ili ukipate. Hali ya kutafuta maarifa juu ya majira na nyakati hayavutii sana au yanakatisha tamaa, lakini ukipata kujua unachokitaka na thamani yake, utahakikisha unaweka bidii na juhudi, (Daniel alipotaka kujua haki ya taifa lake na Yeye mwenyewe alianza kusoma Vitabu kwa bidii, na akapata ufahamu, nini kilipotea na wangekuwa wapi muda huo, na juhudi zake zikasababisha MUNGU amtume malaika amfahamishe juu ya mambo aliyoyagundua) ‭..... Katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake Mfalme, mimi Danieli, kwa KUVISOMA VITABU, NALIFAHAMU HESABU ya MIAKA, ambayo neno la BWANA lilimjia Yeremia nabii, ya KUTIMIZA UKIWA wa YERUSALEMU, yaani, miaka sabini. Nikamwelekezea BWANA MUNGU uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu. Malaika akaongea nami, akasema, Ee Danieli, nimetokea sasa, ili nikupe AKILI upate KUFAHAMU. .... Dan 9:2-3, 22..... Kama umeona vizuri hapo juu Daniel kama asingevisoma Vitabu asingejua miaka ya Yerusalemu kuteseka na kikomo chake, kwa hiyo Yerusalemu na watu wake wangeendelea kuteseka (kubaki utwamani na Yerusalemu ingeendelea kuwa ukiwa yaani bila watu ingawa muda wa ukiwa umeisha muda mrefu) Kuna watu wengi wanapitia MATESO kwa sababu hawakujua muda wa kujaribiwa kwao. Daima jaribu uwa limefungwa ndani ya muda fulani, lakini usipojua muda wake na muda wake ukaisha bila kujua, uwa SIO JARIBU TENA ball ni MATESO ya shetani, chunguza ulilonalo ni Jaribu au ni mateso na unaendelea kujifariji ni jaribu langu, kumbe ni mateso. Pia kuna haja kubwa ya kuweka Bidii, juhudi na maarifa ya kulinda majira na nyakati nlizomo sasa na zile zijazo. Kati ya HASARA KUBWA kwenye maisha ya mtu ni KUTOKUJUA UNAELEKEA WAPI , Kesho yako itakuwaje. Unasema inawezekana vipi nijue kesho yangu!, INAWEZEKANA. Ukiachana na YESU ambaye ni MUNGU; Paulo alikuwa mtu kama wewe, lakini alijua kifo chake ni lini na cha namna gani, ingawa watu walimkataza asiende, lakini alijua nyakati na majira yake (..Mdo 21:11-14..), kazi ya utume wake Paulo alijua kikomo chake ni lini (ingawa sisi tumeishia kuwaandikia watu wanaokufa kwamba mwendo wao wameumaliza na Imani wameilinda, tunawasemea bila kuwa na uhakika kama kweli wamemaliza mwendo kweli, Je imani wameilinda kweli) na Paulo alijua taji gani atapata mbinguni (Wewe saa nyingine huna hakika kama mbinguni unaenda au la, na kama unaenda huenda hujui taji gani utapewa), Paulo alisema hivi ......."Mimi sasa namiminwa (kutolewa sadaka), na wakati wa kufariki kwangu umefika. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya hayo NIMEWEKEWA TAJI ya HAKI, ambayo BWANA , mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake". .......2 Timotheo 4:6-8..... Kwanini Paulo alijua majira na nyakati zake zilizopita, zilizopo na zijazo?, kwa sababu ya kiwango kikubwa cha mahusiano na MUNGU, na MUNGU akamtuma Roho wake Mtakatifu amjulishe hata yajayo. ......ROHO MTAKATIFU atakapokuja, huyo Roho wa kweli, ATAWAONGOZA awatie kwenye KWELI YOTE; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote ATAKAYOYASIKIA (Kwa MUNGU) atayanena, na MAMBO YAJAYO ATAWAPASHA HABARI yake. .....Yohana 16:13.... Kumbe na (sisi) wewe, Usiishi kwa hasara ishi kwa kujua ulipotoka, ulipo na unapoelekea na majira na nyakati zako zilibeba nini, zimebeba nini na zitabeba nini, ongeza bidii, juhudi na maarifa utafanikiwa. 5. JE, MAJIRA NA NYAKATI ZINABEBAJE MAISHA YAKO? Au KUNA UMUHIMU GANI WA MAJIRA NA NYAKATI KWENYE MAISHA YAKO? ....Tutaendelea.... Rejea “When He, the Spirit of Truth, comes, He will guide you into all the truth [full and complete truth]. For He will not speak on His own initiative, but He will speak whatever He hears [from the FATHER -the message regarding the Son], and He will disclose to you what is to come [in the future]" .....John 16:13..... Ev. Erasmus Pascrates Kakiza +255 782 546 914 @2024 The year of my shining.❤

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza 22 дні тому

    MUNGU akubariki sana

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza 22 дні тому

    Somo: MAJIRA NA NYAKATI ZIMEBEBA MAISHA YAKO °°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°° Fuatilia UA-cam. Https://youtube.com/@Rwizakakiza Sehemu 11: ‭""Kwa KILA JAMBO kuna MAJIRA yake, Na WAKATI kwa KILA KUSUDI chini ya mbingu"" .....Mhubiri 3:1..... 4. JE KAMA NIMEPOTEZA MAJIRA NA NYAKATI NIFANYE NINI ILI KUFIDIA NA KUTOKUPOTEZA TENA? 4. 3. LINDA SANA MAJIRA NA NYAKATI. Ukitaka kulinda majira na nyakati yasije kupotea, lazima ujue kinachosababisha mzunguko wa maisha yako ukabadilika ni nini. MOYO /NAFSI ndicho kitu cha kulinda kuliko unavyo fikiri kwa sababu Moyo Ukivurugwa, maisha yanavurugika, maisha yakivurugika, majira na nyakati hayapo salama kwa kuwa ndani ya moyo ndimo uzima unapotokea kama moyo (nafsi) imeponywa. ......LINDA MOYO wako KULIKO yote UYALINDAYO; Maana ndiko ZITOKAKO CHEMCHEMI za UZIMA ... .....Mithali 4:23..... Kwanini MUNGU anaweka mkazo KUULINDA moyo, kwa sababu usipoulinda moyo ukajeruika yaani ukaumizwa, kinachotokea badala ya kutoa chemichemi ya uzima, Moyo utatoa chemichemi za Mauti, hivyo moyo ulioumizwa usiambatane nao wala usiendee njia zake nawe utaumizwa na utaangamia. .....‭MOYO wako USIZIELEKEE NJIA ZAKE, Wala USIPOTEE katika MAPITO yake. Maana AMEWAANGUSHA wengi WALIOJERUHI, Naam, jumla ya WALIOUAWA naye (moyo) ni jeshi kubwa. ......Mithali 7:25-26.... Umeona hapo juu namna ya kulinda moyo, kujiepusha na mtu mwenye maumivu, lakini haimaanishi usimsaidie. Kuna watu wamepoteza hatma zao baada ya majira na nyakati zao kuvurugwa na moyo uliojeruika, unatoa uovu badala ya mema. ......Kwa maana ndani ya MIOYO ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi. .....Marko 7:20-23.... Mfano 1 Kuna watu kutokana na maumivu ya nafsi (moyo), WAMEHARIBU MAISHA YAO WENYEWE kwa Unywaji na Ulevi, Wengine wamebaka hatma yake wakaishia Gerezani, Wengine wameua na Kuishi kujuta, kukimbia na kutangatanga, Wengine wameumizwa kimahusiano wameishia kutojithamini na kujiuza, Wengine wamekosa uaminifu kutokana na maisha waliopitia. Watu wa namna hiyo hawawezi kulinda mioyo yao, na kutoulinda moyo, majira na nyakati zao zimeandamwa na matukio ya masikitiko na huzuni. Mfano 2. Wengine WAMEJIHARIBU kutokana na kuambatana na walioumizwa mioyo. Daima mtu aliyeumia kwake ni malalamiko, Mashaka, ukatili, matusi, na manung'uniko. Watu wengi wamejiingiza kwenye vitendo vya ajabu (Ushoga, Visasi, Ushirikina, Wizi, Ulevi, Madawa ya kulevya, Usaliti, nk) kwa sababu ya kuambatana na makundi au watu walioumizwa na mwisho wa siku nao wamejikuta majira na nyakati zao zimeharibika. Kwa hiyo namna nzuri ya kulinda majira na nyakati zako ni kulinda moyo wako, maana bila hivyo utateseka na ukiteseka hakuna namna majira na nyakati zako zinaweza kuwa salama. Na kama umepitia maumivu yoyote kwenye maisha yako, lazima majira na nyakati zimevurugika, kuna makusudi ya MUNGU na baraka zako zilichengeshwa, yakupasa uzikomboe na kuzirejesha kwa kufunga na maombi. 4. 4. ONGEZA BIDII, JUHUDI NA MAARIFA KUPATA MAJIRA NA NYAKATI. ....Tutaendelea.... Rejea “Watch over your heart with all diligence, For from it flow the springs of life. .....Proverbs 4:23.... Ev. Erasmus Pascrates Kakiza +255 782 546 914 @2024 The year of my shining.❤

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza 28 днів тому

    Somo: MAJIRA NA NYAKATI ZIMEBEBA MAISHA YAKO °°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°° Fuatilia UA-cam. Https://youtube.com/@Rwizakakiza Sehemu 10: ‭""Kwa KILA JAMBO kuna MAJIRA yake, Na WAKATI kwa KILA KUSUDI chini ya mbingu"" .....Mhubiri 3:1..... 4. JE KAMA NIMEPOTEZA MAJIRA NA NYAKATI NIFANYE NINI ILI KUFIDIA NA KUTOKUPOTEZA TENA? 4. 2. REJESHA MAJIRA NA NYAKATI Somo lililopita tuliona kama umepoteza majira na nyakati njia mojawapo ya kufanya ni KUKOMBOA MAJIRA NA NYAKATI. Leo tunapozungumzia swala la UREJESHO WA MAJIRA NA NYAKATI ni kama vinafanana lakini vina utofauti mkubwa. Nini maana ya UREJESHO? Urejesho ni hali au kitendo cha kukomboa kitu au mtu na kumrudisha kwenye NAFASI yake. .....Maana NITAKURUDISHIA afya, nami NITAKUPONYA JERAHA zako, asema BWANA, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye. ......Yeremia 30:17..... Kwenye andiko hilo unagundua wazi mtu anaweza akaponywa, lakini akabakia na majeraha au makovu ya ugonjwa. Urejesho unakurudisha kwenye nafasi yako ya awali. Labda uliugua Ukoma ukakatika mikono, utaokolewa na ugonjwa wa Ukoma na utapona lakini haimaanishi mikono imerudi, ili mikono ilirudi dai Urejesho wa mikono. Swala la Ukombozi (Wokovu) ninaweza kusema unalenga sana kuanzia Rohoni, lakini Urejesho unalenga sana kuona kwa macho ya kawaida. Hivyo Usikubali kuishi kwamba nimeomba na naamini yametukia nayo ni yangu, hakikisha unayaona kwa macho ya kawaida (upate majibu ndio unyamaze) Watu wengi Wanaongoka (wokovu) lakini maisha yao hayana radha, utakuta hali yake, Uchumi wake, mipango yake inazidi kuporomoka badala ya kustawi. Wokovu sio ufukara ingawa unaweza kupita, Furaha ya MUNGU urejeshewe kila kitu ulichokipoteza hata awali. ....Nami NITAWARUDISHIA hiyo MIAKA ILIYOLIWA na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu. ....Yoeli 2:25.... Lengo kuu la MUNGU kukurudishia hata vilivyopotea hataki uhuzunike na kujutia Kwanini ni Mkristo, bali ndani ya nafsi yako pawepo raha (Haimaanishi hutopitia changamoto, utazipitia lakini furaha ya MUNGU ndani haiondoki) .....Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi YESU ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; NANYI MTAPATA RAHA NAFSINI mwenu. ......Mathayo 11:29..... Nafsi yako ikifurahi na ukatajirishwa kwa kila kitu (sio pesa tu), utakuwa na ukarimu wa kuwasaidia wengine, na watu watataka kumjua YESU wako uliyenaye. .....MKITAJIRISHWA KATIKA VITU VYOTE MPATE KUWA na UKARIMU WOTE, umpatiao MUNGU shukrani kwa kazi yetu. .....2 Kor 9:11...... Tunakosa ukarimu kwa sababu na sisi tuko hoi, hatuna kitu na kama huna kitu kuna watu hautowafikia au hawatakuelewa. Lakini unaweza kuamua kuanza upya na MUNGU akabadilisha hali yako. .....‭Badala ya aibu yenu mtapata heshima maradufu, na badala ya fedheha wataifurahia sehemu yao; basi katika nchi yao watamiliki maradufu; furaha yao itakuwa ya milele. .....Isaya 61:7..... Usiishie kusema nimeokoka, Mimi ni Mkristo wakati maisha yako hayamtangazi YESU bali yanamwaibisha YESU kuanzia kwenye HALI yako, MATENDO yako, na maisha yako kiujumla, yakupasa urejehe kila kitu chako na uongezee na ya sasa ili MUNGU atukuzwe kwenye kila majira na nyakati zako zote. ......Kwa sababu hiyo BWANA asema hivi, UKIRUDI, ndipo mimi NITAKAPOKUREJEZA, upate kusimama mbele zangu; nawe UKITOA KILICHO cha THAMANI KATIKA KILICHO KIBOVU, utakuwa kama kinywa changu; nao watakurudia wewe, bali hutawarudia wao. ......Yeremia 15:19..... Unaweza kutoa kitu kizuri kwenye kibovu, hata kama ni mdhambi kiasi gani unaweza kuamua leo kumpa nafasi BWANA YESU awe BWANA na Mwokozi wako binafsi na YESU KRISTO atakuokoa na kukurejesha. Hata kama ni Mkristo unaishi kwa majuto na maangaiko, unaweza kurejea kwa MUNGU upya na maisha yako yakabadilika, Amina. 4. 3. LINDA SANA MAJIRA NA NYAKATI. ....Tutaendelea.... Rejea “Therefore, thus says the LORD [to You], “If you repent [and give up this mistaken attitude of despair and self-pity], then I will restore you [to a state of inner peace] So that you may stand before Me [as My obedient representative]; And if you separate the precious from the worthless [examining yourself and cleansing your heart from unwarranted doubt concerning My faithfulness], You will become My spokesman. Let the people turn to you [and learn to value My values]- But you, you must not turn to them [with regard for their idolatry and wickedness]. .....Jeremiah 15:19..... Ev. Erasmus Pascrates Kakiza +255 782 546 914 @2024 The year of my shining.❤

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza 29 днів тому

    Somo: MAJIRA NA NYAKATI ZIMEBEBA MAISHA YAKO °°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°° Fuatilia UA-cam. Https://youtube.com/@Rwizakakiza Sehemu 9: ‭""Kwa KILA JAMBO kuna MAJIRA yake, Na WAKATI kwa KILA KUSUDI chini ya mbingu"" .....Mhubiri 3:1..... 4. JE KAMA NIMEPOTEZA MAJIRA NA NYAKATI NIFANYE NINI ILI KUFIDIA NA KUTOKUPOTEZA TENA? 4.1. KOMBOA MAJIRA NA NYAKATI. Maana ya UKOMBOZI ni hali au mchakato wa kutoa kitu au mtu sehemu isiyo sahihi na kumwamishia /kumweka sehemu salama. .....MUNGU alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake". .....Kolosai 1:13..... Maana ya Ukombozi wa majira na nyakati ni kuokoa majira na nyakati uliyoyapoteza tangu kuzaliwa kwako mpaka sasa, Na katika ukombozi huo lazima upitie hatua kadhaa kukamilisha ukombozi wa majira na nyakati kama ifuatavyo:- (i). PELELEZA UJUE ULICHOKIPOTEZA. Kama hautojua ulichopoteza, hautoona umuhimu wa kukomboa. Uliza watu Utotoni walikuonaje na ulikuwa unapendelea nini, Jiulize mwenyewe maisha unayoyaishi ndiyo uliyotaka kuishi. Waulize watu MUNGU aliwaleta karibu na wewe, Ungefaa kuwa nani, kuwa wapi, na wanakuonaje. Itakusaidia kufahamu ulichopoteza. .....Uliza sasa SIKU ZILIZOPITA, zilizokuwa kabla yako, tangu siku ile MUNGU aliyoumba mwanadamu juu ya nchi, na toka pembe hii ya mbingu hata pembe hii, kwamba KUMETUKIA NENO LO LOTE kama neno hili kubwa, au kwamba kumesikiwa habari ya neno kama hili? .....Kumb 4:32...... (ii). TAMBUA THAMANI YA ULICHOPOTEZA. Baada ya kujua ulipoteza nini tambua thamani ya baraka na kusudi lililokuwa limebebwa ndani ya majira na nyakati ulizopoteza, Itakusaidia kudai na kuomba kwa mzigo. MUNGU alijua thamani na heshima ya mtu ndio maana alishuka kumkomboa. .....Kwa kuwa ULIKUWA wa THAMANI MACHONI PANGU, na MWENYE KUHESHIMIWA, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako. ......Isaya 43:4..... (iii). BEBA SILAHA YA IMANI. Unachoenda kukikomboa kinategemea kiko wapi, kiko na nani, na kimezingirwa ulinzi kiasi gani. Hivyo mengine kuyakomboa yanahitaji Imani ya kawaida lakini mengine yanahitaji imani kubwa (silaha kubwa na nzito) kuhamisha milima. Omba MUNGU akupe sikaha ya imani na kumtegemea yeye akupiganiaye. .....Mitume wakamwambia BWANA, Tuongezee imani. ......Luka 17:5.... Usipokomboa wakati, wakati utakutaabisha kwa sababu zama tulizomo ni za uovu na madanganyifu mengi. ....Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; MKIUKOMBOA WAKATI kwa maana zamani hizi ni za uovu. .....Efeso 5:15-16.... 4.1. REJESHA MAJIRA NA NYAKATI ....Tutaendelea.... Rejea “For He has rescued us and has drawn us to Himself from the dominion of darkness, and has transferred us to the kingdom of His beloved Son" ......Colossians 1:13..... Ev. Erasmus Pascrates Kakiza +255 782 546 914 @2024 The year of my shining.❤

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza Місяць тому

    Somo: MAJIRA NA NYAKATI ZIMEBEBA MAISHA YAKO °°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°° Fuatilia UA-cam. Https://youtube.com/@Rwizakakiza Sehemu 8: ‭""Kwa KILA JAMBO kuna MAJIRA yake, Na WAKATI kwa KILA KUSUDI chini ya mbingu"" .....Mhubiri 3:1..... 3. JE UNATAMBUA MAKOSA UNAYOYAFANYA KWENYE MAJIRA NA NYAKATI YANATAABISHA MAISHA YAKO? ....Namaanisha kama hautatambua ni wapi au kipi kinafanya nipoteze wakati, maisha yako yote yatakuwa ya kutaabika kwa sababu majira na wakati zikipita zimepita na baraka zinazobebwa ndani ya muda huo unazikosa. Tukio au Kitu chochote ambacho unakifanya ambacho SIO cha majira hayo Au Unachopuuzia kukifanya wakati ni cha majira hayo na kikapita bila kukifanyia kazi, uwe na uhakika kitakutaabisha mbeleni. Ikumbukwe ukishindwa na kusudi lililobebana na jambo hilo halitatimia. Tuchukue Mifano kwenye MHUBIRI 3:2-8 .....Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; (Wakati wa Uzalishaji, kwako ndio kila kitu unaharibu, kwa kuvunja uhusiano na watu muhimu, Wakati wa kupata watoto unawaza utawalisha nini, unatamani kufanya mambo makubwa lakini mazingira yanakuonyesha haiwezekani, Majira yakipita yamepita Usione kutoweza yaani kufa, bali dhubutu na tenda) ....Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa; (Ebu fikiri ni majira ya kupanda wewe ndio unaandaa shamba, kamwe huwezi kubarikiwa ingawa utapanda, lakini nje ya wakati, na ukikosa faida utang'oa tu). ....Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza; (Watu wengi wakati wao unakuwa ni wakati wa kicheko na kucheza, lakini kwa sababu ya walipoteza na kupishana na majira na nyakati wapo kwenye kuomboleza na kulia, kumbe ni wakati wa kufurahi) ....Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; (Wakati wa kujiwekeza kiuchumi, kiroho, kihuduma, na kimaendeleo, Wewe unatupa mawe yaani unapoteza muda kwa kubet, movie, ushabiki, nk. Wakati wa kukusanya uzeeni unalaaani watoto wako kisa hawakujali, kumbe wewe ndiwe wa kuwapa urithi). ....Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia; (Wewe ni mwanafunzi ngazi yoyote, ni wakati wa kusoma, Unaishi na mtu kama Mme na mke, uwe na uhakika wakati Ukifika wa kufurahia ndoa (kukumbatia), utakuwa uko kwenye majuto, umeharibu mwenyewe). ...... Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa; (Wakati kutafuta kwa bidii na nguvu zako zote, lakini unaamka muda utakao wewe, unapoteza wakati, utakuja kuwasumbua watu). .....Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena; (Wakati wa kutoongea, Wewe unaongea, utararua baada ya kushona). ....Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani. (Vita yoyote ni kosa la wakati na majira, inaanza hivi... Wakati wa kupenda haunyeshi upendo na yule anayekupenda unampoteza, Unakuja kugundua ulipaswa kupenda kumbe umeisha chelewa, kwako utaona unaonewa, unanyanyaswa, kitakachofuata ni Chuki na visasi na hapo hakuna amani tena ni vita). Je umetambua makosa tunayoyafanya kwa kupoteza majira na nyakati yanavyoleta maomnolezo kwenye maisha yetu? ....... Mhubiri 3:2-8...... 4. JE KAMA NIMEPOTEZA MAJIRA NA NYAKATI NIFANYE NINI ILI KUFIDIA NA KUTOKUPOTEZA TENA? ....Tutaendelea.... Rejea “A time to love and a time to hate; A time for war and a time for peace". .......Ecclesiastes 3:8..... Ev. Erasmus Pascrates Kakiza +255 782 546 914 @2024 The year of my shining.❤

  • @felixmushi3354
    @felixmushi3354 Місяць тому

    MUNGU atukuzwe endeleeni kutuma tunabarikiwa sana @mtwara

    • @Rwizakakiza
      @Rwizakakiza Місяць тому

      Amina MUNGU akubariki sana, sikujua unafatilia kutoka huko, MUNGU akubariki sana

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza Місяць тому

    Somo: MAJIRA NA NYAKATI ZIMEBEBA MAISHA YAKO °°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°° Fuatilia UA-cam. Https://youtube.com/@Rwizakakiza Sehemu 7: ‭""Kwa KILA JAMBO kuna MAJIRA yake, Na WAKATI kwa KILA KUSUDI chini ya mbingu"" .....Mhubiri 3:1..... JE, NINI MAANA YA MAJIRA NA NYAKATI? 2. MAANA YA NYAKATI. Nyakati ni wingi wa Neno.... Wakati.... Na maana ya Wakati ni kipindi au muda maalum unaonyesha tukio lililofanyika /linalofanyika /litakalofanyika. ZINGATIO: MAJIRA yamebeba TUKIO (Jambo fulani), Lakini NYAKATI zinabeba KUSUDI la tukio. Hivyo majira na nyakati huwezi kuvitenganisha (Kila tukio liwe baya au jema kwenye maisha yako, imebeba lengo au kusudi maalum) .....Mhubiri 3:1..... Shetani anaweza akakuruhusu ukatambua majira (yaani tukio ulilopo linalokuandama), lakini atakuzuia usijue kusudi lililomo kwenye tukio. Au akazui vyote viwili yaani usijue upo majira gani, na nyakati zimebeba nini kwa ajili ya maisha yako. Kati ya vitu vinavyomuhuzunisha MUNGU ni kutotambua majira na nyakati ulizomo kwa sasa. (Soma kwa makini) .....‭YESU Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia, akisema, "Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa YAMEFICHWA machoni pako. Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua MAJIRA YA KUJILIWA kwako. ....Luka 19:41-44.....(SUV‬) Tusome tafsiri nyingine tuelewe zaidi, ......‭YESU alipoukaribia mji wa Yerusalemu, akautazama kisha akaanza kuulilia, akisema, “Laiti ungelijua leo KILE KINACHOKULETEA AMANI. Lakini KIMEFICHWA kwako USIKIJUE sasa. WAKATI unakuja, ambao adui zako watajenga ukuta kukuzunguka na kukuzingira pande zote. Watakuteketeza wewe na watu wako wote. Hakuna jiwe hata moja katika majengo yako litaachwa juu ya jiwe jingine. HAYA YOTE YATATOKEA KWA SABABU HUKUJUA WAKATI ambao MUNGU ALIKUJA KUKUOKOA.” .....Luka 19:41-44 TKU‬..... Yerusalemu ilikuwa kwenye tukio yaani majira ya furaha na amani (kumbuka kwenye majira nilisema... Unapokuwa kwenye furaha au amani uweke tahadhari). Lakini Yerusalemu haikutambua ni nani anaupa amani Yerusalemu, na MUNGU akashuka kwa ajili ya Yerusalemu kwa sababu aliona taabu itakayoipata Yerusalemu, Cha ajabu Yerusalemu haikutambua majira na nyakati kwamba MUNGU aneyeleta amani, ameshuka kuwaokoa. Kuna matukio mengi yamepita kwenye maisha yetu lakini hatukujua yamebeba nini kwenye maisha yetu, kwa sababu ya kutojua tupo kama tulivyo leo. Mfano 1 Majira ya kupata Elimu, unaelewa kusudi liliobebeshwa kwenye Elimu (usipojua majira ya kusoma, utaponda raha na majira ya kuponda raha yakifika utaponda shida, taabu na majuto). Mfano 2 Majira ya kuwa na familia, Je unaelewa kusudi la MUNGU la kuwa na familia? Ulifanya sherehe/harusi unaelewa kusudi la MUNGU kuruhusu ukasherekea?. Umepata watoto au huna watoto, Unaelewa ni kwanini? (Usipotambua ndoa /familia yako itakuwa kwenye mafarakano, ugomvi usioisha, Chuki na visasi) Mfano 3 Majira ya Utajiri na Umaskini, Unaelewa kusudi kwanini wewe una mali nyingi una nyumba, unakula unachotaka, ni tajiri? Au kwanini wewe huna hata pa kulala, unapanga, kipato ni shida, kula taabu, ni maskini? (Usipojua utaukosa Ufalme wa MUNGU na kuambulia moto wa milele yaani Jehanamu. Mfano 4 Majira ya Cheo /Nafasi /Wadhifa /Huduma /Elimu, Unambua kusudi lake au unaona ni jitihada zako au wazazi wako wsmekupa hizo nafasi? (Usipotambua utaishia kutumia, lakini hautatumikiwa yaani kuwa boss sahau). JE UNATAMBUA MAKOSA UNAYOYAFANYA KWENYE MAJIRA NA NYAKATI YANATAABISHA MAISHA YAKO? ....Tutaendelea.... Rejea “There is a season (a time appointed) for everything and a time for every delight and event or purpose under heaven" ......Ecclesiastes 3:1..... Ev. Erasmus Pascrates Kakiza +255 782 546 914 @2024 The year of my shining.❤

  • @agripinamsolomoka
    @agripinamsolomoka Місяць тому

    ❤❤❤

  • @agripinamsolomoka
    @agripinamsolomoka Місяць тому

    ❤❤❤❤

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza Місяць тому

    Somo: MAJIRA NA NYAKATI ZIMEBEBA MAISHA YAKO °°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°° Fuatilia UA-cam. Https://youtube.com/@Rwizakakiza Sehemu 6: ‭""Kwa KILA JAMBO kuna MAJIRA yake, Na WAKATI kwa KILA KUSUDI chini ya mbingu"" .....Mhubiri 3:1..... JE, NINI MAANA YA MAJIRA NA NYAKATI? 1. MAANA YA MAJIRA. Baada ya kujifunza nini maana ya majira, Tuanze kuchunguza. Je, majira haya manne kwa mwanadamu kiroho yana maana gani? 1. (d). MAJIRA YA MASIKA (SPRING SEASON) ....Huu ni msimu wa mvua nyingi, machipuko na kustawi sana hasa uoto. Msimu wa mvua pamoja na kuonekana mzuri, lakini ni muhimu kuchukua tahadhari kwa sababu mvua za ajabu unyesha na kusababisha Mafuriko na maafa makubwa hutokea. Kiroho msimu huu ni mzuri sana na nyimbo nyingi uimbwa kama vile.... NIMENYESHEWA NA MVUA YA BARAKA... ni wakati wa kicheko, kufurahi na kusahau huzuni, MUNGU anyeshe mvua ya baraka kwako. ......FURAHINI, basi, enyi wana wa Sayuni, MKAMFURAHIE BWANA, MUNGU wenu; kwa kuwa yeye HUWAPA ninyi MVUA ya MASIKA, kwa KIPIMO cha HAKI, naye HUWANYESHEA mvua, mvua ya MASIKA, na mvua ya VULI, kama kwanza. ....Yoeli 2:23.... Wakati unafurahia masika kuna mwingine majira hayo mvua yamezuiliwa kwake hayapo, Hajawahi kujua kwamba kuna mvua ya baraka kwake ni Ukame, maangaiko, Mashaka ya kesho nitaishije, itakuwaje nk. .....Tena NIMEIZUIA MVUA msiipate, ilipobaki miezi mitatu kabla ya mavuno; nami nimenyesha mvua juu ya MJI MMOJA, NIKAIZUIA mvua ISINYESHE juu ya mji MWINGINE; sehemu moja ilipata mvua, na sehemu isiyopata mvua ilikatika. .....Amosi 4:7... Mwingine ananyeshewa na mvua, ila muulize ni mvua gani inanyesha kwake (Ni mvua ya gharika, Maafa, uharibifu) na yenyewe ni mvua pia ....Badala ya mvua aliwapa MVUA YA MAWE, Na MOTO wa miali katika nchi yao. .....Zaburi 105:32.... Wakati unaomba usiombe Mvua, bali Tambua unaomba mvua ya aina gani. Ukiomba Mme /mke, tambua Mme /mke wa aina gani. Ukiomba mtoto, sio ilimradi mtoto - hata kibaka ni mtoto pia, Ukiombea Uchumi bainisha wazi unaomba upi na MUNGU atanufaikaje nao, la sivyo unaweza kupewa na usijue kama umejibiwa au ukakulemea (ukakuangamiza). Tunaomba kwa roho na kwa akili pia. ....Imekuwaje, basi? NITAOMBA kwa ROHO, tena NITAOMBA kwa AKILI pia; mtaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia. .....1 Kor 14:15.... ZINGATIO KWENYE MAJIRA (i). Je umetambua upo majira gani kwa sasa na unaelekea majira gani? (Jibu) (ii). Tambua wazi kwamba majira na wakati yamewekwa na MUNGU, hivyo kila mtu uwe unamjua MUNGU au humjui MUNGU lazima utapita kila majira (Iwe kiangazi, Vuli, baridi au masika) hauwezi kukwepa hata ukikemea ni jambo lililoamriwa na limefungamanishwa na maisha yako. .....Muda NCHI IDUMUPO, MAJIRA ya KUPANDA(Masika), na MAVUNO(Vuli), wakati wa BARIDI(Kipupwe) na wakati wa HARI(Kiangazi), wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma. .....Mwa 8:22.... 2. MAANA YA NYAKATI. ....Tutaendelea.... Rejea “The blessing of the Lord brings [true] riches, And He adds no sorrow to it [for it comes as a blessing from God]" .....Proverbs 10:22..... Ev. Erasmus Pascrates Kakiza +255 782 546 914 @2024 The year of my shining.

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza Місяць тому

    Ahsante sana kwa Watazamaji na Wasikilizaji kutoka kokote duniani MUNGU akubariki sana

  • @MINISTERBAHATIMPUME-px4pf
    @MINISTERBAHATIMPUME-px4pf Місяць тому

    MUNGU akubariki unatusaidia sana

    • @Rwizakakiza
      @Rwizakakiza Місяць тому

      Amina Naombeni sana zenu, niwe na Vifaa kamilifu

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza Місяць тому

    Somo: MAJIRA NA NYAKATI ZIMEBEBA MAISHA YAKO °°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°° Fuatilia UA-cam. Https://youtube.com/@Rwizakakiza Sehemu 5: ‭""Kwa KILA JAMBO kuna MAJIRA yake, Na WAKATI kwa KILA KUSUDI chini ya mbingu"" .....Mhubiri 3:1..... JE, NINI MAANA YA MAJIRA NA NYAKATI? 1. MAANA YA , MAJIRA. Baada ya kujifunza nini maana ya majira, Tuanze kuchunguza. Je, majira haya manne kwa mwanadamu kiroho yana maana gani? 1. (c). MAJIRA YA KIPUPWE (WINTER SEASON). .... Huu ni msimu wa baridi kali, maeneo mengine husababisha watu au wanyama kuhama au kubadilika kwa sababu ya barafu (baridi kali) na upepo mkali. Kiroho msimu huu wa baridi kali unahitaji umakini, uvumilivu na kujipanga upya. Ni wakati ambao unahitaji uwe na akiba isiyooza ambayo inaweza kutumiwa kipindi hiki. .......Mtu mwema katika AKIBA NJEMA hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya. ....Mathayo 12:35.... Kwenye andiko hili linaonyesha asili ya akiba inaanzia rohoni na matokeo yake yanaonekana wazi nje. Kama umezoea mawazo mabaya ndicho kitakachotokea nje, kama ni mvivu kuanzia rohoni hata nje bidii haitaonekana. Lakini pia kama umezoea kujiwekea akiba, wakati wa uhitaji hautasumbuka. .....Ewe mvivu, mwendee chungu, ZITAFAKARI NJIA ZAKE ukapate hekima. Kwa maana YEYE HANA akida, Wala msimamizi, wala mkuu, Lakini HUJIWEKEA AKIBA ya chakula wakati wa JUA; Hukusanya chakula chake wakati wa MAVUNO. .....Mithali 6:6-8..... Pia msimu wa baridi kinaweza kubeba lawama (Utaona uhalisia halisi), Mfano..... Sherehe ina mikakati ya kuikamilisha binafsi, usipokuwa makini unaweza kulaumu watu kumbe linakuhusu mwenyewe, maana nyuma msimu wa jua umepita na msimu wa mavuno umepita ukasahau kwamba kuna msimu wa kipupwe alafu ndio wakati wa sherehe, tulia jipange vizuri na MUNGU. Msimu huu wa kipupwe muda wa kazi ni mfupi sana, na Wakati wa giza (usiku) ni mwingi sana. Hapa ndipo pa kuonyesha nuru yako gizani, hata kama wote wamelala, kwako sio wakati wa kulala, Bali kutafakari Kwanini upo msimu huu, Kuomba, kutulia kwenye Neno la MUNGU, na kutengeneza ushirika mzuri ili msimu ujao uwe wa kuchanua na kutoa nuru kamilifu ya kuwasaidia watu. .....Nuru yako na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yako mema, wamtukuze BABA yako aliye mbinguni. .....Mathayo 5:16.... Wakati wengine wanasema baridi inatuua, Wewe uwe nuru kwao uwaambie cha kufanya. Msimu wa baridi ni muda wa kujiponya, kujirekebisha, kupokea maoni hata kama yanauma na kujipanga upya kabisa. Matokeo ya kujipanga upya kitaruhusu Uzalishaji mzuri na mwema wenye manufaa. Kipindi hiki usitumie njia mbadala kwa sababu ni baridi (Mfano vinywaji vikali ukifikiri utamaliza baridi). Namaanisha nini - Watu wengi hawataki kukubaliana na uhalisia kwamba nipo majira fulani na nifanye nini, bali anaweza yuko majira ya jua kali ila anajidai yupo kwenye kipindi cha mavuno, ukiwa hivyo, Ukumbuke kuna kipindi cha kipupwe chenye upepo. Kazi ya upepo ni kuondoa visivyo na nguvu, ili vyenye nguvu vibaki (Kipindi hiki utafichuliwa, kama huna Ufalme wa MUNGU usioweza kutetemeshwa na majira wala nyakati) na wewe unaweza kutikiswa, kaa ndani ya Ufalme uwe salama. .....Basi kwa kuwa tunapokea UFALME usioweza KUTETEMESHWA,... .....Ebrania 12:28... 1. (d). MAJIRA YA MASIKA (SPRING SEASON) ....Tutaendelea.... Rejea “Therefore, since we receive a KINGDOM which cannot be shaken, let us show gratitude, and offer to GOD pleasing service and acceptable worship with reverence and awe" ....Hebrews 12:28.... Ev. Erasmus Pascrates Kakiza +255 782 546 914 @2024 The year of my shining.❤

  • @witnessmgulisi5559
    @witnessmgulisi5559 Місяць тому

    Ameeen in Jesus Name

  • @agripinamsolomoka
    @agripinamsolomoka Місяць тому

    Amina ❤

  • @agripinamsolomoka
    @agripinamsolomoka Місяць тому

    MUNGU atukuzwe sana

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza Місяць тому

    ❤❤ ❤

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza Місяць тому

    ❤❤❤

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza Місяць тому

    ❤SHUKRANI KWA MUNGU Familia ya Mr&Mrs Erasmus Pascrates Kakiza inamshukuru MUNGU kufikisha miaka 5 ya ndoa takatifu. Tunakushukuru na wewe ambaye umekua baraka kwa kutuombea, kutushauri na kujitoa kwa ajili yetu. MUNGU awabariki sana, MUNGU akubariki sana, Wewe ni baraka.❤

  • @hellenhenry5030
    @hellenhenry5030 Місяць тому

    Mungu wetu ni mwema sana , tunarudisha sifa na utukufu

  • @MaryStellah-zg5uy
    @MaryStellah-zg5uy Місяць тому

    🙏🙏🙏🙏

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza Місяць тому

    Somo: MAJIRA NA NYAKATI ZIMEBEBA MAISHA YAKO °°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°° Fuatilia UA-cam. Https://youtube.com/@Rwizakakiza Sehemu 4: ‭""Kwa KILA JAMBO kuna MAJIRA yake, Na WAKATI kwa KILA KUSUDI chini ya mbingu"" .....Mhubiri 3:1..... JE, NINI MAANA YA MAJIRA NA NYAKATI? 1. MAANA YA , MAJIRA. Baada ya kujifunza nini maana ya majira, Tuanze kuchunguza. Je, majira haya manne kwa mwanadamu kiroho yana maana gani? 1. (b). MAJIRA YA VULI (AUTUMN /FALL SEASON). ......Huu ni msimu maarufu kwa nyakati zake za MAVUNO (Kuacha kutengeneza /kuzalisha chakula), KUGEUZA Majani (Yaani Majani kubadilika na kuanguka), Halijoto ya KUPOEZA (kupunguza joto kali), USIKU wenye GIZA nene na MWANGA mdogo wa jua kwa sababu siku ni fupi. Kuna msemo unaosema.... Mchumia juani, hulia kivulini.... Majira ya vuli kiroho ni kipindi cha mapumziko umetoka juani, kwenye maangaiko sasa unakula ulichopanda (mavuno), Ni kipindi cha utimilifu wa Ahadi za MUNGU, mfano.. .....Jengeni nyumba, mkakae ndani yake, kapandeni bustani, mkale matunda yake; oeni wake, mkazae wana na binti; kawaozeni wake wana wenu, mkawaoze waume binti zenu, wazae wana na binti; mkaongezeke huko wala msipungue. ....Yeremia 29:5-6.... Majira haya ya MAVUNO ni HATARI kuliko vipindi vyote kwa sababu ya STAREHE, maandiko yanaonya kipindi kwa kusema... .....Wakati wasemapo, "Kuna AMANI na SALAMA, NDIPO UHARIBIFU UWAJIAPO kwa GHAFLA, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika HAWATAOKOLEWA"... .....1 Thesalonike 5:3..... Majira ya mavuno, ingawa ni kipindi cha STAREHE, MAPUMZIKO na kujipongeza, tukumbuke kuna hatari kadhaa mfano... i. UZALISHAJI WA CHAKULA UNAPUNGUA. {Kama ulikuwa unaomba sana, unapunguza kuomba, unapunguza kusoma na kutafakari Neno la MUNGU, Ukimya unaacha, kwenda kanisani mpaka uamue sio lazima tena, nk.} ii. MABADILIKO (Majani kugeuka rangi). {Hapa mazingira kukubadilisha ni rahisi (Umepata milioni 500, hatukuoni tena) kuna kujisahau MUNGU alipokutoa, kuanza kuona ulitumia jitihada nyingi kutafuta mafanikio, umesali sana, ulifunga sana ndio maana umefanikiwa. Au umefanya kazi kwa bidii sana, hata tabia, mienendo, lugha ubadilika na kuanza kuchagua watu wa kukaa nao. ....Jihadhari, usije ukamsahau BWANA, MUNGU wako, kwa kutozishika amri zake, na hukumu zake, na sheria zake, Angalia, utakapokuwa UMEKULA na KUSHIBA, na KUJENGA nyumba nzuri na KUKAA ndani yake; Moyo wako USIINUKE, UKAMSAHAU BWANA, MUNGU wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa; .... Kumb 8:11-14.... iii. MAJANI KUANGUKA Ukimsahau MUNGU kwamba upo kwenye kipindi cha mavuno kwa sababu YEYE ndiye amekupa nguvu za mafanikio, hapa anguko lako huja na giza uwa nene kwenye maisha yako, ndio maana nimesema kipindi cha vuli ni hatari sana, lakini usipomsahau MUNGU wako na kujifanyia tathimini binafsi juu ya maisha yako ya kiroho na kimwili na kukumbuka MUNGU alipokutoa, Majira haya ni majira ya raha na furaha sana. 1. (c). MAJIRA YA KIPUPWE (WINTER SEASON). ....Tutaendelea.... Rejea “But you shall remember [with profound respect] the LORD your GOD, for it is He who is giving you power to make wealth, that He may confirm His covenant which He swore (solemnly promised) to your fathers, as it is this day. .....Deuteronomy 8:18.... Ev. Erasmus Pascrates Kakiza +255 782 546 914 @2024 The year of my shining.❤

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza Місяць тому

    Leo ilikuwa siku ya pekee tumemsifu na kumwabudu MUNGU na ametuponya

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza Місяць тому

  • @agripinamsolomoka
    @agripinamsolomoka Місяць тому

  • @agripinamsolomoka
    @agripinamsolomoka Місяць тому

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza Місяць тому

    Somo: MAJIRA NA NYAKATI ZIMEBEBA MAISHA YAKO °°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°° Fuatilia UA-cam. Https://youtube.com/@Rwizakakiza Sehemu 3: ‭""Kwa KILA JAMBO kuna MAJIRA yake, Na WAKATI kwa KILA KUSUDI chini ya mbingu"" .....Mhubiri 3:1..... JE, NINI MAANA YA MAJIRA NA NYAKATI? 1. MAANA YA MAJIRA. Baada ya kujifunza maana ya majira, Tuanze kuchunguza. Je, majira haya manne kwa mwanadamu kiroho yana maana gani? 1. (a). MAJIRA YA KIANGAZI (SUMMER SEASON). .....Haya ni majira yenye joto, jua kali, na mwangaza. Kipindi hiki kiroho kwako cha raha na Furaha, lakini ni kipindi cha kuwa MAKINI zaidi pia. Haya ni majira ya kuangaza, kujulikana, kutambulika na kwa sababu ya Mwanga wako watu wengi watavutiwa na wewe, na kupitia wewe nao watafanikiwa, kama ilivyo majira ya kiangazi. ......Ondoka, UANGAZE; kwa kuwa NURU YAKO imekuja, Na UTUKUFU wa BWANA UMEKUZUKIA. Maana, tazama, GIZA LITAIFUNIKA dunia, Na GIZA KUU LITAZIFUNIKA kabila za watu; Bali BWANA ATAKUZUKIA WEWE, Na utukufu wake utaonekana juu yako. Na MATAIFA WATAIJILIA NURU YAKO, Na wafalme KUUJIA MWANGA wa kuzuka kwako. Utaoona na kutiwa nuru, Na moyo wako utatetemeka na kukunjuka; Kwa kuwa wingi wa bahari utageuzwa KUKUJIA, UTAJIRI wa mataifa UTAKUWASILIA. Na FEDHA yao na DHAHABU yao pamoja NAO, Kwa ajili ya jina la BWANA, MUNGU wako, Kwa kuwa amekutukuza wewe. Na WAGENI WATAJENGA KUTA zako, Na WAFALME wao WATAKUHUDUMU; MALANGO yako nayo YATAKUWA WAZI daima; HAYATAFUNGWA mchana wala usiku; Ili WATU wapate KUKULETEA UTAJIRI wa mataifa, Na WAFALME wao wakiongozwa pamoja nao. Kwa maana kila taifa na ufalme wa watu WASIOTAKA KUKUTUMIKIA WATAANGAMIA; Naam, mataifa hayo wataharibiwa kabisa. Na wana wa watu wale WALIOKUTESA Watakuja kwako na KUKUINAMIA; Nao wote WALIOKUDHARAU WATAJIINAMISHA hata nyayo za miguu yako; Nao watakuita, Mji wa BWANA, Na Badala ya shaba nitaleta dhahabu, Na badala; ya chuma nitaleta fedha, Na badala ya mti, shaba, Na badala ya mawe, chuma; Tena nitawafanya wasimamizi wako wawe amani, Na hao WAKUTOZAO fedha kuwa HAKI. Jeuri haitasikiwa tena katika nchi yako, UKIWA na UHARIBIFU hazitakuwa mipakani mwako; Bali utaziita kuta zako, Wokovu, Na malango yako, Sifa. .....Isaya 60:1-22.... Pamoja na furaha ya kutoa Mwanga, majira haya uwe na tahadhari kwa sababu tunaambiwa, MWANGAZA WAKO, UNAWEZA KUWA FIMBO KWAKO, kwa sababu unaangaza kwenye giza, kuna watu wanafanya mambo yao katika giza hawatapenda kuangaza kwako. Kipindi hiki watu wanaweza kukusema kama ilivyo kipindi cha jua kali watu hulalamika, wanaweza kukusema ili kuzuia mwanga wako. Kumbuka andiko hili MWANGA UNAWEZA KUKUPIGA USIPOKUWA NA TAHADHARI MAJIRA YA KIANGAZI. .....Jua HALITAKUPIGA mchana, WALA mwezi wakati wa usiku. .....Zaburi 121:6.... 1. (b). MAJIRA YA VULI (AUTUMN /FALL SEASON). ....Tutaendelea.... Rejea “NATIONS will come to your LIGHT, And KINGS to the BRIGHTNESS of your RISING" .....Isaiah 60:3.... Ev. Erasmus Pascrates Kakiza +255 782 546 914 @2024 The year of my shining.❤

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza Місяць тому

    Amina

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza Місяць тому

    Somo: MAJIRA NA NYAKATI ZIMEBEBA MAISHA YAKO °°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°° Fuatilia UA-cam. Https://youtube.com/@Rwizakakiza Sehemu 2: ‭""Kwa KILA JAMBO kuna MAJIRA yake, Na WAKATI kwa KILA KUSUDI chini ya mbingu"" .....Mhubiri 3:1..... JE, NINI MAANA YA MAJIRA NA NYAKATI? 1. MAANA YA MAJIRA. Ni msimu au sehemu ya mwaka yenye tabia mbalimbali (hasa tabia nne yaani kiangazi, Kipupwe, Vuli na Masika) katika hali ya hewa kutokana na mzunguko wa dunia kulizunguka jua. Majira haya yanahusiana sana na mwanadamu kiroho, kuna majira kwako yanaweza kuwa kiangazi au yakawa kipupwe au yakawa ya vuli au masika. Na ikumbukwe kila majira yanakaribisha majira mengine yaani Mwisho wa msimu mmoja ni mwanzo wa msimu mwingine. Anza kuchunguza upo kipindi gani itakusaidia kiroho ZINGATIO: Kila mtu lazima majira yakupitie haijalishi umeokoka au hujaokoka, haijalishi ni mpagani au unamjua MUNGU, majira HAUTAYAKWEPA. Bora ujifunze na kujua namna ya kupambana. MUNGU anapoleta jambo linakuwa juu ya wote, uwe mwema au mbaya kila mtu ataingia kwenye majira. BWANA YESU alisema hivi .....MUNGU huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. .....Mathayo 5:45.... Narudia, swala la majira na nyakati lazima upite hauwezi kukwepa, lakini tutatofautishwa kwa Neno la MUNGU lililoko ndani yako, kwa mapigo utapita, kwa moto utampimwa. .....Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, YESU KRISTO. Lakini kama mtu AKIJENGA JUU YA MSINGI HUO, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri. Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe UTAIJARIBU KAZI YA KILA MTU, ni ya namna gani. Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake IKIKAA, atapata THAWABU. Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto. ......1 Kor 3:11-15.... Cha ajabu hata Wakristo wenyewe watapita ingawa amejenga juu ya KRISTO, Inategemea umejenga na nini, kama umejenga kwa nyasi au dhahabu vyote vitapimwa kwa moto. .....Kwa sababu kila mtu atatiwa chumvi kwa moto. .....Marko 9:49..... Tuanze kuchunguza. Je, majira haya manne kwa mwanadamu kiroho yana maana gani? 1.(a). MAJIRA YA KIANGAZI. ....Tutaendelea.... Rejea “For everyone will be salted with fire 🔥" ......Mark 9:49..... Ev. Erasmus Pascrates Kakiza +255 782 546 914 @2024 The year of my shining.

  • @agripinamsolomoka
    @agripinamsolomoka Місяць тому

    MUNGU mkuu ❤

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza Місяць тому

    MUNGU awabariki sana ❤

  • @Rwizakakiza
    @Rwizakakiza Місяць тому

    Somo: MAJIRA NA NYAKATI ZIMEBEBA MAISHA YAKO °°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°° Fuatilia UA-cam. Https://youtube.com/@Rwizakakiza ‭""Kwa KILA JAMBO kuna MAJIRA yake, Na WAKATI kwa KILA KUSUDI chini ya mbingu"" .....Mhubiri 3:1..... Sehemu 1: Tunapoanza Utangulizi somo hili la "MAJIRA NA NYAKATI ZIMEBEBA MAISHA YAKO" tunataka kujenga uelewa wa kupata kilichopo ndani ya majira na kuenenda na kilichobebwa ndani ya wakati huo. Majira yakipita utambue wazi hata kilichopo ndani ya wakati huo kimepita na uwe na uhakika kusudi halitatimilika maana kusudi limefungwa ndani ya muda. Je andiko hili kiongozi kwenye Mada hii, linalosema .....Kwa KILA JAMBO kuna MAJIRA yake, Na WAKATI kwa KILA KUSUDI chini ya mbingu....linalenga kutuambia nini hasa?. Ni hivi .....Mazingira mbalimbali tunayopitia maishani hayatokani na tukio tu, bali yametungwa au kuruhusiwa na MUNGU kwa kusudi kubwa na kwa Umakini..... Hivyo mambo yanayotokea sio bahati mbaya yanaruhusiwa kwa kusudi maalum, tukio liwe baya au liwe jema linaruhusiwa na MUNGU ila chanzo cha tukio kinaweza kisitoke kwa MUNGU lakini kikaruhusiwa na MUNGU. Nataka ujenge uelewa kwamba jambo kuruhusiwa na MUNGU, haimaanishi limeanzishwa au limeletwa na MUNGU, ingawa MUNGU anaweza kurihusu akiwa na uhakika kwamba wewe unaliweza, lakini kwa upande wako wewe wakati huo Huelewi unaweza kuona ni mateso, ni maangaiko, MUNGU hakupendi kakuacha nk. Ebu fikiri Ayubu anapitia Majaribu ambayo kwake yalikuwa au yalionekana ni mateso, lakini ikumbuke chanzo cha mateso ni shetani, na MUNGU alimruhusu shetani ampige Ayubu, Na kusudi la MUNGU kumruhusu shetani, ni kwamba MUNGU alijivuna Ayubu kwa sababu MUNGU alijua Ayubu hawezi kumuasi MUNGU wake. .....Ayubu 1:6 - 2:10.... Mfano wa pili MUNGU hakumuumba mwanadamu afe, bali alimuumba aishi daima, lakini alipokubali kishawishi cha shetani akatenda dhambi, ukawa ndio mwazo wa mauti (kifo) kuingia kwa mtu na ulimwengu mzima ukawa chini ya utawala wa shetani. Lakini nyakati zilipotimia, MUNGU akamtuma YESU KRISTO kwa ajili ya ukombozi wa ulimwengu. Mpaka sasa tupo nyakati za neema yaani nyakati za wokovu, lakini haimaanishi watu wote ulimwenguni wameokoka, la hasha!. Lakini wokovu umefungwa ndani ya maisha ya mtu anayoishi ndio maana umewekewa uchaguzi (Ufalme wa MUNGU au Ufalme wa giza). Je nini maana ya NYAKATI na majira? ....Tutaendelea.... Rejea “There is a season (a time appointed) for everything and a time for every delight and event or purpose under heaven .....Ecclesiastes 3:1.... Ev. Erasmus Pascrates Kakiza +255 782 546 914 @2024 The year of my shining.❤

  • @felixmushi3354
    @felixmushi3354 Місяць тому

    MUNGU AKUBARIKI sana Kwa hii Kazi ... Tunabarikiwa sana

    • @Rwizakakiza
      @Rwizakakiza Місяць тому

      Amina MUNGU akubariki sana kwa kufuatilia TUMAINI JIPYA DUNIANI TV